Wednesday 10 October 2012

Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?

Mimi siyo Kafumu na wala sijabahatika kusoma kitabu chake lakini kwa
kuiangalia sehemu uliyonukuu "...kwamba kuishi kwa uaminifu katika
jamii iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki
aliyejeruhiwa baharini" unaweza kutoa tafakari. Maneno hayo ni ya
kiswahili yanayoweza kueleweka kwa wasomaji japo mwandishi anaweza
kuwa na tafsiri zaidi.

Kwa vile katuandikia wasomaji ili tusome kitabu chake na bila shaka
kuelewa ujumbe anaokusudia tuupate. Binafsi namuelewa kwamba si rahisi
kuuona uaminifu wa mtu au watu waaminifu wachache wanaoishi na jamii
kubwa isiyokuwa na uaminifu (wala rushwa). Kwa kufafanua
anachokimaanisha akafananisha mchango wa mtu mwaminifu na tone la damu
ya samaki baharini.
Kwa ufupi kama mada inahusu rushwa na tukiamua kujielekeza katika
tukio lililompata mwandishi wa kitabu hicho tunaweza kupata maana
zaidi. Yeye Kafumu amevuliwa ubunge kwa sababu ya ukiukwaji wa
taratibu za uchaguzi yumkini ikiwemo rushwa.

Maana pana zaidi tunayoweza kupata ni kama waziri mstaafu (Sumaye)
alivyosema juma lililopita kwamba rushwa inanuka katika chaguzi za
CCM. Inawezekana Kafumu alianza kudaiwa rushwa tangu kuteuliwa na
chama chake hadi kwenye uchaguzi wenyewe. Hivyo anavyosema mtu
mwaminifu hawezi kutokea kwenye kundi la wala rushwa maana
hawatampitisha na hivyo hawezi kuonekana au kueleweka kwa namna
yoyote.

Lakini pia Kafumu anaweza kuwa na maana pana zaidi ya kwamba
watanzania kwa ujumla wetu tulikofikia ni mwendo wa kutoa chochote ili
uchaguliwe "Toa kula nikupe kura"
Kwamba nchi imekuwa ya watu wasiokuwa waaminifu na hivyo mchango wa
mtu mwaminifu hauwezi kuonekana kwa namna yoyote. Nafikiri Kafumu hana
mpango wa kuomba radhi bali ameamua kuanika alichokiona ndani na nje
ya CCM

Naamini Kafumu mwenyewe atatueleza nini hasa alichokimaanisha ili
tuweze kununua na kukisoma kitabu chake kwa uelewa zaidi

2012/10/10 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>:
> Hi All,
> Nd. Peter Kafumu ameandika kitabu kuhusu rushwa nchini kinachoitwa "Sauti
> Inayolia-Tafakuri Binafsi" (a Crying Voice-personal reflections).
> Maelezo yake ya mbio mbio yananipa fikra kama huyu Mhe anatubia labda kwa
> kushinda kule Igunga kwa kupitia mambo ya rushwa na sasa anaomba radhi.
> Anyway, kila mtu atafahamu kivyake, lakini mimi ninamuona kama anaomba
> radhi, hasa pale alipoandika kuwa...."...kwamba kuishi kwa uaminifu katika
> jamii
> iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki aliyejeruhiwa
> baharini".
>
> Najua Mhe Kafumu yupo hapa ukumbini. Ningelimuomba atupe briefing ya kitabu
> chake ambacho kidogo hakifahamiki - yaani haeleweki kama anai-expose
> rushwa au anaomba radhi kwa rushwa iliyotendeka Igunga mpaka akashinda?
>
>
> http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/peter-kafumu-alishinda-kutokana-na.html
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment