Thursday 11 October 2012

Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?

Dear Kaka Kafumu,
Kaka  HK anaandika kuwa, hakukuwa na tuhuma za rushwa kwako wala kiongozi yoyote wa CCM ama serikali aliyetuhumiwa na kukutwa na hatia ya kutoa rushwa kule Igunga.
Definitely Kaka HK hajui nini rushwa. Kwake yeye labda ukikutwa unatoa pesa ndio unaweza kutuhumiwa na hatia ya rushwa. 
Rushwa, Kaka Kafumu, is any dishonest act committed in return for personal gain. Hata yule aliesema kuwa daraja halitomalizwa Igunga kama CCM haitoshinda – nae pia alitenda kitendo cha rushwa kwa upande wako.
Mahkama Kuu imegundua kuwa dishonest acts (yaani rushwa) zilitumika na ndio maana ikapinduwa ushindi wako.
Kaka HK nae anaeleza kuwa yumo katika kuandika kitabu chake pia. Hili ni jambo zuri sana na ninampongeza kama ninavyokupongeza wewe, kwani 'vizazi na vizazi vitapata kusoma na kujifunza',
lakini sijui kitabu chake kitakuwa kuhusu nini – most probably his book will be titled - How fast a Cowboy draws his  gun on his enemy.
Hapa netini, mimi nilikuwa katika watu wa mwanzo kukupa hongera baada ya ule ushindi wako na nilikuwa peke yangu nilie-withdraw hongera zangu baada ya kufahamu nini kilitokea Igunga na kuwa kumbe ulishinda kwa mazonge na rushwa. 
Ninastaajabu, vipi mtu anaandika kitabu kuhusu ubaya na extent ya rushwa nchini na huku anakuenda kugombania ubunge kupitia CCM na sio Chadema. Are we serious? The only CCM member ambae alikuwa free of rushwa kwa bahati mbaya amefariki tokea 1999. Sidhani kama yupo mwengine. Mwengine ambae tungelimdhania juzi aliadhirika Kisutu kuenda kudai kodi zake alizotapeliwa. Sisi tulimpa usukani ndugu yetu kumbe mwenzetu alikuwa busy kujenga nyumba za kukodisha katika kila corner ya DSM. Kama ni mimi nisingelikuenda Kisutu kujiadhirisha na ningelimuachia tu huyo mwizi hicho alichochukuwa – kama vile na yeye amechukua chake mapema kutoka kwangu!


Anyway, najua mpo wengi hapa ukumbini (Tony, HK, etc) na kwahivyo bora nikimbie kwa haraka!

//Nkumba.
 


From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, October 10, 2012 3:55:48 PM
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?

Waungwana
 
Nawaomba mnunue kitabu kwanza msome, na kufanya "a book review" na mjadili na kutoa maoni yenu. Kitabu ni cha kingereza mwandishi wa gazeti kajaribu kutafsiri - ni vizuri kusoma mwenyewe. Tuwasiliane mpate kitabu. Kinauzwa Shs 15,000 tu. Karibuni..
 
Ng'wizukulushilinde

--- On Wed, 10/10/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, October 10, 2012, 5:05 PM

Mimi siyo Kafumu na wala sijabahatika kusoma kitabu chake lakini kwa
kuiangalia sehemu uliyonukuu "...kwamba kuishi kwa uaminifu katika
jamii iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki
aliyejeruhiwa baharini" unaweza kutoa tafakari.  Maneno hayo ni ya
kiswahili yanayoweza kueleweka kwa wasomaji japo mwandishi anaweza
kuwa na tafsiri zaidi.

Kwa vile katuandikia wasomaji ili tusome kitabu chake na bila shaka
kuelewa ujumbe anaokusudia tuupate. Binafsi namuelewa kwamba si rahisi
kuuona uaminifu wa mtu au watu waaminifu wachache wanaoishi na jamii
kubwa isiyokuwa na uaminifu (wala rushwa). Kwa kufafanua
anachokimaanisha akafananisha mchango wa mtu mwaminifu na tone la damu
ya samaki baharini.
Kwa ufupi kama mada inahusu rushwa na tukiamua kujielekeza katika
tukio lililompata mwandishi wa kitabu hicho tunaweza kupata maana
zaidi. Yeye Kafumu amevuliwa ubunge kwa sababu ya ukiukwaji wa
taratibu za uchaguzi yumkini ikiwemo rushwa.

Maana pana zaidi tunayoweza kupata ni kama waziri mstaafu (Sumaye)
alivyosema juma lililopita kwamba rushwa inanuka katika chaguzi za
CCM. Inawezekana Kafumu alianza kudaiwa rushwa tangu kuteuliwa na
chama chake hadi kwenye uchaguzi wenyewe. Hivyo anavyosema mtu
mwaminifu hawezi kutokea kwenye kundi la wala rushwa maana
hawatampitisha na hivyo hawezi kuonekana au kueleweka kwa namna
yoyote.

Lakini pia Kafumu anaweza kuwa na maana pana zaidi ya kwamba
watanzania kwa ujumla wetu tulikofikia ni mwendo wa kutoa chochote ili
uchaguliwe "Toa kula nikupe kura"
Kwamba nchi imekuwa ya watu wasiokuwa waaminifu na hivyo mchango wa
mtu mwaminifu hauwezi kuonekana kwa namna yoyote. Nafikiri Kafumu hana
mpango wa kuomba radhi bali ameamua kuanika alichokiona ndani na nje
ya CCM

Naamini Kafumu mwenyewe atatueleza nini hasa alichokimaanisha ili
tuweze kununua na kukisoma kitabu chake kwa uelewa zaidi

2012/10/10 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>:
> Hi All,
> Nd. Peter Kafumu ameandika kitabu kuhusu rushwa nchini kinachoitwa "Sauti
> Inayolia-Tafakuri Binafsi" (a Crying Voice-personal reflections).
> Maelezo yake ya mbio mbio yananipa fikra kama huyu Mhe anatubia labda kwa
> kushinda kule Igunga kwa kupitia mambo ya rushwa na sasa anaomba radhi.
> Anyway, kila mtu atafahamu kivyake, lakini mimi ninamuona kama anaomba
> radhi, hasa pale alipoandika kuwa...."...kwamba kuishi kwa uaminifu katika
> jamii
> iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki aliyejeruhiwa
> baharini".
>
> Najua Mhe Kafumu yupo hapa ukumbini. Ningelimuomba atupe briefing ya kitabu
> chake ambacho kidogo hakifahamiki - yaani haeleweki kama anai-expose
> rushwa au anaomba radhi kwa rushwa iliyotendeka Igunga mpaka akashinda?
>
>
> http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/peter-kafumu-alishinda-kutokana-na.html
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment