Monday 10 September 2012

Re: [wanabidii] UWEKEZAJI WETU

Ahsante sana kwa kutukumbusha Nd Kessy. Inauma sana.
 
Unapoona familia wanapochangia arusi kuliko shida ya mtoto kusoma awe hata mmoja aliyetelekezwa na mzazi au mzazi hajiwezi ila ndugu kuwa na majungu na kuchangia vingine kuliko vile vya msingi.
 
Upoona kuna matajiri wenye fedha za kutupa kuchangia siasa na vyama vya mpira, lakini sio kuungana kuunda kampuni ya kuchimba madini, kuajiri vijana waliosomea madini, kununua mashine kutoka nje na kuajiri wataalamu toka nje kuja kuwapa vijana uzoefu. Tunasubiri wawekezaji.Wakija-milolongo mirefu ya rushwa. Akitaka kuchimba madini hapa au pale-tayari afisa ardhi au madini ana title pale ili alipwe mabilioni kumbe ni ubinafsi tu.Wawekezaji wanakimbia au wakiingia nao wanakuwa wabadhirifu kupitia mianya ya rushwa wanayojifunza na kusaidiwa kuwa hivyo.
 
Unaona jinsi mtu anavyolima nyanya kwenye mabonde na kujaza lori kuzileta sokoni DSM na miji mingine,lakini hapo kulimwako nyanya hizo wapo waliokaa kitako hapo kijijini kutwa kusubiri vishuke kutoka angani hao wajishughulishao kama wajinga hivi!! Huyo jirani alimaye nyanya, matango, kabichi hamuoni-ila asubiri kumuibia usiku na vijana wake kutwa wapo chini ya mti wanavuta bangi eti kazi hakuna-nyanya hizo jirani hapo mbona anavuna malaki ya pesa?
 
Watachangia mazishi ya ufahari-sio kuuguza bali kungoja kuuza hiyo ardhi na vibanda vyake. Kwa wafugaji, sio kuuza mifugo na kusomesha bali kukioza umri miaka 12 kiongeze mifugo na watamchangia hasa mifugo akioe kichanga au watachangia arusi ya kifahari. Kwa mkulima, akiuza nazi, korosho, magunia ya mpunga-anaongeza mke au sherehe ya mtoto-maurid, ekaristi ya kupotesa fedha. Wenye hela watachangia milo siku ya Eid-Iftah ya kula mamilioni siku moja leo kulisha kundi hili kesho lile; kugharimia ubwabwa wa kristmas lakini sio kuchangia kitu cha kudumu cha msingi cha hao yatima kujitegemea-mfano kuwajengea makazi yenye shule na madarasa ya ufundi na shughuli za kilimo cha bustani kwa kutumia drip irrigation; kuwawekea banda za kuhifadhi mazao, banda za mifugo ya kisasa ya maziwa, kuweka makazi ya walimu wa ufundi, kuleta peace corps wenye ujuzi na shule ikawa ya mfano badala ya mamilioni ya fedha kulisha kundi hili leo, kesho hili etc.  Kala leo kesho atakula nini?-Mpaka kristmas, Iftah ya Eid ijayo mwaka kesho?
 
Mabonde mazuri ya kilimo cha mpunga na mazao kibao-twaingiza wafugaji toka Burundi kuwapa makazi, kufuga mifugo yao na kukata miti. Kisha tunalalamika tunanyanyaswa na wageni-kawaingiza nani kijijini kwenu? Aliwachagua nani uongozi? Kwao mnathubutu kuingia kulima na kufuga? hatujifunzi?
 
Unavuna madini unalimbikiza mifugo ukiwa unafahamu pia kuwa hata ardhi ina kiwango chake cha kubeba mzigo. Maghorofa yanajengwa kubanana na kuzima barabara za mitaa unaangalia kama Afisa Ardhi na ujenzi. Moto utakapotokea utasaidiaje? Unajali kodi za majengo tu sio usalama kiafa na moto. Majumba makubwa yameziba hewa madogo!! Yanachimba visima vya maji (Boreholes) nani katoa certification? Matokeo yake ni fracture ardhini na majumba hayo ya ghorofa kuporomoka kuziwa watu serikali ianze kutumia mamilioni kufukua watu badala ya kuzuia kabla ya kutibu. Hayo maghorofa yasiyopimwa usito, yanayooteshwa kama uyoga ina maana hamyaoni wahusika. Upofu wa leo-gharama ya Taifa kesho.
 
Unajenga hoteli mwenge, mikocheni unaingiza fedha za kutosha-unajua unatakiwa uunganishe mabomba yako ktk Mabomba ya DAWASA ya Maji Taka-hufanyi hivyo, hutaki kulipia gharama na kodi ya mwezi, unaunganisha ktk mfereji wa wazi wa maji ya mvua. Jirani wakilalamika-unatoka na pistol kuwatishia. Kesho, unaleta wakaguzi wa leseni kuwatesa hao jirani wenye viduka na vigenge kwa vile unapesa. Maji machafu yanayozalisha mbu wa matende yanazagaa, miji michafu mitaro malundo ya taka na maji machafu hakutezamiki ukiulizwa-serikali. Wewe na matendo yako ya uchafu, ubadhilifu, upandaji mbegu mbaya ya rushwa hujiangalii. Kama kila mmoja ndani ya familia angekuwa mshauri wa mwengine, mkali mtaka familia kuwajibika, kukaripia maovu na kupenda usafi, haki na usawa kusingekuwa na matendo maovu ktk jamii.Ila, kuukataa ukweli, kupenda kuongea tu na lawama juu, uvivu, kujifanya kujua wakati hujui unahitaji ushauri, uvivu na kutegemea kuletewa, uharibifu wa raslimali, kushabikia mapungufu na kuyakuza karne badala ya kusonga mbele, kupenda kutesa au kuumiza wengine kwa kupata raha mwingine atesekapo, umangimeza kwa kutaka mtu akuhonge au akuone kuwa wewe ndio mwenye madaraka ndio kumetufikisha hapa tulipo. Vi-nchi vidogo vitapigana vita vitatupita na vitatushinda.Maneno mengi kuliko matendo imeua na inaendelea kuua vikundi vingi vya umoja ambapo kila mmoja anataka kutumia umoja huo kufaidika binafsi kuliko kutumia kikundi kukua kiuchumi kwa kumuinua mmoja, kuchukua mkopo benki akaiunuka mwingine na baadae wakawa na miradi binafsi na mmoja wa kampuni yao badala ya kikundi na wakaajiri watoto wao wasomi kuendesha kampuni. Ni wachache sana kufanya hivi kwa waafrika labda wahindi. Inaumiza sana moyoni mwa wengine.
 
Bado hiyo mercury tunayokunywa daily kupitia maji ya Ruvu, Ruaha, Pangani, Kilombero na mito mingine. Migodi ya dhahabu kila mara na kuoshea ni mtoni twanywa maji hayo vijijini na mijini.Wape maelekezo ya afya-nani azingatie ni lawama tu; nani ajikinge na madhara hayo ya zebaki-hawezi kujikinga kwa utumia condom ataweza kujikinga kwa matumizi ya zebaki yatakiwayo? Akizaliwa kilema asiye mikono na miguu kamilifu-twakimbilia kutaka kumuiba tunaona ndio dili la kupatia hela. Bongoland hatari, sijui kama tutafika ktk malengo yetu hata yale ya 2025. Yatubidi haswa kubadili mtazamo wa maisha ama sivyo tutazidi kuvuna kibovu tunachopanda ktk uwekezaji wetu mbovu kiakili na kimaisha.

From: Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, 10 September 2012, 19:50
Subject: [wanabidii] UWEKEZAJI WETU

Yabidi tubadili mtazamo wa maisha.
 Tutavuna tunachopanda!

It is indeed rather too much.
 

 

 
 
 
 






--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment