Sunday 21 October 2012

Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

unajua sometimes nawaza hawa wanaosema wanapigana na mfumo Kristo tanzania je wanataka mfumo gani kama mbadala wa huo wanaosema mfumo kristo? Ktk uchunguz wangu kwa kuangalia matendo na maneno ya watu hao,nimegundua kuwa wanachotaka watu hao ni mfumo islam.Na wangelifurah sana kama sharia ingeshika ktk utawala wa kiserikali. Na matukio haya ni moja ya agenda za kikao kilichofanyika Abuja Nigeria ili kugeuza nchi za kusini mwa jangwa la saharah zote ziwe za kiislam.Hivyo basi hii ni vita.Ni vita ya kuleta mageuzi ya kiislam Tanzania.Na kama wakristo wakizembea,hawa jamaa wakapata nguvu zaidi ya hii waliyokuwa nayo,wale wote wasiokubaliana nao watauawa.Na hatimaye bila kipingamiz chochote tz itabadilika kuwa dola ya kiislam.Wanachotaka kufanya waislam ndicho kilichofanyika ktk nchi ya misri,moroco,tunisia,nk.
Swali langu kwa waislam je ni nani asiyejua kuwa mwenye bajeti ndiye hushika dola?.ni nani anayeendesha bajeti ya Tz kama si germany,norway,sweden,australia,canada,uk na usa?kwa minajili hii ni nani anayeweza kuipinga mising ya kimagharibi?Taliban,Al-queda,al-shabab ,boko haram wote wameshindwa.Osama ameambulia kifo tu.Sadam ndo usiseme.Ona kitachotokea iran hiv karibuni. Mim binafsi,ningependa niwashauri waislam wanajoina wana Mungu zaidi ya wengine,watulie tu wajitafutie maendeleo yao.adui yao ni uvivu,ujinga na umasikini wa kufikiri..waogope sana mtu mwenye akili na aliye kimya.Watu wako kimya wanaangalia tu mchezo unavyochezwa na wanajua nini cha kufanya. Ngupula


------------------------------
On Sun, Oct 21, 2012 6:03 PM EEST Hosea Ndaki wrote:

>Kule Zenj, wapo wakatoliki, wanglikana na wapentekoste lakini
>wamekandamizwa kweli, hakuna hata mbunge mkristo! bado tu wanawachomea na
>makanisa! Hapana kuna haja ya kufikiria upya uhusiano huu na wenzetu.
>Pamoja na malumbano haya mtoto mdogo wa miaka 13 anasota rumande kwa ujinga
>tu! wala hatujui kama yuko rumande ya watoto au wakubwa!
>
>
>2012/10/21 Willy Makundi <wrlmakundi@aol.com>
>
>> Jee tunaweza kusema serikali ni ya mfumo Nabii Issa unayoongozwa na *Dr
>> Jakaya Mrisho Kikwete, Dr Mohamed Bilal**, Dr Ali Mohamed Shein, **Chief
>> Justice Mohamed Chande Othman, Mkurugenzi Usalama wa Taifa Rashid Othman,
>> IGP Said Mwema, Minister of Defense Shamsi Vuai Nahodha*, *Chief of Staff
>> Abrahamani Shimbo*, ambao kwa wanaojua mamlaka za serikali, hawa ndicho
>> kiini, ndio moyo, ndio uti wa mgongo wa serikali. Hawa Waislamu wote hawana
>> maslahi ya Waislamu moyoni ila kulelea mfumo Nabii Issa?
>>
>> Binafsi sipendi kuona majina ya miungu na manabii wetu yanatumika kurahisisha
>> maelezo magumu ya mapungufu yetu ya kijamii. Kuna ugumu gani kueleza
>> mapungufu ya mfumo wetu wa utawala bila kuyaficha kwa nabii Issa? Mifumo ya
>> utawala ya magharibi haiwezi kurahisishwa kiasi cha kuipa jina la nabii
>> Issa. Fikiria Israel, India, Japan, Russia nk uone urahisishaji huu
>> unavyopotosha na kutoheshimu miungu na manabii wetu.
>>
>>
>> mchilyi7.0
>>
>>
>> -----Original Message-----
>> From: mngonge <mngonge@gmail.com>
>> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
>> Sent: Sun, Oct 21, 2012 5:05 pm
>> Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>>
>> Naungana na mchambuzi wa maadui wa uislamu, kwa mtiririko kwamba adui
>> namba moja inawezekana kabisa ikawa ni elimu. Mimi naongeza kwa kuiita
>> elimu bora na sahihi. Wapo wachangiaji wengi wetu ambao nawajua kwamba
>> wamesoma na wana shahada moja au zaidi lakini bado ndo kwanza kabisa
>> wanaeneza dhana ya mfumo kristo na hivyo kuwapotosha wale wasiokuwa na
>> elimu.
>>
>> Kweli kabisa wakisoma na kuelimika vizuri hawataendlea kupotoshwa
>> maana watakuwa na uwezo wa kuchambua mbichi na mbivu. Kwa upande wa
>> wakristu haswa kwa madhebu ya katoliki na KKT si rahisi wahumini
>> kufuata na kutekeleza atakayowaambia padri bila kwanza kulipima na
>> kuona kama lina mashiko au la. Anaweza kusema na wasimjibu kanisani
>> lakini wakishatoka kanisani watayaacha hapo hapo bila kumuunga mkono.
>>
>> Pamoja na ushauri mzuri kwa waislamu juu ya kuongeza na kuboresha
>> shule na vyuo. Nataka niseme kwamba pia wanaokosa elimu bora si
>> waislamu tu ni watanzania kwa ujumla wao. Shule nzuri ata kama ni ya
>> wakristu au waislamu mlalahoi hawezi kupeleka mtoto wake uko. Ukienda
>> Uingereza utawakuta watoto wengi wa kiislamu hasa toka Pemba wakisoma
>> huko katika shule nzuri. Kama shule na vyuo vya serikali vingekuwa
>> vinatoa elimu bora mbona watu wengi wangekuwa wameelimika vilivyo,
>> kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa elimu tunayoitoa kwa vijana
>> wetu. Iwe ni elimu ya kuwasaidia kuchambua jambo kwa akili zao wenyewe
>> na kuweza kupambana na mazingira yanayowazunguka
>>
>> Mwisho ninaomba wale wanaosema seriakli ni ya mfumo kristo
>> watufafanulie zaidi pengine kuna ukweli. Wakitaja tu kwamba serikali
>> ni ya mfumo kristo bila kufafanua si rahisi kuelewa wanchokilalamikia
>>
>> 2012/10/21 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>:
>> > Katika Tanzania hakuna adui wa muislamu wala adui wa dini yoyote ,
>> > Sisi wote ni wamoja , tuendeleze umoja wetu .
>> >
>> > On Oct 21, 4:31 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>> > Ndugu zangu.
>> >
>> > Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani
>> > wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande
>> > wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya
>> > ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita
>> > unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda
>> > kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati
>> > wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye
>> > mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>> >
>> > Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu
>> > wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii
>> > dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo
>> > kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu,
>> > wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia
>> > watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo
>> > ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu
>> > zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu
>> > lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni
>> > mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif
>> > hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu
>> > na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata
>> > nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.
>> >
>> > Wanao ongela mfumo kristo hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha
>> > madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na
>> > ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana
>> > wa jua kali.
>> >
>> > Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa
>> > waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine
>> > zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.
>> >
>> > Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na
>> > kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia
>> > za amani kupata suluhu.
>> > Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.
>> >
>> > 1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi
>> > vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande
>> > wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana
>> > lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa
>> > mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani
>> > ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa
>> > masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza
>> > harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri
>> > walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanao
>> > endana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya
>> > ushindani na pia viongozi bora wa dini.
>> >
>> > 2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya ccm kupata uhalali wa kutawala kwa
>> > kura za waislamu. Lazima tujue kuwa ccm wametutumia vya kutosha na
>> > kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya
>> > swala la mahakama ya kadhi wakati wa kampeni 2010 waislamu waliotaka
>> > tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya ccm wakapiga kura za kuhadaiwa lakini
>> > baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa
>> > kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho hakita tugawa lakini pia
>> > ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.
>> >
>> > 3.Bakwata imekuwa ni kama taasisi ya ccm, wanamuweka wanaye taka wao.
>> > Lazima tupiganie bakwata kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke
>> > viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia
>> > kurejesha imani kwa bakwata. Napendekeza Qualification ya kuongoza
>> > Bakwata iwe ni pdh kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia
>> > lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu
>> > cha mum kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji
>> > wengine wa bakwata ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe
>> > shahada moja na kuendelea.
>> >
>> > 4.Kutokufuata mafundisho ya mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa
>> > mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na
>> > kukumbushana mema na kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye
>> > misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya.
>> > Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha
>> > Mungu, uka

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment