Wednesday 26 September 2012

[wanabidii] Re: Jee unataka kuwa Tajiri?

Papa,

I believe Charles was addressing Tanzanians, not dog sellers like you.

You replied out of turn. Sasa umetuaibisha sote wakenya.

Courage


On 9/25/12, Papa Likondi <papalikondi@gmail.com> wrote:
> How come you yourself is still poorer than most gnus here. People are
> planning how to get tsimillion pap, na wewe unataka kutufunza jinzi ta
> kutengeza shilling kumi. Buuuurrrrrreeeeee kaaaaabbbbbiiiiissssa kama
> ile yako
>
> On 24/09/2012, Charles Nazi <cnazi2002@gmail.com> wrote:
>>
>>
>> Mshauri wa biashara Charles Nazi na mtunzi wa kitabu cha mbinu za
>> biashara
>> na maarifa ya kupata pesa na utajiri, ameanzisha program ya miezi 18 ya
>> kuwasaidia watu wenye malengo ya kutafuta utajiri kufanikisha malengo yao
>> kwa gharama nafuu. Mfumo kama huu umesaidia watu wengi duniani hasa
>> katika
>> nchi zilizoendelea kwa haraka sana. Kwa mfano Anthony Robins huko
>> Marekani
>> alibadilisha maisha yake kutoka kwenye umasikini alivyokuwa akiishi
>> kwenye
>> nyumba ya kupanga na kuwa milionea kwa muda wa miaka 3. Aliweza
>> kufanikiwa
>> namna hii baada ya kumpata mwalimu Mentor aitwaye Jim Rohn. Ukitaka
>> habari
>> zaidi za watu hawa wawili unaweza kuzipata kwenye Google.
>> Kuna njia mbili za kutafuta utajiri njia ya kwanza ni ya kuhangaika
>> mwenyewe bila msaada wowote hii ni njia ndefu. Njia ya pili ambayo ni
>> fupi
>> ni kutafuta Mwalimu,mshauri wa biashara mwenye mafanikio wa kukuongoza.
>> Kwa
>>
>> kiingereza anaitwa (Mentor)
>>
>> Namna ya kupata mshauri na Mwalimu (Mentor) wa biashara
>>
>> Kama unatafuta huduma ya mshauri/mwalimu (Mentor) ni muhimu kutafuta
>> yule mwenye uzoefu na sifa nzuri. Kuna njia mbalimbali za kupata mshauri
>> wa
>>
>> biashara. Katika ngazi ya msingi sana, unaweza kumpata kutokana na
>> ushauri
>> wa mfanyabiashara ambaye amewahi kupata huduma kutoka kwa mshauri fulani
>> kwa mafanikio. Unaweza kupata ushauri kutoka kwa mfanyabiashara maarufu
>> ambaye atakuwa tayali kutumia muda wake.(Kitu ambacho ni kigumu)
>>
>> Kama wewe unashindwa kulipia huduma za ushauri hicho siyo kikwazo, kuna
>> idadi ya mashirika na makampuni binafsi ambayo hutoa ushauri bure au kwa
>> bei nafuu. Ukweli ni kwamba kwa kuwa huduma zao ni bure au za bei nafuu
>> haina maana wao hawana sifa au uzoefu. Baadhi ya wataalamu na washauri
>> wametoa ushauri kutoka huko nyuma kwa jamii zao na kupata uzoefu kama
>> mkufunzi au mshauri, Charles Nazi ni mshauri wa biashara mwenye sifa
>> hizo.
>>
>> Programu ya Utajiri.
>>
>> Utangulizi
>>
>> Programu ya utajiri ni mpango wa kutoa ushauri na msaada kwa watu wote
>> wenye malengo ya kutafuta utajiri kwa njia halali. Wajasiriamali
>> hufanyiwa
>> tathmini, kuangalia shughuli wazofanya au biashara wanazotaka kuanzisha
>> kisha kuendelea kupata ushauri kwa kipindi cha miezi 18 ili kusaidia
>> ukuaji
>>
>> wa biashara zao na kuzifanya ziwe endelevu.
>>
>> Malengo ya mpango.
>>
>> • Kuhamisha ujuzi wa biashara na maarifa miongoni mwa wajasiriamali
>> • Kuongeza fursa endelevu na ukuaji wa biashara
>> • Kutoa jukwaa kwa ajili ya uchumi mdogo kuchangia katika uwezeshaji wa
>> uchumi mkubwa.
>>
>>
>> Kwa nini kuwe na mpango huu?
>>
>> Duniani kote biashara nyingi huanza kwa msaada wa kifedha wa familia na
>> marafiki,pamoja na msaada huu kwa kawaida huja na ushauri wa biashara
>> pia
>>
>> ushauri wa upatikanaji wa masoko. Mpango huu ni programu ya kujaza
>> nafasi
>>
>> ya familia kwa ajili ya watu wasio na ajira na kujiajiri hasa vijana kina
>> mama na watu wote wasio na uwezo.
>> Lazima tutambue kwamba changamoto ya kuanzisha biashara, kupata vyanzo
>> vya
>>
>> mitaji mara nyingi ni kazi ngumu, na muda mwingi hutumika kwa ajili ya
>> kutafuta mbinu za kuanzisha biashara. Mara biashara inapoanza changamoto
>> nyingine huzuka nazo ni kuifanya biashara iweze kuanza kupata faida kwa
>> kutafuta masoko ili uweze kuuza sana na kulipia gharama zikiwepo za
>> uendeshaji na hata kulipia mikopo ambayo ina riba kubwa. Kwa changamoto
>> hizi mjasiriamali mdogo hana uwezo wa kulipia gharama za mshauri wa
>> biashara ambaye anatoza gharama kubwa. Mpango huu unawasaidia
>> wajasiriamali wadogo kupata ushauri mzuri wa kuwasaidia kuanzisha na
>> kuendesha biashara zao kwa ufanisi.
>> Uzoefu na uwezo wa Mshauri charles Nazi
>> Charles Nazi ni msomi mwenye stashada ya Uhasibu kutoka kwenye bodi ya
>> Wahasibu na wakaguzi. Ana uzoefu wa miaka 24 katika kazi ya ukaguzi.
>> Amekuwa kiongozi wa SACCOS kwa miaka 20. Pia ni mjasiriamali ambaye
>> amefanya shughuli mbali mbali na kubuni miradi mbali mbali, kwa mfano
>> amewahi kuanzisha kwa ubia kampuni ya Ujenzi iliyojulikana kwa jina la,
>> Shinyanga annex Building contractors, kiwanda kidogo cha chaki, kuendesha
>> biashara ya mtandao kupitia Makampuni mbali mbali ya kigeni, biashara
>> hizi
>>
>> ameachana nazo. Sasa hivi anajishughulisha na kutoa huduma ya Ushauri wa
>> biashara. Huduma ambazo anazitoa ni; Kutoa ushauri wa biashara kwa
>> Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa, Kuandaa michanganuuo kwa ajili
>> ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili, Kutoa mafunzo ya
>> Ujasiriamali kwa wafanyabiashara, Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu
>> na
>>
>> kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu, Kuandaa katiba za
>> vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni, Kuandaa nyaraka za Tenda,
>> Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi, Kutoa ushauri kwa
>> Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa
>> ufanisi, Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.
>>
>> Charles Nazi ni mtunzi wa vitabu na ametunga kitabu cha Ujasiriamali
>> kinachopendwa sana, kiitwacho, Mbinu za biashara na maarifa ya kupata
>> pesa
>> na utajiri. Kitabu hicho kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta
>> utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa,
>> mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya
>> biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili
>> kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri.
>> Kitabu hicho kilichapishwa kwa mara ya kwanza na Business Printers mwezi
>> March mwaka 2008 na mpaka sasa zimechapishwa na kuuzwa nakala 4,000.
>> Amewawezesha wajasiriamali kupata mikopo ya shilingi milioni 400 kutoka
>> katika mabenki kwa kuwaandikia michanganuo ya biashara. Amewasaidia watu
>> wengi kuweza kuinuka kupitia kitabu chake, semina, ushauri, simu na
>> vipindi
>>
>> vya redio na televisheni.
>> Hitimisho
>> Programu hii inapatikana kwa ghrama ya sh. 300,000.00 za Tanzania kwa
>> kipindi chote cha miezi 18. Kwa kujiunga na program hii utapata huduma
>> zifuatazo;
>> Kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri.
>> Tathmini ya wazo la biashara au biashara yako ili kuweza kujua uanze vipi
>> na kujua vikwazo vinavyokukwamisha usianze au kusogea mbele.
>> Mafunzo ya ujasiriamali ambapo utapata fursa ya kuuliza maswali na kupata
>> majibu papo hapo.
>> Ushauri kwa kipindi chote cha mkataba
>> Mawasiliano ya karibu na mshauri kwa simu au email unapopatwa na vikwazo
>> katika biashara yako.
>> Mbinu za hali ya juu za uwekezaji ili kupanua uwezo na kuongeza mtaji
>> wako.
>> Kuunganishwa kwenye mtandao wa wajasiriamali wateja wake ili kubadilshana
>> mawazo.
>>
>>
>>
>>
>> Je, wewe unataka kuwa tajiri?
>>
>> Tafadhali wasiliana CHARLES Nazi mshauri Biashara Dar es salaam kwa
>> maelezo
>>
>> zaidi tafadhali piga 0755394701 pia tembelea blog yake katika;
>> http://www.squidoo.com/mshauricharles
>>
>>
>>
>
> --
> Sent from my mobile device
>
> *COPYRIGHT © 2012 PAPA LIKONDI*
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment