Wednesday 12 September 2012

[wanabidii] Kupotelewana vitambulisho


Ndugu wanabidii poleni kwa majukumu ya kila siku
Samahani naomba niwajulishe yaliyonitokea jumamosi ya juzi tar 8/9/2012. Siku hiyo nilikuwa natoka nyumbani kijijini kwetu tukuyu - busoka kwenye msiba wa kakangu Daud Mwangos kuja dar, lakini niliamua kupitia iringa kuwaona  watoto wa marehemu ambao tuliwasafirisha kurudi iringa mara baada tu ya mazishi ya baba yao.
 
Nilipofika uyole mbeya nilipata gari binafsi aina ya Noah ila sikumbuki namba ya hiyo gari.Dereva wake alikuwa msikaji tu wa kati ya miaka 25 hadi 30.Tulipofika iringa alitushusha kwenye stand ya mabsi nami niliona nikate  tiketi kabla sijaenda nyumbani kwa marehem maeneo ya kihesa bwawani,nilipoingia ofisini kwa ajili ya kukata tiketi ndipo nilipogundua kuwa nimedondosha waleti iliyokuwa na kadi ya benk NMB,kitambulisho cha kazi na cha mpiga kura pamoja na kiasi cha pesa ambacho sikumbuki vizuri ilikuwa kiasi gani ila nahisi ilikuwa kati ya sh. 60 elfu au 65elfu.
 
Niliamua kuchukua tax kufukuzia ile gari kwenda Tosa njia panda kwani ilikuwa ni muda mfupi nilipogundua kuwa nimedondosha hiyo walet na tulipokuwa tunaingia mjini alisema nataka niwashushe ili nirudi Tosa kwa jamaa zake ambao alisema wanamsubili huko.lakini pia alikuwa na safari ya kuja dar siku ya jumatatu kwa ajili ya interview ya driving ambayo alisema itafanyika jumanne ila sijui ni kampuni gani.Lakini bahati mbaya sikufanikiwa kuiona ile gari ukizingatia kuwa nilikuwa sijui namba zake wala namba ya simu ya dereva huyo.
 
Niliwapigia simu jamaa zangu ili angalau wanitumie pesa kwa m pesa kwani pale nilikuwa sina hata shilingi mfukoni na tax driver tayari alikuwa ananidai elfu 30,000 kwa kunipeleka  tosa njia panda na kunirudisha mjini.Bahati nzuri nilifanikiwa kupata pesa kwa ajili ya tax pamoja na kunifikisha dar kesho yake jumapili.
 
Ukweli ni kwamba nilidondosha ile walet kwenye gari kwani niliiweka kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yangu aina ya kadet,lakini pia sikuandika namba zozote za simu ndani ya ile walet,pengine naye jamaa alikuwa ananitafuta.Simlaumu kwa aina yeyote ile ila ni bahati mbaya tu ilinitokea.Na nilkuwa nawashirikisha tu yaliyokuwa yamenikuta siku ile.
 
Siku njema
 
 

 
With regards
Mwakigali John

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment