Sunday 14 October 2012

Re: [wanabidii] Natamani watanzania tuwe kama Kingunge ili kukomesha udini

Comrades
Naungana na Kalulunga pamoja na Kalogosho katika kuliangalia swala zima la mtu kuwa na imani ya kidini. Siku ya vurugu za Mbagala nilipanda basi la kutokea Posta kwenda Mbezi. Nilikaa na kijana aliyekuwa amevalia sare za FFU nilipomuuliza akaniambia kwamba anatoka Mbagala kwenye zoezi la kutuliza fujo. Nilipomuuliza ni nini chanzo cha tatizo alinijibu " tatizo ni uchokozi waliouanzisha wakristo kwa waislamu, hawa watu wana dharau sana kwa dini za wenzao. Wana matatizo makubwa ya kuwanyanyasa waislamu" Nikadakia na kumwambia hivi wewe binafsi unaona wakristu ndo wachokozi? akasema hilo halina ubishi.

Sikuona sababu ya kuendelea na maongezi zaidi na mtu kama huyo, yumkini ni kijana aliyemaliza form IV na ameajiriwa, japokuwa sikumuuliza dini yake lakini maelezo yake yalionyesha ni mfuasi wa dini ya kiislam. Kabla ya hapo nilikuwa na mtazamo kama wa Kalogosho kwamba wanaoleta vujo ni vijana ambao hawajavuka darasa la saba kielimu na wala hawana ajira rasmi. Kumbe ata waliosoma zaidi ya darasa la saba na kuajiriwa wana tatizo hilo na pengine ndiyo viongozi.

Tatizo la udini lililopandikizwa vichwani mwa vijana haswa wa kiislamu ni kubwa na inaelekea lina historia ndefu. Ipo misikiti ambayo kwa muda mrefu badala ya kuhubiri habari za Mungu wamekuwa wanahubiri kitu ninachoweza kuita DINI-SIASA. Inaonekana kwao kila tatizo walilo nalo ni sababu ya kuwepo ukristo, na kwamba nchi inabidi iongozwe kwa sharia si vinginevyo.

Ndugu zetu wenye msimamo wa fujo hawataki kuona Kanisa wala sehemu waliko inafanyika biashara ya kuuza nyama ya nguruwe au pombe, kumbuka sababu ya vurugu za Manzese Ajentina waliyotoa ni kwamba mtoto alitumwa nyama ya ng'ombe akaleta ya kitimoto (nguruwe). Waumini wote kwa pamoja wakaanzisha fujo kubwa sana na kuvunja mabutcher ya nguruwe yote kwa kisingizio cha mtoto. Mbagala imekuwa hivyo hivyo kwamba mtoto kakojolea kitabu kitakatifu. Hawa watu wana ajenda zaidi ya wanachokitaja

Watu hawa wanaojiita waislamu binafsi nafikiri si waislamu bali ni kikundi kimeundwa kwa madhumuni wanayoyajua wao. Iweje kila mara kuwe na sababu za kusingizia watoto? Mtoto ameusishwa vipi na makanisa tofauti waliyochoma? Huko Zanzibar walichoma makanisa kwa visingizio kama hivyo kwa vyovyote vile kuna sababu wanazozijua wao na kuwasukuma kufanya uharifu huo na wala siyo hizo wanazokuwa wakitwambia. Ni juu ya serikali kufuatilia kwa makini kujua madhumuni ya kikundi hicho na kutafuta namna ya kuwafanya kufuata masharti ya usajiri wa dini wanakojiegemeza

Wanasahau kwamba pia wapo watanzania kama Kingunge ambao si wafuasi wa ukristo wala uislamu na kwamba wakipewa nafasi wasingependa kusikia milio ya kengele za makanisa au kusikia sauti kutoka kwenye vipaza sauti vya misikiti alfajiri. Serikali ya Tanzania haina dini na wala tusilazimishane kuingia na kutii masharti ya dini yoyote. Kwa wale wenye imani zao wajue imani hizo ni zao wala haziwahusu watanzania wengine na hivyo tukae na imani zetu ndani ya nyumba zetu za imani au tunakoishi lakini tukiwa kwenye michanganyiko tuishi kama Kingunge.

Tuache kutumiwa na watu wenye nia zao mbaya za kuchafua amani yetu kwa visingizio vya kulinda imani, pamoja na kujitahidi kutengeneza ajira kwa vijana pia tupige marufuku miadhara ya kidini yenye nia ya kubeza na kudharau imani za wenzao. Tunatambua mchango wa dini katika kueneza amani na utulivu na hivyo tuzitumie vizuri dini zetu kwa ajili hiyo.

2012/10/15 Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org>

Kuna haja ya kujitambua sisi ni akina nani, tunataka nini, tulitoka wapi, tuko wapi na tunakwenda wapi? Kuna haja ya kufanya upembuzi yakinifu. Tuache kuchukulia mambo kirahisi  raihisi. Dini ni habari ya yote uliyoyataja; utumwa,ukoloni,ubepari,ukandamizaji,mauaji ya vita za kidini nk. Dini ni vyombo vinavyotumika kufunga akili zetu na kutulaza usingizi mpaka tusijitambue. Ukifanya utafiti zaidi utaelewa. Nakuombea uwe Raisi uweze kuleta mabadiliko. Naomba kuuliza swali; Mbona sikuv kuu ya 'Ashura'  haipo kwenye kalenda za serikali? Mbona Wahindi hawadai ? Mbona Wahindi wana maendeleo ya maisha yao? Mimi naona wakati ufike wa serikali kutengeneza ajira kwa ajili ya vijana waweze kujishughulisha. Maana wanaofanya fujo kama zile za Mbagala ni vijana wanaoona wafanye fujo kama kutumikisha akili zao, la sivyo mtu mwenye shughuli ya kufanya hana muda wa kupoteza kwa shughuli ya kufanya fujo za jinsi hiyo. 'CREATE JOBS FOR THEM'

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of GORDON KALULUNGA
Sent: Sunday, October 14, 2012 8:50 AM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Natamani watanzania tuwe kama Kingunge ili kukomesha udini

 

NA, GORDON KALULUNGA.

 

MTINDO wa kumsifia mtu baada ya kufa nafananisha na sifa za kijinga hivyo nimeona ni vema nitoe mwanga kuwa ni vema sasa kwa mtu akifanya jambo jema asifiwe akwa hai badala ya kubaki na fikra mgando na misemo ya kimazoea.

 

Mzee wetu Kingunge Ngombale Mwiru binafsi namwona ni mtu ambaye wa mfano wa kuigwa na kupongezwa na kuheshimiwa katika Taifa letu.

 

Moja ya mambo ambayo namsifu Kingunge ni jambo la kujitanabaisha kuwa yeye hana dini, sijui ni maono gani ambayo alikuwa nayo mpaka akaamua kujiweka wazi katika jambo hilo ambalo kwa wanaoendeeza udini wanajua hasara zake katika Taifa.

 

Katika suala hilo kwa kweli natamani Watanzania sote tuwe kama yeye kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa hapa nchini na ninajua hapa nitawaudhi sana wenye mikakati na mipango ya kuimarisha kwa nia ovu udini katika Tanzania yetu.

 

Nirudie kama nilivyowahi kusema katika makala zilizopita kuwa nitasema ukweli daima fitina kwangu ni mwiko nia yangu ni maslahi ya Taifa kwanza kwa kusema ukweli mchungu unaouma.

 

Nimekuwa nafuatilia kwa kina mjadala wa Mahakama ya Kadhi na mambo ya udini kwa ujumla katika nchi yetu. Wengi wanadai kuwa Tanzania ni nchi ambayo haina dini na kwamba eti haipaswi kuchanganya dini na siasa katika utawala wa nchi kwani madhara yake yanafahamika.

 

Kinadharia ni kweli kuna jambo hilo lakini kiuhalisia Tanzania ina dini ambazo si za asili zetu bali ni dini za kimapokeo ambazo zisipotumika kiuzalendo na kuangalia kwanza maslahi ya Taifa zitatupeleka mahala ambapo sijajua mwisho wake utakuaje.

 

Sijajua kuwa kusema Tanzania haina dini maana yake ni nini kwasababu kuna sukuu zinazotambuliwa rasmi kiserikali kuna mfano sikukuu ya Idd, Krismas, Pasaka na inawezekana zipo zingine, msomaji wangu utanisaidia.

 

Shere hizi za dini ni zile zinatokana na dini zinazoitwa dini za "kweli" yaani Uislamu na Ukristo.

 

Katika sherehe hizi mara kadhaa kwa umri wangu nimeona viongozi wa Serikali wakijihusisha kiuhakika wakiwa kama wageni rasmi na kutoa hotuba za kitaifa kupitia sherehe za dini hizo jambo ambali nahisi Tanzana ina dini.

Wakati Serikali inazitambua sikukuu hizo lakini hazitambui na kujihusisha na sherehe za wahindu na za watu wanaitwa wapagani.

 

Kwa baadhi ya watanzania wengine aidha kwa kujua mikakati ya dini zao kuhusu utawala wa nchi ama kwa kutokujua wanaamua kuueneza udini huo hadharani mahala pengi nchini na hili kwa sasa linajidhihilisha kwenye mikutano ya tume ya maoni ya katiba.

 

Mfano moja wapo ni hivi karibuni mkazi wa kata ya Forest Jijini Mbeya, Juma Nkwabi (22), alitoa lugha ya kuwakashifu waumini wa dini ya kikristo, ambapo aliwaita kuwa ni Makafiri, wakati akichangia maoni yake mbele ya wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba.

 

Kijana huyo alitamka wazi jambo hilo na mengine katika mkutano huo uliokuwa umefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Meta kata ya Mbalizi Road ya Jiji na Mkoa wa Mbeya, ambapo alisikika akisema Katiba ijayo iseme wazi kuwa watu wa dini ya kikritu ni Makafili hivyo wasiruhusiwe kuchinja mnyama yeyote.

 

Suala hilo halijaanza leo kuibuka katika nchi hii bali limewahi kuibuka hata katika vikao nyeti vya Serikali ambapo kwa kujua mikakati endelevu ya dini ama kwa kutojua baadhi yetu tumeendelea kusumbuliwa na tatizo linalohusiana na uchinjaji wa nyama tunayotaka kuitumia watu wa imani na dini mbalimbali.

 

Dini kama Uyahudi , Ukristo kwa kuzitaja kwa uchache zilikwisha kuwapo. Je hao walikuwa hawali nyama? Na kama walikuwa wanakula walikuwa wanachinjiwa na nani Waislamu wakiwa hawapo? Nani aliyekuja kutangaza baadaye kuwa ni Waislamu tu ? Je ni serikali?

 

Kwa muda mrefu baadhi yetu tumekuwa tunaishawishi Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itunge sheria moja itakayoitambua dini moja tu ya Kiislamu ndiyo ihusike na uchinjaji wa wanyama kwa ajili ya matumizi ya Watanzania wote.

 

Hoja ya namna hiyo iliwahi kupelekwa katika kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mh. Hafidh Ali Tahir, Mbunge wa CCM, Dimani, Zanzibar, katika Mkutano wa Tano, Kikao cha Tano cha Bunge , cha tarehe 6 Novemba,2009 kama alivyonukuliwa na Taarifa Rasmi ya Bunge, (HANSARD),uk.55,56.

 

Ninamnukuu " Sasa Mheshimiwa Waziri, ningemwomba basi akaangalia na sehemu zote hizi mbili. Sitaki aende ndani sana lakini ninachosema ni kwamba bodi ifike mahali iweke sheria, kuwe na kanuni ya uchinjaji wa nyama ambao tunataka tuwatumie.

 

Tusichinje tu. Ndiyo nikasema kwamba Tanzania haina dini lakini Watanzania wana dini, tunakula kula nyama hii. Sasa kuwe na utaratibu maalumu. Sasa Mheshimiwa Waziri, hili atakuja kutuambia vipi angalau basi tuweke utaratibu unaofahamika. (Makofi).

 

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakupa mfano ukienda nchi za wenzetu hasa nchi za Kiarabu, si kwamba wote watakuwa Waislamu kwa sababu ni nchi za Kiarabu hapana. Ndani ya nchi za Kiarabu kuna watu wana dini nyingine na wala usije ukasikia mtu anaitwa Hafidh Al-Saad kwa mfano, ukafikiria ni Muislamu,hapana ni jina tu hilo.

 

Lakini dini yake ikawa nyingine. Abdulaziz utasema kwa jina hili huyu Muislamu hapana si Muislamu jina kitu kingine dini kitu kingine. Sasa wenzetu kwa sababu ya kuweka tofauti pale ambapo kunachinjwa nyama halali, basi unapokwenda katika ranchi yao ya kuchinjia kile kisu kimeandikwa Bismillah na kule alikoelekea yule ng'ombe ndiko kunakokubalika.

 

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyama zinauzwa Dar es Salaam, Dodoma na mahali pengine,wallah hawaulizwi kwenye bucha wamechinja wapi nyama hiyo, hawaulizi wala hawaulizwi kwamba ngombe huyo alivyochinjwa kaelekea Kibla, sote tunakwenda kununua nyama, tunaondoka.

 

Lakini nasema lazima kama ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunataka kupitisha jambo hili lazima tuwe na tahadhari. Sasa namwomba Mheshimiwa Waziri awe na tahadhari na hili mbaya hajitokezi sasa anajitokeza baadaye" Mwisho wa kunukuu

 

Hilo ndiyo ombi lililopelekwa Bungeni ili Bunge litunge sheria ya namna ya uchinjaji wa nyama. Mh. Hafidh Ali Tahir alipendekeza sheria itakayotungwa lazima izingatie zaidi utaratibu wa Kiislamu akimaanisha wanyama wanapochinjwa wachinjwe kwa kuelekezwa Kibla, uelekeo ambao Waislamu huelekeza nyuso zao wakati wa kufanya ibada zao, yaani Makka.

 

Waziri wa Mifugo wa kipindi hicho Mh. Anthony Diallo (MB) akijibu ombi hilo alitoa msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kuhusu uchinjaji. Ninamnukuu kama alivyonukuliwa katika uk.88 wa Hansard hiyo hiyo ya Bunge.

 

Anasema " Kwa hiyo, muuzaji nyama yeyote ni lazima atazingatia kitu ambacho ni desturi na mila na matakwa ya wanunuzi wa nyama hiyo. Kwa hiyo, hatuhitaji kuweka kwenye sheria kwa sababu tunafahamu Serikali yetu haina dini na hatuwezi kuanza kuingiza vifungu vya kutamka mahitajio ya dini moja au dhehebu moja ndani ya sheria tunakiuka Katiba ambayo inatukataza Serikali isijihusishe na uhuru wa dini ni wa kila mtu sio wa Serikali". Mwisho wa kunukuu.

 

Qur'an nayo inayaeleza makundi yanayotakiwa kuchinja na chakula hicho kiwe halalai kwa Waislamu. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maidah, 5:5 " Leo mmehalalishiwa kula vilivyo vizuri na chakula cha wale waliopewa kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao…….."

 

Sitaki kwenda mbali zaidi lakini niseme kwamba kuna chembechembe za udini nchini jambo ambalo linapaswa ukemewa vikali kwa ajili ya umoja wetu wa kitaifa.

Kuna mhubiri mmoja wa Kiislamu aliwahi kushtakiwa Mahakama Kuu aliposema Yesu si Mungu, na likawa zogo la kitaifa lakini sijawahi kusikia serikali hii hii imeingilia kati kuhusu udhalilishaji wa wazi wa imani zetu za jadi na hao watu wa dini za "kweli"

 

Sasa kwa mtu kama mimi ninyeambiwa naabudu "mashetani" wapi serikali inanitambua katika hizo documents zake?

 

Ninapozungumzia jambo hilo nazungumzia dini za kigeni ambazo zimeonekana kutumeza hata haldari za fikra zetu yaani dini ya Uislamu na Ukristo na waka si dini ya inayoitwa ya waabudu mizimu ''upagani''.

 

Hata huu mjadala wa Mahakam ya kadhi wahusika wakuu wa malumbano ni hao hao na wala si "wapagani" na waabudu "mizimu" na "uchawi"

 

Waislamu na wakristo wamefaidi rasilmali nyingi za nchi wengine wanatoa hata mifano ya majengo ya TANESCO Morogoro kutumika kwa ajili ya chuo kikuu cha kiislamu.Najua baadhi yenu mtaudhika sana na ukweli huu.

 

Yapo mengi tu ya kuweza kuthibitisha kuwa nchi hii ni ya kidini na hizo dini zinafahamika.

 

Naamini ni wale tu ambao wataweka pembeni upenzi wa dini na kuvaa uzalendo wa Tanzania yetu ndiye ataniunga mkono kuhusu jambo hili.

 

Kibaya zaidi mpaka nafikia kusema kuwa ingekuwa amri yangu sote tutangaze kuwa hatuna dini kama Kingunge Ngombare Mwiru au tuendelee kuabudu dini zetu za asili kwasababu nahisi dini hizi ni zile zile zilizotumika katika maouvu ambayo historia ya dunia imeshuhudia:utumwa,ukoloni,ubepari,ukandamizaji,mauaji ya vita za kidini nk.

 

Wakati tunasema Mungu tuepushie mbali na udini wa fikra mbaya kwa taifa letu, tusimame imara na kukemea na kulaani kwa kauli za kutoka katika sakafu za mioyo yetu siyo unafiki na kusema kweli kuwa tuzichunguze na kuziangamiza mbinu zote chafu za udini katika nchi yetu ili tuwe salama vinginevyo hatutabaki salama sisi na vizazi vyetu.

 

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.

 

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwaq simu 0754 440749,www.kalulunga.blogspot.com

 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment