Sunday 21 October 2012

Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

bwana Chamani,mfano wa India unaeleweka. Anachokisema ni hiki,tatizo la udini linalobebelewa na waislam hapa kwetu linakuwa kubwa kwa kuwa ni njaa ndio inayosumbua.Wangekuwa na shibe,hiyo isingekuwa shida.Na akatolea pia mfano wa indonesia. Mim pia naungana naye kwa asilimia 90.Kwani,tulijua kuwa kwa kadri ya gape ya watu wa kipato cha chini na cha juu linapoongeza ingeleta shida baadae.Lkn,watu wazembe wa kuwaza wameugeuza mgogoro huu na kuufanya uwe wa kidini kwa maslah yao.Suprisingly,hata wasomi nao wanashawishiwa na hao al_shababu type2.And.wanataka waangaliwe tu wafanye watakavyo.How?ngupula



------------------------------
On Sun, Oct 21, 2012 8:33 PM EEST amour chamani wrote:

>Matinyi,
>Aya ya kwanza sijakuelewa.Nadhani kuna tyiping error.
>
>Elimu yangu niya Madrasa.Kusaidia kashindwa poti kwa miaka yake 24 nitaweza mie.
>
>Mfano wako wa India unahusiana vipi na tunachosema? Kwahiyo tatizo la Waislam wa Tanzania ni nini? maana sasa wewe unakuja na doctrine mpya kabisa au ndiyo tunatoana kwenye mada ndugu yangu.
>
>
>
>
>________________________________
> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
>To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
>Sent: Sunday, October 21, 2012 8:11 PM
>Subject: RE: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>
>
>
>Chamani,

>Hata kwenye nchi zenye Waislamu 99% au zaidi malalamiko huwa ni haya haya - tunataka serikali ya kiislamu. Na ikiwepo ya kiislamu yanazuka malalamiko mengine kwamba haina uislamu wa kweli. Kuna mahali nimeona watu wakidai kwamba hata marais watano wa Tanzania wote ni waislamu na kisha wakataja vyeo vingine kibao - je, ulitaka na wewe upewe? 

>Dawa ya yote haya ni elimu - watu wakiwa na elimu hawatakimbilia kazi za serikali ambazo mishahara yake ni midogo mno ukilinganisha na kwenye kampuni binafsi. Chamani unafahamu kuwa mtu mwenye shahada moja ya uhandisi akiajiriwa kwenye sekta binafsi anamzunguka mhandisi wa serikali karibu mara tano? Hivi wewe mwenyewe Chamani hebu tueleze, una utaalamu na elimu kiasi gani na unafanya nini na umehawahi kuwasaidia wangapi na wao wapate elimu dunia?

>Unajua kwamba India ni taifa la pili duniani kwa kuwa na Waislamu wengi baada ya Indonesia? Unajua kwa nini wao hawana matatizo na hawalalamiki? Hebu tafuta uone. Huko Indonesia mwaka 2000 Waislamu waliwaua Wachina maelfu kwa madai kama yako kwenye upande wa uchumi (siyo siasa kama Tanzania) lakini ukweli ukabaki pale pale, kwamba wenzao wanachapa kazi na wao wanalalamika tu isipokuwa familia ya rais na washikaji zake ndio waliokuwa na ukwasi wa kutisha. Ipo mifano mingi ila wasiwasi ni kwamba Chamani husomi habari za dunia wala vitabu vya utafiti, kazi kulalama tu na kujenga chuki.

>Matinyi.

>
>
>________________________________
>Date: Sun, 21 Oct 2012 09:28:44 -0700
>From: abachamani@yahoo.com
>Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
>Peter,
>Tunataka serikali isiyoegemea upande wowote wa dini kwani hii nchi si ya dini yoyote.
>
>
>Walewale.
>
>
>
>________________________________
> From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Sent: Sunday, October 21, 2012 6:35 PM
>Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>
>
>Mfumo wowote una malengo, viongozi na sifa zake. Waacheni watwambie malengo, viongozi na sifa za mfumo kristo ni zipi? Msiwalishe maneno. Badala yake watwambie wanataka mfumo gani?
>Lwega.
>
>
>------------------------------
>On Sun, Oct 21, 2012 7:41 AM PDT Willy Makundi wrote:
>
>>Jee tunaweza kusema serikali ni ya mfumo Nabii Issa unayoongozwa na Dr Jakaya Mrisho
> Kikwete, Dr Mohamed Bilal, Dr Ali Mohamed Shein, Chief Justice Mohamed Chande Othman, Mkurugenzi Usalama wa Taifa Rashid Othman, IGP Said Mwema, Minister of Defense Shamsi Vuai Nahodha, Chief of Staff Abrahamani Shimbo, ambao kwa wanaojua mamlaka za serikali, hawa ndicho kiini, ndio moyo, ndio uti wa mgongo wa serikali. Hawa Waislamu wote hawana maslahi ya Waislamu moyoni ila kulelea mfumo Nabii Issa?
>>
>>Binafsi sipendi kuona majina ya miungu na manabii wetu yanatumika kurahisisha maelezo magumu ya mapungufu yetu ya kijamii. Kuna ugumu gani kueleza mapungufu ya mfumo wetu wa utawala bila kuyaficha kwa nabii Issa? Mifumo ya utawala ya magharibi haiwezi kurahisishwa kiasi cha kuipa jina la nabii Issa. Fikiria Israel, India, Japan, Russia nk uone urahisishaji huu unavyopotosha na kutoheshimu miungu na manabii wetu.
>>
>>
>>mchilyi7.0
>>
>>
>>
>>
>>-----Original Message-----
>>From: mngonge <mngonge@gmail.com>
>>To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
>>Sent: Sun, Oct 21, 2012 5:05 pm
>>Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>>
>>
>>Naungana na mchambuzi wa maadui wa uislamu, kwa mtiririko kwamba adui
>>namba moja inawezekana kabisa ikawa ni elimu. Mimi naongeza kwa kuiita
>>elimu bora na sahihi. Wapo wachangiaji wengi wetu ambao nawajua kwamba
>>wamesoma na wana shahada moja au zaidi lakini bado ndo kwanza kabisa
>>wanaeneza dhana ya mfumo kristo na hivyo kuwapotosha wale wasiokuwa na
>>elimu.
>>
>>Kweli kabisa wakisoma na kuelimika vizuri hawataendlea kupotoshwa
>>maana watakuwa na uwezo wa kuchambua mbichi na mbivu. Kwa upande wa
>>wakristu haswa kwa madhebu ya
> katoliki na KKT si rahisi wahumini
>>kufuata na kutekeleza atakayowaambia padri bila kwanza kulipima na
>>kuona kama lina mashiko au la. Anaweza kusema na wasimjibu kanisani
>>lakini wakishatoka kanisani watayaacha hapo hapo bila kumuunga mkono.
>>
>>Pamoja na ushauri mzuri kwa waislamu juu ya kuongeza na kuboresha
>>shule na vyuo. Nataka niseme kwamba pia wanaokosa elimu bora si
>>waislamu tu ni watanzania kwa ujumla wao. Shule nzuri ata kama ni ya
>>wakristu au waislamu mlalahoi hawezi kupeleka mtoto wake uko. Ukienda
>>Uingereza utawakuta watoto wengi wa kiislamu hasa toka Pemba wakisoma
>>huko katika shule nzuri.  Kama shule na vyuo vya serikali vingekuwa
>>vinatoa elimu bora mbona watu wengi wangekuwa wameelimika vilivyo,
>>kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa elimu tunayoitoa kwa vijana
>>wetu. Iwe ni elimu ya kuwasaidia kuchambua jambo kwa akili zao wenyewe
>>na kuweza
> kupambana na mazingira yanayowazunguka
>>
>>Mwisho ninaomba wale wanaosema seriakli ni ya mfumo kristo
>>watufafanulie zaidi pengine kuna ukweli. Wakitaja tu kwamba serikali
>>ni ya mfumo kristo bila kufafanua si rahisi kuelewa wanchokilalamikia
>>
>>2012/10/21 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>:
>> Katika Tanzania hakuna adui wa muislamu wala adui wa dini yoyote ,
>> Sisi wote ni wamoja , tuendeleze umoja wetu .
>>
>> On Oct 21, 4:31 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>> Ndugu zangu.
>>
>> Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani
>> wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande
>> wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye
> na ni nusu ya
>> ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita
>> unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda
>> kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati
>> wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye
>> mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>>
>> Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu
>> wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii
>> dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo
>> kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu,
>> wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia
>> watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo
>> ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na
> ndugu
>> zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu
>> lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni
>> mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif
>> hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu
>> na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata
>> nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.
>>
>> Wanao ongela mfumo kristo hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha
>> madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na
>> ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana
>> wa jua kali.
>>
>> Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa
>> waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine
>> zinazopatikana kwenye huu
> ulimwengu.
>>
>> Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na
>> kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia
>> za amani kupata suluhu.
>> Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.
>>
>> 1. Adui

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment