Tuesday 25 September 2012

[wanabidii] BIG UP SAMAGOAL

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata ameendelea kung'ara baada ya kuinga kwenye orodha ya wafungaji bora 71 duniani sambamba na Lionel Messi, Neymar na Cristiano Ronaldo.

Katika orodha iliyochapishwa jana na mtandao www.iffhs.de inaonyesha Samata anashika nafasi ya 61 baada ya kufunga mabao 6, wakati swahiba yake Tresor Mputu Mabi wanaocheza wote TP Mazembe mwenyewe amekamata nafasi ya 26 baada ya kufunga mabao 8.

Mwanasoka bora wa dunia, Messi wa Barcelona anaongoza baada ya kuzifumania nyavu mara 19, akifutiwa na Neymar wa Santos (16) nafasi ya tatu imeshikwa na Radamel Falcao, Atletico de Madrid (15), wakati Mohamed Aboutreika, Al-Ahly (13 ) akiwa nafasi ya nne, huku nafasi ya tano ikienda kwa Leandro Damiao wa SC Internacional (13).

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshika nafasi ya sita akiwa amefunga mabao 12, sawa na Michael Mifsud (Valletta ), Klaas Jan Huntelaar (FC Schalke 04) na Emmanuel Atukwei Clottey (Berekum Chelsea), huku nafasi ya 10 ikishikwa na Ricardo Oliveira (Al-Jazeera Abu Dhabi).

Orodha hiyo ndefu ya wafungaji bora, inazingatia mabao yaliyofungwa na wachezaji kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Dunia, michuano ya mabara kwa timu za taifa, Olimpiki, pamoja na mashindano ya klabu ya kimataifa.

Uwezo mkubwa ulioonyeshwa na Samata kwenye michezo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndiyo ulimfanya kuingia kwenye orodha hiyo.

Samagoal anakumbukwa zaidi na mashabiki wa soka wa jiji la Cairo baada ya kufunga mabao manne katika mechi mbili alizocheza dhidi ya Al Ahly na Zamalek.

Jambo la kuvutia zaidi katika mabao hayo ya Samagoal yote aliyafunga kwa kichwa kwa mtindo unaofafana wa kuruka juu zaidi ya mabeki wa timu pinzani akiwa umbali wa mita 5 na futi 50.
Baadhi ya nyota waliokuwomo kwenye orodho hiyo na mabao yao

1. Lionel Messi (Barcelona) 19
2. Neymar (Santos) 16
3. Radamel Falcao ( Atletico de Madrid) 15
4. Mohamed Aboutreika (Al-Ahly ) 13
Leandro Damiao (SC Internacional ) 13
6. Cristiano Ronaldo (Real Madrid) 13
7. Michael Mifsud (Valletta) 12
8. Klaas Jan Huntelaar (FC Schalke 04) 12
9. Emmanuel Clottey (Berekum Chelsea) 12
Ricardo Oliveira (Al-Jazeera Abu Dhabi) 12
11. Mohamed Salah Ghaly (FC Basel ) 10
12. Zlatan Ibrahimovic (Milan / PSG) 10
13. Mario Gomez (Bayern Munchen) 10
14. Christopher Wood (Bristol City ) 9
15. Didier Drogba (Ivory Coast ) 9
26 Tresor Mputu (TP Mazembe) 8
33. Edin Dzeko (Manchester City ) 7
48. Robin van Persie ( Man U ) 6
56. Karim Benzema (Real Madrid) 6
61. Mbwana Samata (TP Mazembe) 6

--
Jonas Kiwia  |  Director
Speedy Computers
Tel:+255 754882825  |  Cell: +255 715882825 | 
P.O.Box: 55133  |  Dar esSalaam  |  Tanzania
Email:jonaskiwia39@gmail.com  URL:www.speedycomputersonline.com
 
    

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment