Wednesday 12 September 2012

Re: [wanabidii] UWEKEZAJI WETU


Kuchangia kuoa kuliko kusoma kutokana na utility value ya kuoa ina prons na cons zake.
 
Wale ambao hutumia mifugo kuoa zaidi au kuoza na kulimbiliza mifugo si ndio hao wanaolalama kuonewa na GVT kwa kuwa na elimu duni? Shule ya kwanza ya secondary kuwa na computer ni ndani ya Ngorongoro iliyohisaniwa. Utapata historia za shule na zahanati kukosa watoto au watu wa kutibu wamehama na wazazi wafugaji. Kitwai A village Manyara kuna zahanati na shule, kunakipindi walihama miaka kadhaa wakaja kurudi baadae.
 
Mtu unaweza kuhoji, Elimu ikiwa duni uwakilishi ktk vyombo vya uwakilishi vya juu utakuwaje?
 
Na sasa tunahitaji mbunge angalau awe amefika form 6 ili aweze kuwa na uwezo wa kusoma makala mbali mbali za kisheria kwa lugha angalau 2 sio kujua kilugha tu. Ndipo utakuta kule ambako watu wamesoma madrasa tu wanasema wanaonewa ktk uwakilishi na ajira. Ukijua lugha ya dini tu iwe kikristo (kilatini, English) au ya kiislamu bila kuwa na lugha yenye elimu dunia ndani yake (Kiarabu na masomo ya hisabati,uinjinia, chemistry, geography etc) au kilatini bila sayansi za elimu dunia utaishia kufundisha dini tu na dini haiajiri wengi.Labda uwe hukusoma elimu dunia lakini u milionea au tajiri uwe na kampuni uajiri wasomi (kama wafanyavyo waarabu matajiri wa mafuta kuajiri makampuni ya wazungu na wazungu). Wasiosoma elimu dunia wengi haimaanishi ni masikini-wana mashamba ya mazao, minazi, majahazi na mashua, wavuvi, wana mifugo. lakini kuendeleza utajiri kisasa tk karne hii ya utandawazi na kumudu ushindani duniani kwataka kusoma au usomeshe ili mazao yako ufunge vizuri, yasiwe na residual chemicals, lebo zitakiwazo usafirishe yakubalike.
 
Ni kukataa kuwajibika ndio kunatufanya tuchukue short-cuts.Elimu dunia husaidia tu katika mengi sio kama ndio solution ya kila kitu kwani elimu bila kujituma, busara na uaminifu, ukweli na kuzingatia sheria husika na misingi mizuri ya maisha  ni sawa na wendawazimu.Kama elimu ingekuwa ndio solution kwa kila kitu tusingekuwa na high rates za HIV/AIDS kwa wasomi, wanandoa wafundishwao uaminifu na kuona wavunjaji sheria ambao baadhi yao ni wanasheria, police au wanajeshi, watu wa Mungu au kuwa na watu wauao wenzao kwa kutumia dini kama kisingizio (anasema-Mungu mkuu-anatupa bomu linaua mtu, kubomoa nyumba na kuzika watu, kuchoma watu ndani ya makanisa, kupigana vita kwa jina la yesu huku anaua watu ndio alete demokrasia) kama elimu nayo inasaidia akina kibwetere na wafuasi wao wasingekuwepo. Wala wasomi wa ulaya waliotuletea Biblia wasingepitisha sheria ya ndoa za jinsia moja za kufungiwa Kanisani.  Hawa wamesoma na wanajua Biblia inasemaje.
 
Wapo waliofindishwa kuhusu SACCOS matumizi na sheria zake na madhara ya matumizi mabovu ya mkopo. Tuliwakuta mwanamke kachukua mkopo bila ya kumuarifu mume, siku ya kuchukuliwa vyombo nyumbani kwake alitoroka asirudi na kumuacha mume na familia. Wapo waume  waliooa waliofanya hivyo pia na kumuacha mama na watoto akatokomea. Kisa-alichukua laki 3 tatu au 5 akatumia na kimada au akanunua khanga na heleni za dhahabu, anakimbia aibu hakumueleza mwenzake. Kwa sasa mikopo ya SACCOS mke au mume lazoma naye ajaze fumu hiyo atie sahihi ili kulinda ndoa. Kutokuwa na mipango ya sasa na baadae ya maisha. Una mipango na mtazamo gani wa maisha yako? 
 
Mtu anafahamu kabisa kuwa huruhusiwi kujenga mashimo yaliyochimbwa mawe, vibao vinaweka na matangazo, hutakiwi ujenge barabarani au uzibe njia kati ya nyumba na nyumba kwa ajili ya usalama wa moto. Unajenga jumba la fahari. Unajiona unazidi kabisa kuchukua barabara, kwa akili yako timamu. Kesho unakuja kuvunjiwa. Hata kama una hela na umezoma-hii inakusaidia nini badala ya kukutia hasara? Kama hukusoma huna elimu-hata kuona huoni, hata mifano ya kubomolewa wengine huelewi pia-Kichwa pumba au upofu! Sasa hao wanaouana kila siku na kuchomeana nyuma Tana River Kenya-hawaoni madhara yake ktk kujitia vilema na umasikini. Ni ujinga uliokithiri, tamaa, wenda wazimu wa kisiasa, ni nini hasa. Na tunavyochukua silaha na kuuana wenyewe kwa wenyewe miaka nenda miaka rudi Congo ni kukosa elimu, kutokuona mifano, ujinga au tamaa? watupao silaha wanavuna madini sisi vilema, ukimwi yatima-kusaka demokrasia. Elimu pekee kwa karne hii bila busara haisaidii.Na kutokusoma-ni tatizo kubwa sana pia maana ndio tunakimbilia kuua albino, vizee, ushirikina ndio solution ya kupeta kibiashara badala ya kujiunga na kutumia hizo SACCOS effectively and efficiently.
 
Hata michango ya arusi au ya kifo muangalie sana-kuna vilaza ambao hukusanya lakini kuzibania mifukoni mwao. Anaweza pia akachangiwa ofisini laki 3+ kuwa amefiwa na mzazi au mtu wake wa karibu, akifika home kilioni akatoa mchango wake elfu 20 badala ya zote au nusu ya hela ofisi yake iliyompa. TAMAA tumeweka mbele kuliko utu na ukweli.
 
Huwa inatia kichefuchefu unapoangalia mali iliyopo TZ na Africa halafu jinsi tulivyo biashara kichaa.
From: Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, 12 September 2012, 8:08
Subject: Re: [wanabidii] UWEKEZAJI WETU

Hi Herment
nakubaliana na maoni yako. Siku moja nilikuwa kwenye mkutano wa wafanyakazi wa sekta fulani binafsi. Kilichokuwa kinahamasishwa ni kuanzishwa kwa SACCOS  ya sekta hiyo.

Mtu mmoja alisimama na kusema "NINYI WASOMI MNATUDANGANYA TU. MNATAKA KULA HELA YETU"

Nilishtuka  kweli na kauli ile kwani iliungwa mkono na wengi. Kumbe kusoma katika jamii inaonekana ni kiini macho cha kuwaibia wasiosoma. Tukiangalia wanasiasa wetu, Madaktari na waalimu wanaogoma na kudai mambo mbali mbali; kwa mtu asiyekuwa na upeo anaona YA NINI KUCHANGIA WATU WAPATE ELIMU maana wanakuja kutugeuka baadae.

Hivyo wasomi wawe na muone wa Nyerere kuhusu kijiji kilichokuwa na njaa ya kufa mtu..."WATU WALICHANGA KIDOGO WALICHOUWA NACHO KUMCHANGIA MMOJA KUSAFIRI MBALI...... ili aje kuwaokoa"

Kazi ipo!


From: Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, September 10, 2012 11:58 PM
Subject: RE: [wanabidii] UWEKEZAJI WETU

Wanabidii,

Hao wanaochangia sherehe za harusi kwa wingi zaidi kuliko kuchangia kusoma wana sababu za msingi.  Sababu kubwa ninayoiona hapa ni utility au satisfaction mtu aipatayo kwa kujumuishwa na kusherekea na wenzake ina value zaidi kuliko kuchangia kusoma.  Watu wanajiuliza hao waliosoma wamefanya nini, wamechangia kubadili maisha ya mtu binafsi na mtanzania kwa kiasi gani. Je mchango huo una utility au satisfaction inayolingana na kusherekea na kupata temporary relief of stress, anxiety and anger mtu aliyo nayo towards life in general. Kila kitu kinafanyika kwa sababu fulani na tukipata sababu hiyo basi tumepata dawa ya kutibu hicho kinachotokea kukibadilisha kuwa positive kama ni negative.

Bila kuonyesha wazi wazi kuwa kusoma kunaleta faraja zaidi kuliko kuchangia kuoa watu wataendelea kuchangia kuoa.

Tutafakari jambo hili na tulizungumze tupate muafaka hwenda likatusaidia kubadilisha tabia, maono na preference zetu za kimaisha

Ahsante

Herment

Date: Mon, 10 Sep 2012 20:13:43 +0300
Subject: Re: [wanabidii] UWEKEZAJI WETU
From: mngonge@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Lazima kuna kitu kinachowasukuma

On Mon, Sep 10, 2012 at 7:50 PM, Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com> wrote:
Yabidi tubadili mtazamo wa maisha.
 Tutavuna tunachopanda!

It is indeed rather too much.
 

 

 
 
 
 







Lazima kuna kitu kinachowasukuma kuwekeza kwenye bakuli la kuoa kuliko la Elimu. Utamaduni wetu toka enzi za mababu unahimiza kuchangia chakula na pombe wakati wa sherehe na misiba. Wenzetu Kenya walikwishaondokana na hizo mila lakini sisi mmmhuu. Ukianza ubishi wa kisiasa na kidini mtaani utagundua kwamba bado tuna tatizo sugu na hivyo kuchangiana mambo ya msingi itachukua muda mrefu.

Kazi ipo




 
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment