Monday 17 September 2012

[wanabidii] FFU wa Ngoma Africa band watimulisha Vumbi ! AFRIKA-MESSE, Bremen

FFU wa Ngoma Africa band watimulisha Vumbi ! AFRIKA-MESSE, Bremen


Kikosi kazi cha Ngoma Africa band iliyozoeleka kwa katibia zake za
kupagawisha washabiki wa muziki ughaibuni, Jumamosi ya 15.9.2012
kilifanya kweli katika maonyesho makubwa ya biashara ya Afrika-Messe,
mjini Bremen,kule Ujerumani,bendi hiyo maarufu ilipanda jukwaani na 
kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki kwa mara nyingine tena
kwa kuwadatisha akili na muziki wenye raha kamili.
CD za bendi hiyo zimekamata nafasi ya juu katika vituo mbali mbali vya
Redio ndani na nje ya Ughaibuni,baadhi ya vituo vya radio zikiwamo
Redio maarufu nchi Ujeruamani Radio Funkhaus Europa na Radio 
Mult-Kult ndizo zinarusha kwa fujo nyimbo za Ngoma Africa band,
inayoongozwa na kamanda Ras Makunja wa FFU.
Unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao at
http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com

0 comments:

Post a Comment