Sunday 21 October 2012

Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

Ngapula,
Kwani kinyume cha mfumo Kristo ni mfumo Islam?
Sisi tunapinga mnavyotubagua kwa kutumia mfumo wenu huo na naomba watu wasilichanganye hili na secularity ni vitu viwili kabisa.
South Africa walikuwa wanapinga apartheid na walikuwa Waislam kwani? Rwanda wakati wa Jeneral Juvenari Habyarimana kulikuwa na ubaguzi wa kabila nayo vipi walikuwa wanapinga Western Civilization?
Tunapinga Mfumo Kristo ambao ni ubaguzi hatupingi huo Umagharibi wenu.Msipotoshe hili.



Walewale



From: Godfrey Ngupula <ngupula@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, October 21, 2012 8:23 PM
Subject: RE: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam



napenda ungezipinga hoja.Useme wav wanaopinga mfumo Kristo wana maana gani na wanataka mfumo gani.Rejea pia matakwa 30 ya waislam
ktk katiba mpya na useme kama hayo yakikubaliwa ni nini kitatokea?
Useme pia kabla ya uislam kuingia moroco,tunisia na misri zilikuwepo dini gani na nini kilitokea? Hayo uliyauliza ya kuhusu osama,taliban,na sadam hussein nayajua yote,but sijui yanahusiana vipi na mazungumzo haya.Jibu hoja rafiki,jazba ktk maandisha itakupotezea mwelekeo.
hivi,kuna mkristo gani ambaye amehoji uhalali wa waislam kudominate zanzibar?can u change history kwa porojo?Ngupula.
------------------------------
On Sun, Oct 21, 2012 7:58 PM EEST Mobhare Matinyi wrote:

>
>Chamani,Fanya hisani moja kubwa: Toa maelezo ya maswali yote hayo uliyouliza ili mbishani wako aelimike; usiishie kumpiga mkwara tu. Toa somo Maalim.Katika somo lako jadili hali ya dini ilivyo Irak, Uturuki, Iran na kote huko ukigusia watu wasiokuwa Waislamu huwa wanafanywa nini. Usiiache Misri.Toa somo Yakhe.Matinyi.
> Date: Sun, 21 Oct 2012 09:40:49 -0700
>From: abachamani@yahoo.com
>Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>To: wanabidii@googlegroups.com
>
>Ngupula,Usilete komedi humu.Angalia isijekuwa wewe ndiyo mlemavu wa kufikiri wakati wenzio ni wavivu tu.Unazungumza uzushi wenu OIC hapa unakusaidia nini.Misri na Moroco kimefanyika nini mbona pilipili usiyokula ina kuwasha?Unafurahiya mauaji yanayofanyika Mashariki ya Kati kwa jina la Yesu na ndiyo maana siku hizi hata bendera ya USA na Israel mnaitumia kwenye nyumba za ibada.Unamjua vema Sadam Husein na uhusiano wake na USA na UK baada ya mapinduzi ya Iran 1979?Unajua uhusiano wa Usama na USA wakati wa kupambana na USSR Afghanistan na je unajua uhusiano wa TALEBAN na USA walipokuwa na mpango wa kupitisha gesi nchini mwao?Angalia kaka usidandie gari kwa mbele
> utaumia.Jitahidi kufikiri usiwe mlemavu wa kufikiri.
>
>
>
>Walweale.
>        From: Godfrey Ngupula <ngupula@yahoo.co.uk>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Sunday, October 21, 2012 6:40 PM
> Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

>
>unajua sometimes nawaza hawa wanaosema wanapigana na mfumo Kristo tanzania je wanataka mfumo gani kama mbadala wa huo wanaosema mfumo kristo? Ktk uchunguz wangu kwa kuangalia matendo na maneno ya watu hao,nimegundua kuwa wanachotaka watu hao ni mfumo islam.Na wangelifurah sana kama sharia ingeshika ktk utawala wa kiserikali. Na matukio haya ni moja ya agenda za kikao kilichofanyika
> Abuja Nigeria ili kugeuza nchi za kusini mwa jangwa la saharah zote ziwe za kiislam.Hivyo basi hii ni vita.Ni vita ya kuleta mageuzi ya kiislam Tanzania.Na kama wakristo wakizembea,hawa jamaa wakapata nguvu zaidi ya hii waliyokuwa nayo,wale wote wasiokubaliana nao watauawa.Na hatimaye bila kipingamiz chochote tz itabadilika kuwa dola ya kiislam.Wanachotaka kufanya waislam ndicho kilichofanyika ktk nchi ya misri,moroco,tunisia,nk.
>Swali langu kwa waislam je ni nani asiyejua kuwa mwenye bajeti ndiye hushika dola?.ni nani anayeendesha bajeti ya Tz kama si germany,norway,sweden,australia,canada,uk na usa?kwa minajili hii ni nani anayeweza kuipinga mising ya kimagharibi?Taliban,Al-queda,al-shabab ,boko haram wote wameshindwa.Osama ameambulia kifo tu.Sadam ndo usiseme.Ona kitachotokea iran hiv karibuni. Mim binafsi,ningependa niwashauri waislam wanajoina wana Mungu zaidi ya wengine,watulie tu wajitafutie maendeleo yao.adui yao ni uvivu,ujinga na umasikini
> wa kufikiri..waogope sana mtu mwenye akili na aliye kimya.Watu wako kimya wanaangalia tu mchezo unavyochezwa na wanajua nini cha kufanya. Ngupula
>
>
>------------------------------
>On Sun, Oct 21, 2012 6:03 PM EEST Hosea Ndaki wrote:
>
>>Kule Zenj, wapo wakatoliki, wanglikana na wapentekoste lakini
>>wamekandamizwa kweli, hakuna hata mbunge mkristo! bado tu wanawachomea na
>>makanisa! Hapana kuna haja ya kufikiria upya uhusiano huu na wenzetu.
>>Pamoja na malumbano haya mtoto mdogo wa miaka 13 anasota rumande kwa ujinga
>>tu! wala hatujui kama yuko rumande ya watoto au wakubwa!
>>
>>
>>2012/10/21 Willy Makundi <wrlmakundi@aol.com>
>>
>> Jee tunaweza kusema serikali ni ya mfumo Nabii Issa unayoongozwa na *Dr
>> Jakaya Mrisho Kikwete, Dr Mohamed Bilal**, Dr Ali Mohamed Shein, **Chief
>>
> Justice Mohamed Chande Othman, Mkurugenzi Usalama wa Taifa Rashid Othman,
>> IGP Said Mwema, Minister of Defense Shamsi Vuai Nahodha*, *Chief of Staff
>> Abrahamani Shimbo*, ambao kwa wanaojua mamlaka za serikali, hawa ndicho
>> kiini, ndio moyo, ndio uti wa mgongo wa serikali. Hawa Waislamu wote hawana
>> maslahi ya Waislamu moyoni ila kulelea mfumo Nabii Issa?
>>
>> Binafsi sipendi kuona majina ya miungu na manabii wetu yanatumika kurahisisha
>> maelezo magumu ya mapungufu yetu ya kijamii. Kuna ugumu gani kueleza
>> mapungufu ya mfumo wetu wa utawala bila kuyaficha kwa nabii Issa? Mifumo ya
>> utawala ya magharibi haiwezi kurahisishwa kiasi cha kuipa jina la nabii
>> Issa. Fikiria Israel, India, Japan, Russia nk uone urahisishaji huu
>> unavyopotosha na kutoheshimu miungu na manabii wetu.
>>
>>
>>
> mchilyi7.0
>>
>>
>> -----Original Message-----
>> From: mngonge <mngonge@gmail.com>
>> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
>> Sent: Sun, Oct 21, 2012 5:05 pm
>> Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>>
>> Naungana na mchambuzi wa maadui wa uislamu, kwa mtiririko kwamba adui
>> namba moja inawezekana kabisa ikawa ni elimu. Mimi naongeza kwa kuiita
>> elimu bora na sahihi. Wapo wachangiaji wengi wetu ambao nawajua kwamba
>> wamesoma na wana shahada moja au zaidi lakini bado ndo kwanza kabisa
>> wanaeneza dhana ya mfumo kristo na hivyo kuwapotosha wale wasiokuwa na
>> elimu.
>>
>> Kweli kabisa wakisoma
> na kuelimika vizuri hawataendlea kupotoshwa
>> maana watakuwa na uwezo wa kuchambua mbichi na mbivu. Kwa upande wa
>> wakristu haswa kwa madhebu ya katoliki na KKT si rahisi wahumini
>> kufuata na kutekeleza atakayowaambia padri bila kwanza kulipima na
>> kuona kama lina mashiko au la. Anaweza kusema na wasimjibu kanisani
>> lakini wakishatoka kanisani watayaacha hapo hapo bila kumuunga mkono.
>>
>> Pamoja na ushauri mzuri kwa waislamu juu ya kuongeza na kuboresha
>> shule na vyuo. Nataka niseme kwamba pia wanaokosa elimu bora si
>> waislamu tu ni watanzania kwa ujumla wao. Shule nzuri ata kama ni ya
>> wakristu au waislamu mlalahoi hawezi kupeleka mtoto wake uko. Ukienda
>> Uingereza utawakuta watoto wengi wa kiislamu hasa toka Pemba wakisoma
>> huko katika shule nzuri.  Kama shule na vyuo vya serikali vingekuwa
>> vinatoa elimu
> bora mbona watu wengi wangekuwa wameelimika vilivyo,
>> kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa elimu tunayoitoa kwa vijana
>> wetu. Iwe ni elimu ya kuwasaidia kuchambua jambo kwa akili zao wenyewe
>> na kuweza kupambana na mazingira yanayowazunguka
>>
>> Mwisho ninaomba wale wanaosema seriakli ni ya mfumo kristo
>> watufafanulie zaidi pengine kuna ukweli. Wakitaja tu kwamba serikali
>> ni ya mfumo kristo bila kufafanua si rahisi kuelewa wanchokilalamikia
>>
>> 2012/10/21 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>:
>> > Katika Tanzania hakuna adui wa muislamu wala adui wa dini yoyote ,
>> > Sisi wote ni wamoja , tuendeleze umoja wetu .
>> >
>> > On Oct 21, 4:31 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>> > Ndugu zangu.
>> >
>> > Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani
>> > wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande
>> > wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya
>> > ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita
>> > unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda
>> > kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati
>> > wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye
>> > mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>> >
>> > Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu
>> > wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii
>> >
> dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo
>> > kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu,
>> > wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia
>> > watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo
>> > ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu
>> > zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu
>> > lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni
>> > mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif
>> > hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu
>> > na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata
>> > nikiungalia kwenye wizara na taa

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment