Wednesday 26 September 2012

[wanabidii] Msaada Tutani (Je kuna mkaa Kutoka Tanzania unasafirishwa nje ya nchi ?)

Habari wanajukwaa

Waswahili wanasema "ukitingwa usiwe mbishi" nami nimetingwa na nimeona ni vyema niombe msaada hapa jukwaani

Hivi majuzi nilikuwa naongea na mfanyabiashara/msafirishaji wa mkaa mkoani morogoro, na  moja kati ya mambo mengi aliyoniambia

ni kuwa mkaa wa tanzania unauzwa nje ya nchi hasa nchi za kiarabu kama yemen na Saudia,

Nijuavyo mimi (nipo tayari kusahihiswa ) bidhaa ya mkaa hairuhisiwi kuuzwa nje ya nchi, na hata mbao ni lazima ziwe semi processed ndiyo zinaweza kuuzwa.

Sasa,je ni kweli uko ughaibuni kwenye supermarket kuna mkaa Kutoka tanzania unauzwa?,

Wadau mliotembelea ughaibuni hasa nchi tajwa hapa,mmeliona hili? Au yule mfanyabiashara alinipa taarifa zisizo sahii,

Shukrani Wadau





--
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment