Sunday 16 September 2012

[wanabidii] KENNETH SIMBAYA kwa hili umepotoka

"Yani mnasema nini, hatuwezi kuandika habari za polisi kwani ata
hitima ya Daud Mwangosi bado nyie mnasema nini…" anasikika
mwandshi mmoja wa kike akilia kwa sauti na uchungu katika mkanda
maalumu wa sauti uliorekodiwa katika kikao maalumu baina ya
waandishi wa habari Mkoani Iringa na Rais wa Vilabu vya wanahabari
Tanzania , Kenneth Simbaya.

Kikao hicho kilifanyika siku ya Jumamosi tarehe 14 septemba 2012 saa
9 mchana hadi saa 1 usiku kujadili namna ya kufikia maliadhiano baina
ya polisi na wanahabari hao na kuwaomba angalau waanze kuandika
habari katika juma hili la nenda kwa usalama.

Wanahabari hao waliokusanyika katika kikao hicho walipata taarifa ya
kuombwa kuhudhuria kikao hicho wakiwa hawana mwenyekiti wa klabu
ya wanahabari Iringa mara baada ya msiba wa Daud Mwangosi ambaye
ndiye alikuwa mwenyekiti wao hadi umauti ukimfika.

Msimamizi wa kikao hicho Frank Leonard ambaye ni katibu akiwa jijini
Dar es Salaam aliombwa kuhudhuria kikao hicho ambapo aliweza kufika
na kuwa mwendeshaji wa kikao hicho lakini agenda kubwa ikiwa ni
ombi la Rais wa Vilabu vya wanahabari Tanzania Kenneth Simbaya
kuwaomba wanahabari wa Iringa kurejesha mahusiano mema na polisi
katika mkoa huo uliokumbwa na balaa kwa wanahabri kwa mauaji ya
Daud Mwangosi.

Ombi hili liliunganishwa sambamba na ombi la mlezi wa Klabu hiyo ya
wanahabari Mkoani Iringa Salim Abri ambaye ni Kada wa Chama cha
Mapinduzi akiomba angalau waandishi hao warejeshe ushirikiano huo na
polisi. Lakini kama lilivyo tarajio la wengi wanahabari wa iringa
walisimama imara kupinga kitendo hicho huku wakisema jambo hilo
kufikiwa muafaka ni mapema mno.

"Ata mjane wa Mwangosi ndiyo amerudi leo kutoka Mbeya wala
hatujaenda kumuona , mnasema turejeshe mahusiano na polisi, hiyo
haiwezekani na ni fedhea kwa tasnia yetu ya habari."anasema
mwanahabri mmoja ambaye alikuwemo kikaoni.


Kukiwa na malalamiko kuwa hivi sasa kumekuwa na mbinu za kuwagawa
wanahabari hao huku pia kukiwa na madai kuwa kuna kikundi cha watu
wanaotaka kuneemeka na kujipatia sifa kutokana na msiba wa Mwangosi.

"Kuna mtu mmoja kaja hapa kawaambia jamaa zake mimi ninawaweza sana
waandishi wa habari wa Iringa ndiyo maana tunashawishiwa kuanza
kuandika habari hizo za polisi, mimi binafsi sitofanya hivyo."
anasema mwanahabari mwingine kijana.

Mpaka kikao hicho kinamalizika majira ya saa moja usiku hakukuwa na
makubaliano yoyote kutoka kwa Rais wa Vilabu vya wanahabari Tanzania
, kutoka kwa Mlezi wa Kilabu ya wanahabari wa Iringa na wanahabari
hao. Huku wanahabari wa Iringa wakiendelea kuwa na msimamo mkali juu
ya maamuzi yao.


Lakini swali lililopo ni Je kaka yetu Kenneth Simbaya ambaye ni
mwanahabari wa muda mrefu amabye pia amewahi kuiongoza kilabu ya
wanahabari ya Iringa, pia ninaweza kusema ni mwalimu wetu
aliyetufundisha kuandika habari za kimombo Je, ni jambo gani
limemsukumu kuwaomba wanahabari wa Iringa kuandika habari za polisi
wakati suala hilo likiwa bado liko jikoni? Sili ya hilo na jawabu lake
nadhani analo yeye mwenyewe kaka yetu Kenneth Simbaya.

Wasalaam ndugu yenu Adeladius Makwega.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment