Thursday 13 September 2012

Re: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z’bar

Tukitaka kuwa wakweli budi kuongea ukweli katika jamii ili tubadilike. Tukipita katika tafiti majumbani inakuwa tabu sana kuingia nyumba zao. Malalamiko yanatolewa pia na viongozi wa Mitaa jinsi ushirikiano unavyokuwa mgunu nao. Aidha unaambiwa mwenye nyumba hayupo ndani lakini yupo hataki kuhojiwa; au unachunguliwa kutoka upenyo wa mlango unaambiwa'haituhusu' wakimaanisha utafiti unahusu wabara. Wachache sana hushirikiana vizuri mitaani na katika majumba ya sala kama siko kuwa na maendeo ya jumba hili la sala wa waafrika wa bala, hili waarabu na wahindi na wa ZNZ, hili la matajiri sana na viongozi labda wa serikali vitu ambavyo katika dini zetu tuviangalie 'Class zipo'.
 
Tatizo la watu weusi ila akina babu  wamechanganya damu karne ya 600-1000 AD  lipo nchini na katika mwambao wa pwani, visiwa vyetu na hata visiwa vilivyo Tanzania bara (Mafia na visiwa vyake 7), Pangani, Kilwa Kisiwani na maeneo ambapo wanaishi watu waliochanganyika (Kilosa, Tabora etc). Bado ule ukabila uliopo ambao hatuuongelei ila upo na ethnocentrism yake na udini ambao unakuwa donda sugu la cancer hata miale ya ocean road itashindwa wa kumwagia watu tindikali, kuwachomea nyumba, biashara na makanisa.
 
Tuone mifano kwa nchi nyingine wanavyobomoa majuma na miundo mbinu, kutiana vilema na umasikini wa kudumu kisha wanakimbilia ulaya na nchi zetu kutukorofisha amani wanayoivuruga wenyewe kwa visingizio. Tusishabikie utengano, tushabikie umoja na tuuweke katika mitaala ya kufundisha kuanzia vidudu hadi vyuo vya juu. kwani kwa sasa umoja na historia yetu haifundishwi tena kama zamani. Mikutano ya hadhara ni kuhubiri chuki tu, mapigano, mapambano, mapigano kuwa ndio mbinu ya dialogue na ya kurekebishana. Ikitumika sheria mtu anatishiwa uhani si katika siasa tu mpaka mitaani majumbani au mashambani. Huwezi kumuambia jirani yako anakosea anatupa uchafu kwako au kasogeza mpaka au anatiririsha maji machafu yanawakera. Hapo ni kujitafutia kifo au kisasi. Ndio haya ya kukomoana na muungano ambapo huenda bara ina bili za umeme wa Tanesco huko ZNZ za karne inadai zinasamehewa ili kulinda muungano. Tufundishe na kuhubiri upendo. Tuonyeshe vijana na watoto wetu sinema za CD za vita badala ya CD za mapenzi na vituko vya mzee majuto. Vijana hawaelewi au hawaoni majumba ya ghorofa yanavyowaka na kuzika watu, maiti zinazoelea au kuoza na vilemaa wa vita na watoto wanajeshi walivyolewa bangi na kuchinja watu pamoja na ndugu zao na wanavyosimulia shuhuda zao za mateso yao kama child solders. Zionyeshwe mara nyingi ktk TV na mashuleni ili watoto wajue vita si neno nu ni tukio baya kama la huko Tana River-waone mapigano hayo. Hawaelewi mateso ya wale wanaopelekwa uarabuni kufanya kazi za ndani na ubaguzi wa rangi na utaifa uliopo within Africa na nchi za ulaya. Sio vyote ving'aavyo ni dhahabu na sio wote watakao utengano na mapambano kwa jina la demokrasia wanatutakia mema. Wao watahamishia watoto wao na jamaa zao ulaya kwa vibaraka vyao kabla ya mapigano wayashabikiayo kuanza. Mungu atusaidie.Wamarekani sasa wanavuna walichopanda Libya, Misri na nchi nyingine. Wapiganaji waliopewa silaha ktk kusaidiwa kupata demokrasia, sasa wanazitumia kuwabonda wao wenyewe.Nasi tunaelekea huko? Tusifike huko.
 
 
 

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, 12 September 2012, 17:13
Subject: Re: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z'bar
Dawa yao ni kuwalimit kwenye mambo ya Mungano. Tuanzie Bungeni. Yakiisha ya muungano wakaambiwa wapishe utaona busara zitaanza kufanya kazi

--- On Wed, 9/12/12, Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com> wrote:

From: Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z'bar
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, September 12, 2012, 6:07 AM

Abdurahman,Huoni Tatizo, kwamba Mtanzania wa upande mmoja wa muungano anapoingia sehemu moja ya muungano anakuwa na hadhi tofauti, na wakati huo huo mwenzie anapokuja upande wa pili naye hadhi yake haibadiliki,!!Tuwe wakweli, tatizo la ndugu zangu Wazanzibari ni hulka ya ubinafsi linapokuja suala la pande mbili hizi za muungano, kwao changu chtu bali chao ni chao wenyewe. Muungano kwao ni pale wanaponufaika wao kwa fursa za Bara lakini zile za Zanzibar zinabaki zao peke yao!!Felix
2012/9/12 ABDULRAHMAN ABDULRAHMAN <http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=manidedes@yahoo.com>
Wana ndugu,
 
Nimejaribu kusoma maandishi yanayoowa taarifa za waziri wa Zanzibar kuhusu vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi kwa wenyeji na wageni. Lakini sikuona tatizo lolote katika hilo linalosababisha watu kuponda na kurushiana maneno.
 
Naomba mnisaidie tatizo ni nini?
From: Felix Mwakyembe <http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=fkyembe@gmail.com>
To: http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, September 12, 2012 1:05 PM
Subject: Re: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z'bar
Tena wotehao wenye kujifanya kuweka mikakati ya kuwaengua Wabara huko visiwani, wameweka makazi yao Bara, litapotokea la kutokea wao na familia zao wako salama huku huku wanakokubeza.Hovyo kabisa!!
2012/9/12 Hildegarda Kiwasila <http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=khildegarda@yahoo.co.uk>
Tatizo ni wao ndugu zetu wapo wapo wengi huku, wana biashara kubwa, mashamba, magari, majumba, borehole za kuuza maji walizounganisha majumba kadhaa kama DAWASA wanauza maji kwa kipato. Hadi Kilombero na Rufiji porini wapo kwa biashara na kilimo kwa sasa. Sidhani kama inasaidia kujenga umoja hasa ukichukulia historia ya utumwa kuwa baadhi ya waliokombolewa walihamishiwa Bagamoyo kutoka Unguja wakalelewa kule wakapewa makazi, walioingia ukristu walihamishiwa Msimbazi na Kigogo-Mission Quarters; wakasoma Msimbazi, Mhonda na Ilonga na wanatembelea ndugu zao ZNZ.
 
Maduka makubwa ya Bagamoyo Mjini ni ya Wakojani kutoka Pemba. Hayo yaliyoanza kuuza TV, madela, baiskeli n.k kabla maduka ya namna hiyo hayajafunguliwa Buguruni, Kariakoo na Mbagala. Mitaa yote ya Bagamoyo kwa mfano kuanzia Mangesani, Mtaa wa Sheikh Rahmiya hadi Pwani hospitali na Kaole kila nyumba ina ndugu au ukoo huko ZNZ. Bado hao wapemba waliokuja majuzi kibiashara na waunguja wa miaka mingi ambapo shoping ya watu wa Bagamoyo toka zama za Sultani ni Unguja ambapo ni kilomita 25 za maji kutoka Bagamoyo Pwani ufukwe wa bahari. Wakata mikoko Rufiji, Bagamoyo na Mafia inayotumika kujenga vyombo vya bahari, kusafirisha uarabuni ugomvi zaidi ni watu kutoka ZNZ. Zaidi yao wao kuwa na vyombo vikubwa vya kienyeji vya usafiri na uvuvi baharini (mashua, Jahazi vinavyovua samaki, pweza etc na kusafirisha abiria na mizigo bahari) hakuna tena bongoland labda Vyombo vitengenezwavyo Kisiwa cha Jibondo Mafia. Hivyo wabara sio loosers sana kama kukataza mobility na uhamiaji itakuwa dhana na sera hizi za vitambulisho. Liko linalotafutwa. Kitu gani hasa TZ Bara kama nchi inayokitaka isirudishe serikali ya Tanganyika kukawa na nchi 2 ili muungano uwe wa tatu. Lakini kabla ya yote, kila mtu awe na kitambulisho cha nchi na uraia wake. Itakuja soon, ugomvi wa mipaka ya bahari kama malawi na lake nyasa yake.
Mungu atusaidie.
From: Monica Malle <http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=moninaike@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroup <http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, 12 September 2012, 12:14
Subject: RE: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z'bar
Na  Wazanzibari walioko bara nao wahesabiwe kama wageni? au watanzania?
 
From: http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=c.kudoja@zantel.co.tzTo: http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.comSubject: [wanabidii] Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z'barDate: Wed, 12 Sep 2012 08:53:08 +0000
 
 
 
 
 
12th September 2012
http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Mwinyihaji%20Makame%281%29%281%29.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini
Watanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.

Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.

Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, Oktoba 10 mwaka huu.

Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.

Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.

Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.

"Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii," umesisitiza muswada huo.

Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.

Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.

Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.
SOURCE:IPPMEDIA
No virus found in this message.
Checked by AVG - http://www.avg.com/
Version: 2012.0.2221 / Virus Database: 2437/5263 - Release Date: 09/11/12
This email is Virus free! Has been Scanned.
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  


--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda http://us.mc1612.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  

0 comments:

Post a Comment