Wednesday 12 September 2012

Re: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z’bar

Tena wotehao wenye kujifanya kuweka mikakati ya kuwaengua Wabara huko visiwani, wameweka makazi yao Bara, litapotokea la kutokea wao na familia zao wako salama huku huku wanakokubeza.

Hovyo kabisa!!

2012/9/12 Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Tatizo ni wao ndugu zetu wapo wapo wengi huku, wana biashara kubwa, mashamba, magari, majumba, borehole za kuuza maji walizounganisha majumba kadhaa kama DAWASA wanauza maji kwa kipato. Hadi Kilombero na Rufiji porini wapo kwa biashara na kilimo kwa sasa. Sidhani kama inasaidia kujenga umoja hasa ukichukulia historia ya utumwa kuwa baadhi ya waliokombolewa walihamishiwa Bagamoyo kutoka Unguja wakalelewa kule wakapewa makazi, walioingia ukristu walihamishiwa Msimbazi na Kigogo-Mission Quarters; wakasoma Msimbazi, Mhonda na Ilonga na wanatembelea ndugu zao ZNZ.
 
Maduka makubwa ya Bagamoyo Mjini ni ya Wakojani kutoka Pemba. Hayo yaliyoanza kuuza TV, madela, baiskeli n.k kabla maduka ya namna hiyo hayajafunguliwa Buguruni, Kariakoo na Mbagala. Mitaa yote ya Bagamoyo kwa mfano kuanzia Mangesani, Mtaa wa Sheikh Rahmiya hadi Pwani hospitali na Kaole kila nyumba ina ndugu au ukoo huko ZNZ. Bado hao wapemba waliokuja majuzi kibiashara na waunguja wa miaka mingi ambapo shoping ya watu wa Bagamoyo toka zama za Sultani ni Unguja ambapo ni kilomita 25 za maji kutoka Bagamoyo Pwani ufukwe wa bahari. Wakata mikoko Rufiji, Bagamoyo na Mafia inayotumika kujenga vyombo vya bahari, kusafirisha uarabuni ugomvi zaidi ni watu kutoka ZNZ. Zaidi yao wao kuwa na vyombo vikubwa vya kienyeji vya usafiri na uvuvi baharini (mashua, Jahazi vinavyovua samaki, pweza etc na kusafirisha abiria na mizigo bahari) hakuna tena bongoland labda Vyombo vitengenezwavyo Kisiwa cha Jibondo Mafia. Hivyo wabara sio loosers sana kama kukataza mobility na uhamiaji itakuwa dhana na sera hizi za vitambulisho. Liko linalotafutwa. Kitu gani hasa TZ Bara kama nchi inayokitaka isirudishe serikali ya Tanganyika kukawa na nchi 2 ili muungano uwe wa tatu. Lakini kabla ya yote, kila mtu awe na kitambulisho cha nchi na uraia wake. Itakuja soon, ugomvi wa mipaka ya bahari kama malawi na lake nyasa yake.
Mungu atusaidie.

From: Monica Malle <moninaike@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroup <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, 12 September 2012, 12:14
Subject: RE: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z'bar

Na  Wazanzibari walioko bara nao wahesabiwe kama wageni? au watanzania?
 
From: c.kudoja@zantel.co.tz
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z'bar
Date: Wed, 12 Sep 2012 08:53:08 +0000

 
 
 
 
 
12th September 2012
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini
Watanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.

Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.

Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, Oktoba 10 mwaka huu.

Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.

Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.

Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.

"Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii," umesisitiza muswada huo.

Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.

Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.

Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.
SOURCE:IPPMEDIA
No virus found in this message.
Checked by AVG - http://www.avg.com/
Version: 2012.0.2221 / Virus Database: 2437/5263 - Release Date: 09/11/12

This email is Virus free! Has been Scanned.
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment