Saturday 8 September 2012

[wanabidii] RE: VIONGOZI WA CCM WANACHAGUA VITI KWENYE MELI INAYOZAMA

Katika jambo la kushangaza na kutia mvuto ni kuona bado Viongozi wa CCM waliojivunia heshima nyingi sana katika nchi hii wanaendelea kuchagua viti vya kukalia kwenye meli inayozama.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kurudisha mali zote walizochuma na kuiba ndani ya Serekali.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kuficha malioni ya fedha nje ya nchi huku Watanzania wakikosa huduma muhimu.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kutumia Jeshi la Polisi kuwaua raia wasio na hatia hovyo badala ya kuwalinda wanapodai haki zao  kwa amani.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kuwalipa Wafanyakazi vizuri katika sekta ya Elimu na Afya.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kuweka hadharani mauzo ya mashirika na viwanda vya Umma vilivyouzwa kiholela na kupunguza ajira kwa Watanzania.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kutoa ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kuwaondoa wawekezaji waliovamia ardhi ya wazawa na kupora rasilimali kijanja na kwa nguvu huku wakiwapiga risasi za moto.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kuwaondoa wawekezaji kwenye sekta za madini na utalii ambazo kwa kiasi kikubwa wanaficha fedha nje ya nchi.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kuwafilisi Mafisadi walioibia Umma na kusababisha tabaka kubwa la walio nacho na wasio nacho.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kuwajaza wafungwa wa kuiba Kuku magerezani wakila bure lakini Wezi wa fedha za umma wanapeta uraiani.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kama Serekali italiacha Jeshi la Polisi kuendelea kujitafutia mali badala ya kufanya kazi za umma kwa weledi.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kama haitwapa uhamisho Polisi mara kwa mara ambao ndio wanasababisha kukua kwa rushwa nchini.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kkubali Demokrasia nchini kwa kuwaacha Watanzania wachague chama wanachokitaka.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania katika kukuza sekta ya elimu na kufanya elimu iwe sawa kwa wote.

-CCM haina chake Tanzania bila kurejesha imani kwa Watanzania kwa kutumia utawala wa Sheria na sio kutisha vyama vyaq upinzani ambavyo vina wafuasi wengi vinginevyo watasababisha machafuko nchi. Tedwa tumia busara vinginevyo uchomwe wewe na familia yako kwa kutetea ufisadi.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment