Sunday 16 September 2012

[wanabidii] Neno La Leo: Unapotongozwa Na Usiyemdhania, Jitathmini....

Ndugu zangu,

Maishani wengi wetu tumetongozwa, iwe kwa mwanammke au mwanamme.

Juzi hapa nikiwa kwa Bi Mkora pale Msamvu, akanilalamikia hili, kuwa siku hizi ameanza kutongozwa na hata ambao hakuwadhania.

Ama , makubwa hayo. Lakini, akaniomba nimpe tafsiri ya jambo hilo.

Nikamjibu, kuwa mwanadamu ukianza kuona unatongozwa na wale ambao hukuwadhania, basi, uanze kwanza kujitathmini, maana, kuna mawili;

Ama, ulivyo sasa na mwenenendo wako, ikiwamo staili yako ya maisha, na hata mavazi yako, yamewafanya wale ambao hukuwadhania , kuanza sasa kukutongoza, au, kwa mabadiliko hayo, wale ambao walikuwa wakikutongoza zamani wameacha sasa kukutongoza, na kuwa sasa unatongozwa na wapya wenye kuvutiwa na mabadiliko hayo yenye kukuhusu wewe.

Lililo jema kwa mwanadamu, ni kwa wale waliokuwa wakikutongoza zamani kuendelea kukutongoza, na juu ya hapo, ukapata watongozaji wapya. Hivyo, personal transformation ( Mabadiliko binafsi) uliyoyapitia yatakuwa yamefanikiwa.

Na katika hili unaweza kuzama kifikra. Ukaangalia hata kwenye chama cha siasa. Kama chama cha siasa kitaanza kukimbiwa na wale waliokuwa wakikimbilia zamani, na kupata wakimbiliaji wapya, basi, hapo kuna tafsiri kama ya hapo juu. Nacho kitahitaji kujitathmini.

Wajumbe nakaribisha hoja zenu...

Maggid

Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.com

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment