Saturday 20 October 2012

Re: {Spam?} [wanabidii] Uislamu,Ukristo,Upagani na Dai la 'Mfumo Kristo'

Ndugu Chachage,
Nashukuru sana kwa maelezo ya Dr Chachage, ambayo yamenifungua ufahamu hasa kuhusu kwa nini Waislamu hawakuona kutaifisha shule za Wamisionari ilikuwa jawabu ya kuboresha elimu ya watoto wetu wenye imani ya Kiislamu! Ingawa huyo mjomba wetu labda hafahamu kuwa hao waliotuletea dini ya Uislamu walianza kupeleka watoto wao kusoma vyuo vya "mfumo wa Kikristo" Ulaya, Uingereza na Amerika tangu zamani sana na ndio maana wana uwezo sasa wa kutengeneza hata mabomu ya Nuklia! Lakini swali je ni kweli tuna "mfumo wa Kikristo" katika utawala wetu? Au tatizo ni kuwa haufuati "mfumo wa Sharia"? Kwa maoni yangu kwa Wanazuoni kulichukulia swala hili kama zoezi ambalo suluhu inaweza kupatikana kwenye maongezi ya kwenye blog si kulitendea haki. Ningeelewa kama ingekuwa wananchi wa kawaida wanabadilishana mawazo kwa njia hii. Napendekeza tuitishe kongamano la Wanazuoni na viongozi wa dini (pamoja na Wapagani, kama ni dini??) ili tulifanyie haki inayosatahili jambo hili nyeti. Wasiwasi ni kuwa kwa vile wengi wetu hata hatujawahi kuchukua muda kujifunza kwa malinganisho (comparative analysis) kati ya imani za Kikristo, Kiislamu na Dini za Asili za Kiafrika, na jinsi ambavyo mfumo wa kiutawala unaoitwa wa Kikristo unavyokidhi mahitaji ya imani hizi, ina hatari akatokea mchangiaji hoja akawakashfu wengine bila kukusudia au kwa maksudi na jukwa hili na Wanabidii likaingia dosari.
Wasalaam
Lunogelo

2012/10/19 Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
Japokuwa nchi yetu ya Tanzania inaongozwa na Rais na Makamu wa Rais walio waislamu na ina Katiba ambayo siyo ya kidini bado kuna madai kuwa tupo chini ya 'Mfumo Kristo'. Ukiichambua kwa mapana dhana ya 'Mfumo Kristo' utaona inamaanisha 'Mfumo wa Kimagharibi' kwa kuwa kwa kiasi kikubwa taasisi, elimu, taratibu na sheria zetu zinatokana na 'Ustaarabu wa Kimagharibi' (Western Civilization) ambao unasemekana ni zao la 'Ustaarabu wa Kikristo' (Christian Civilization) ulioletwa 'kwanza' kwetu na wamishionari na wakoloni waliotoka katika 'nchi za kikristo na kimagharibi'. 

Ndio maana kama hivyo ndivyo watoa madai wanavyoamini basi kushambulia watu au/na vitu ambavyo hatuoni uhusiano wa moja kwa moja na madai yao mengine, ni sehemu ya kupambana na huo wauitao 'Mfumo Kristo'. Hoja hii haipingani na hoja jadidi ya Mwanasosholojia wa Dini kuwa nchi yetu iko katika ombwe la dira na matatizo ya ajira na ujira hasa kwa vijana hivyo kufanya iwe kazi rahisi kuwafanya waone tatizo ni huo 'Mfumo Kristo' ambao wanauona ndio, kihistoria, umewanyima elimu na ajira. 

Kwa mfano, mjomba wangu ambaye ni muislamu anadai kuwa tunakosea tunapomsifu Mwalimu Nyerere kwa kuchukua shule za wamishonari/makanisa na hivyo eti kuwasaidia waislamu wasome. Kwa mujibu wa tafsiri yake ya historia ya Tanzania, moja ya sababu ya waislamu kuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru ni ili waweze kujenga shule zao wenyewe zitakazotoa elimu bila kulazimika kufuata misingi ya wakoloni na wamishionari ambao walikuwa ni wakristo. Hivyo kwa tafsiri yake, Nyerere alichofanya baada ya uhuru ni kuwazuia waislamu wasiweze kujenga shule zao na hivyo kuwafanya, kwa ujumla, waendelee kuwa nyuma kuliko wakristo. Inawezekana kabisa kuna ukweli katika hilo.

Ni vigumu kuelewa hoja hizo bila kuvua lensi za Kikristo na kuutafiti kwa kina ukweli wake. Tunapaswa kuelewa watoa madai wanamaanisha nini hasa wanaposema kuwa tatizo ni 'Mfumo Kristo' kujikita katika nyanja ya maisha na taasisi zetu. Inabidi tuwaelewe na tujielewe kwa undani kwanza. Na kama alivyosema mpagani fulani, kudhani kutofikiria dini ni kutokuwa na udini ni sawa sawa tu na kudhani kutofikiria rangi (color blindness) ni kutokuwa na ubaguzi wa rangi. Hivyo, tunapaswa kujiuliza, je, kweli tumesimika mfumo ambao kwa kudhani haufikirii dini (religion blindess) unawaacha nyuma waumini wa dini fulani? Kwa mantiki hii, inawezekana kabisa kuwa yale maneno ya Nyerere aliyoyarejea mwaka 1995 kuhusu Tanzania kutokuwa na dini ya yeye binafsi kutofikiria suala la dini wakati wa kuteua viongozi ni sehemu ya upofu wa dini unaopelekea watu wa dini fulani wasahaulike kwa kuwa hawaonekani kuwa wapo.


[Kwenye hotuba hii Nyerere anaongelea udini kuanzia dakika ya 10 na sekunde 21]


-- Posted By Blogger to UDADISI: Rethinking in Action at 10/19/2012 12:09:00 PM



--
This message has been scanned for viruses and
dangerous content by MailScanner, and is
believed to be clean.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment