Sunday 21 October 2012

Re: [wanabidii] Lowassa Ataka Waislam, Wakristo Kuungana - Mwanzo

yuko right kusema hivyo.l hope at this time anapojiandaa kugombea urais afikirie kwa makini mising ya amani ya nchi hii na atangaze vita ya dhati kwa wote wenye kuhatarisha amani simply kwa kudanganyika kwao.Maendeleo ya mtu ni mipango.na kupanga ni kuchagua.ukichagua vibaya utapata matokeo mabaya.Na kabla ya kulaumu mtu kwa matokeo yako,jilaumu mwenyewe kwa mipango yako mibovu.ukizaa watoto kumi na wawili kwa kipato cha laki 5 kwa mwezi usitake hata kidogo kulingana kistandard ya maisha na aliyezaa watoto 3 kwa kipato hichohicho.Ujinga hauvumiliki tena,na hautafanikiwa.



------------------------------
On Sun, Oct 21, 2012 3:32 PM EEST Magiri paul wrote:

>Na: Daniel Mjema, Mwanga, MWANANCHI.
> WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amewataka waumini wa madhehebu yote
>nchini kuonyesha mshikamano katika ujenzi wa shule nchini bila kujali shule
>inayojengwa ni ya Wakristo au Waislam.
> Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alitoa kauli hiyo jana
>wilayani Mwanga katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Kiislamu ya
>Lambo iliyopo kata ya Shighatini.
> Lowassa alitumia fursa hiyo kusema kuwa Wilaya ya Mwanga ni ngome ya Chama
>cha Mapinduzi (CCM), na kwamba kwa kusema hivyo hakipigii debe chama chake
>bali huo ndio ukweli.
>
>Katika tamasha la harambee hiyo iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Mwanga,
>Profesa Jumanne Maghembe, Masheikh na Wachungaji wa madhehebu mbalimbali,
>Lowassa alichangia Sh10 milioni.
>
>"Mwanga ni nguzo yetu ya CCM na wala hili sio jambo la siri…Namfahamu
>Profesa Maghembe, katika kura hapa hamkukosea hili ni jembe…ni kiongozi
>hodari na mchapa kazi," alisema Lowassa.
>
>http://wotepamoja.com/archives/9407#.UIPrXEp88ww.gmail
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment