Saturday 20 October 2012

Re: [wanabidii] KIZAZI HIKI NI CHA KUDADISI!

Bwana kessy,lengo lako ni zuri lkn mfano umekosea.Aliyeambiwa usiangalie nyuma ni mke wa Luthu nduguye Ibrahim.Na haikuwa ktk kuingia ndani ya safina bali ktk kutoka nchi ya sodoma na gomora.Ngupula Godfrey



------------------------------
On Sat, Oct 20, 2012 9:34 PM EEST Sylvanus Kessy wrote:

>Katika Biblia mke wa Nuhu aliambiwa asiangalie nyuma wakati wa kuingia kwenye Safina. Akaangalia kijanja akawa jiwe LA CHUMVI.
>
>
>Watoto wa siku hizi ukimwambia usishike umeme, utakufa, atashika ili aone kama atakufa. Na kama hatakufa ile shock itamfunza asirudie tena.
>
>
>Misahafu ni vitabu vitakatifu. Vinatakiwa viheshimiwe na vitunzwe vizuri. Ni vema kuwafundisha watoto wetu kuviheshimu na kuvitunza.
>
>
>Tukiwaambia ukikiharibu utalaaniwa na Mungu. Mwanzo ataogopa maana hajui maana ya laana ni nini. Kadiri ya kukua na udadisi wake ataelewa pole pole maana ya laana.
>
>
>Ukimwambia ukikikanyaga utakuwa mbuzi siku moja akiwe mwenyewe atakikanyaga ili aone kama atakuwa mbuzi. Asipokuwa mbuzi ni hatari ya kukidharau kwa kuona kile alichofundishwa ni uwongo amedanganywa na hakuna ukweli.
>
>
>Wazee wetu pia walifundishwa mwanamke mjamzito asile mayai kwa vile atazaa mtoto asiye na nywele. Siku hizi wanakula. Katika kabila langu tukiwa watoto tuliambiwa tusile nyama ya maini maana utakapo tahiriwa utatoka damu nyingi. Siku hizi wanakula. Kumbe mafundisho yale yalikuwa UWONGO. 
>
>Tuangalie Elimu tunayowarithisha watoto wetu. Inaweza kuwapotosha.
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment