Sunday 21 October 2012

Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

Naungana na mchambuzi wa maadui wa uislamu, kwa mtiririko kwamba adui
namba moja inawezekana kabisa ikawa ni elimu. Mimi naongeza kwa kuiita
elimu bora na sahihi. Wapo wachangiaji wengi wetu ambao nawajua kwamba
wamesoma na wana shahada moja au zaidi lakini bado ndo kwanza kabisa
wanaeneza dhana ya mfumo kristo na hivyo kuwapotosha wale wasiokuwa na
elimu.

Kweli kabisa wakisoma na kuelimika vizuri hawataendlea kupotoshwa
maana watakuwa na uwezo wa kuchambua mbichi na mbivu. Kwa upande wa
wakristu haswa kwa madhebu ya katoliki na KKT si rahisi wahumini
kufuata na kutekeleza atakayowaambia padri bila kwanza kulipima na
kuona kama lina mashiko au la. Anaweza kusema na wasimjibu kanisani
lakini wakishatoka kanisani watayaacha hapo hapo bila kumuunga mkono.

Pamoja na ushauri mzuri kwa waislamu juu ya kuongeza na kuboresha
shule na vyuo. Nataka niseme kwamba pia wanaokosa elimu bora si
waislamu tu ni watanzania kwa ujumla wao. Shule nzuri ata kama ni ya
wakristu au waislamu mlalahoi hawezi kupeleka mtoto wake uko. Ukienda
Uingereza utawakuta watoto wengi wa kiislamu hasa toka Pemba wakisoma
huko katika shule nzuri. Kama shule na vyuo vya serikali vingekuwa
vinatoa elimu bora mbona watu wengi wangekuwa wameelimika vilivyo,
kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa elimu tunayoitoa kwa vijana
wetu. Iwe ni elimu ya kuwasaidia kuchambua jambo kwa akili zao wenyewe
na kuweza kupambana na mazingira yanayowazunguka

Mwisho ninaomba wale wanaosema seriakli ni ya mfumo kristo
watufafanulie zaidi pengine kuna ukweli. Wakitaja tu kwamba serikali
ni ya mfumo kristo bila kufafanua si rahisi kuelewa wanchokilalamikia

2012/10/21 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>:
> Katika Tanzania hakuna adui wa muislamu wala adui wa dini yoyote ,
> Sisi wote ni wamoja , tuendeleze umoja wetu .
>
> On Oct 21, 4:31 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>> Ndugu zangu.
>>
>> Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani
>> wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande
>> wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya
>> ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita
>> unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda
>> kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati
>> wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye
>> mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>>
>> Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu
>> wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii
>> dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo
>> kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu,
>> wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia
>> watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo
>> ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu
>> zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu
>> lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni
>> mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif
>> hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu
>> na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata
>> nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.
>>
>> Wanao ongela mfumo kristo hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha
>> madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na
>> ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana
>> wa jua kali.
>>
>> Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa
>> waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine
>> zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.
>>
>> Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na
>> kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia
>> za amani kupata suluhu.
>> Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.
>>
>> 1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi
>> vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande
>> wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana
>> lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa
>> mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani
>> ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa
>> masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza
>> harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri
>> walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanao
>> endana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya
>> ushindani na pia viongozi bora wa dini.
>>
>> 2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya ccm kupata uhalali wa kutawala kwa
>> kura za waislamu. Lazima tujue kuwa ccm wametutumia vya kutosha na
>> kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya
>> swala la mahakama ya kadhi wakati wa kampeni 2010 waislamu waliotaka
>> tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya ccm wakapiga kura za kuhadaiwa lakini
>> baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa
>> kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho hakita tugawa lakini pia
>> ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.
>>
>> 3.Bakwata imekuwa ni kama taasisi ya ccm, wanamuweka wanaye taka wao.
>> Lazima tupiganie bakwata kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke
>> viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia
>> kurejesha imani kwa bakwata. Napendekeza Qualification ya kuongoza
>> Bakwata iwe ni pdh kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia
>> lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu
>> cha mum kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji
>> wengine wa bakwata ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe
>> shahada moja na kuendelea.
>>
>> 4.Kutokufuata mafundisho ya mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa
>> mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na
>> kukumbushana mema na kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye
>> misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya.
>> Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha
>> Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya
>> tutawaepuka wale wanao utumia uislamu wetu kama daraja ambalo baadae
>> hutuchafua wote. Mfano wale walio ingia kuchoma na kuvunja kanisa na
>> kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya kanisa na mikate.
>>
>> "Uislamu ni unadhifu" hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu
>> kipenzi Muhammad S. W. A. Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili
>> tumuenzi kipenzi chetu.
>>
>> Wakatabahu.
>>
>> On Oct 21, 1:46 pm, Magiri paul <kiga...@gmail.com> wrote:
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>> > Ndugu zangu.
>>
>> > Tunapokuwa tunajiuliza mhemuko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha
>> > na kuuasisi, si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu Waislamu.
>> > Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya
>> > kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au
>> > mfumo kristo kama wengine wanavyopenda kuita (Mimi sio muumini wa
>> > dhana ya *mfumo
>> > Kristo*) maana nimeona wakati wote Waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa
>> > Serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>>
>> > Siuoni *mfumo Kristo* kama unavyoitwa au kama baadhi ya Waislamu wenzangu
>> > wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa Kiislamu juu ya hii dhana.
>>
>> >http://wotepamoja.com/archives/9392#.UIPSVsPwbyY.gmail
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment