Saturday 20 October 2012

RE: [wanabidii] Neno La Leo: Udini Ndipo Ulipo Ubovu Kwenye Kamba Inayotuunganisha Watanzania

Historia hujirudia. Dini ni vyombo vya kiutawala. Ujinga ni fursa kwa mtawala katika ngazi yoyote. Hata mume humbadilisha mke jina ili amtawale. Mataifa ya mashariki hutumia uisilamu na ujinga wetu kututawala. Mataifa ya magharibi hutumia dini na ujinga wetu kututawala. Walifanya hivyo enzi ya ukoloni wa mwanzo na wana fanya hivyo enzi ya ukoloni wa sasa. Ufahamu wetu mdogo umeletelezwa na mfumo mbovu wa elimu nchini, wenye uwezo wa kusoma na kuwa watetezi wanaachwa, wanachukuliwa chinja chinja na waporaji wa rasilimali. Watawala wa ndani na nje wamegundua kuwa Watanzania tuko usingizini na wakaitafakari methali;’Usimwamshe aliye lala…….’ Mwalimu alisema ni lazima tukimbie wakati mataifa kandamizi wakitembea. Akatoa elimu bora na bure kwa wote, mpaka chuo kikuu. Mataifa yalipogeuka nyuma na kuona mbio zetu , walichokifanya na wanachoendelea kufanya ndio hiki!!!Wakatushauri kuanzisha na kuendesha mifumo ya kutujaza hasira, huduma za msangi zikafa taratibu elimu ikafishwa zaidi na sasa inauzwa, ajira zikafa, vijana wakapandwa na hasira nyingi vijiweni, matokeo ndiyo haya sasa , kuchijana kwenda mbele. Kama vijana wangesomeshwa vizuri wakapewa ajira wangepata wapi muda wa kupoteza na kuanza kuchinja watu hovyo hoyo? Tafakari na Chukua hatua!!!!!!!!!!!!!

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Tony PT
Sent: Sunday, October 21, 2012 8:47 AM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Neno La Leo: Udini Ndipo Ulipo Ubovu Kwenye Kamba Inayotuunganisha Watanzania

 

Maggid,

Salaam,

Naona umejitahidi sana kueleza hali ya sasa na ya hapo awali. Umetoa mifano mizuri sana, lakini ulichoshau ni kutueleza nini kiliwatokea wale wote waliotaka kuendekeza au kuhubiri chuki za udini, ukabila n.k. Jibu ninalolijua ni kuwa walishughulikiwa na wakati mwingine kupelekwa "internal exile", Mtwara, Mafia n.k.

Je, swali la kujiuliza, bado tuna uwezo huo kushughulikia akina Ponda na wengine kama enzi za Mwl Nyerere? Pili unaweza kusema nini juu ya sheria zilizotokana na tume ya Jaji Nyalali, zilizoleta haki za binadamu, kuondoa makosa ya mkusanyiko n.k? Utakataa kukubali kuwa mabadiliko haya yaliyofanyika kwa nia nzuri nayo yanachangia mmomonyoko huu wa mambo ya utawala unaolenga "usisi" kushamiri hapa nchini?

Naona tunatafuta sababu ambazo sio za msingi kwenye jamii. Jamii ni mfumo wa makuzi na makatazo yanayolenga kuogopesha na kuzuia mtu aliadhibiwe na jamii husika. Inavyoonyesha, huenda demokrasia yetu ilitakiwa kuwa na utofauti na ile ya mataifa ya magharibi, au kutumika polepole kwa kuzingatia elimu na uwezo wa kujiamini kwa watu wetu.

Demokrasia ya magharibi imeingizwa kwenye jamii yetu huenda kwa kasi mno na huenda haya yote tunayoyaona kwa sasa ni msituko wa mabadiliko ya haraka ya mila, desturi na ustaarabu wetu.

Tafakari!

Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.


From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>

Sender: wanabidii@googlegroups.com

Date: Sun, 21 Oct 2012 06:26:41 +0100

To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>

ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com

Subject: [wanabidii] Neno La Leo: Udini Ndipo Ulipo Ubovu Kwenye Kamba Inayotuunganisha Watanzania

 

Ndugu zangu, 

Wahenga walisema; Kamba hukatikia pabovu. Na siku zote, uzoefu ni mwalimu mzuri sana. Mathalan, uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana. 

Ona, moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza kijiji kizima. Na tangu utotoni tumetahadharishwa hatari ya kucheza na moto. 
Naam, binadamu usicheze na moto, labda iwe kwenye mazingaombwe. 

Ndugu zangu,
Jumapili hii ya leo ningependa sana tuyakumbuke maneno ya busara na hekima nyingi kutoka kwa Bi. Joy Mukanyange. Huyu alikuwa Balozi wa zamani wa Rwanda nchini Tanzania. Mama huyu aliyatamka maneno haya miaka 13 iliyopita,  takribani miezi sita kabla ya kifo cha Baba wa Taifa. Bi. Joy Mukanyange ( Pichani juu) alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona. Ni kama vile alikuwa mtabiri, maana, alichokisema mama yule leo ndio tunaanza kukiona. Siku ile ya Aprili 6, 1999, katika iliyokuwa Kilimanjaro Hotel, Bi Joy Mukanyanga aliyatamka haya; 

” Naogopa, kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha maauji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994.” Alisema Balozi yule wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha mauaji yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ndio, Bi Joy Mukanyange alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona. 

Na tutafanya makosa makubwa, kama hata sasa, tutajifanya kuwa hatukioni kile ambacho Balozi Joy Mukanyange alikiona .  Watanzania tukubali  sasa kuwa tumepatwa na bahati mbaya sana ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. 

Hili ni jambo la hatari sana. Ni hulka ya mwanadamu, anapokuwa matatizoni kumtafuta kondoo wa kafara. Mtu mwingine wa kummyooshea kidole kwa matatizo yake. Hali duni ya uchumi wa nchi, hali duni za maisha na umasikini wa watu wetu isiwe chachu ya kuanzisha vurugu za kijamii. 

Maana, taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwapo na WAO. 

Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la wengi wetu kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi, ufahamu mdogo wa historia yetu. Hivyo basi, kupelekea hali ya kutojitambua kama taifa. Ndio, uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana. Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda. Historia ni kama maji ya mto, kamwe haijirudii. Historia ni wakati, ni muda. Kihistoria jana ni sawa na zamani. 

 Karne nyingi zilizopita wahenga wetu walitafsiri muda kama mkusanyiko wa matukio ya zamani na sasa. Waliamini kuwa yaliyotokea zamani na yanayotokea sasa ndiyo yenye kusaidia kubashiri yatakayotea kesho, yataamua mustakabali wetu. 

 Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini na ukabila si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa. Tuliopata bahati ya kutumia kalamu zetu hatuna budi kuliweka hili hadharani. 

Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu ambao hawana nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi yetu. Mengine yanayofanyika sasa sio tu yanaitia doa nchi yetu, bali, yanaiaibisha nchi yetu. 

Ndugu zangu, 

 Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe. Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au wanavyotutaka tufikiri, historia yetu haikuanzia enzi za Mwarabu , Mjerumani au Mwingereza. Historia yetu haikuanzia enzi za TANU wala Afro Shiraz. 

Na dini hizi za kimapokeo zinazotufanya sasa tufarakane zimekuja na kuzikuta dini zetu za asili, na bado tunazo. Na hakika, Afrika hatugombanii matambiko. Afrika kila ukoo una tambiko lake, hivyo basi, dini yake. Kamwe hutasikia Waafrika wanagombania matambiko. Hutasikia Waafrika wakigombana kwa tofauti za matambiko yao. 

Na sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za imani hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo. 

Naam; kamba hukatikia pabovu, wanasema wahenga.Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Tusifike mahali tukagombana kutokana na tofauti za imani ama dini ambazo wala si za asili yetu. Imani au dini ambazo, kama ilivyo dini zetu za asili, nazo zinatutaka wanadamu tuishi kwa amani, upendo na maelewano.

 Na hilo ndilo Neno la leo. 

Maggid Mjengwa, 

Iringa. 

0788 111 765, 0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment