Thursday 13 September 2012

Re: [wanabidii] UTATA KUHUSU URAIA WA SHEIKH PONDA

Kinachomfanya mtu awe raia wa Tanzania si uwepo wa wajomba au mashangazi hapa nchini. Unakuwa raia ama kwa kuzaliwa au kwa kujiandikisha kwa maana ya kuomba uraia kama wale wakimbizi wa Burundi waliopewa uraia wa Tanzania. Inawezekana Sheikh Ponda si mtanzania lakini sababu haiwezi kuwa yeye kutokuwa na shangazi wala mjomba hapa nchini. Kwani watoto wanaookotwa majalalani kila siku na kutunzwa kwenye vituo vya ustawi wa jamii tutawanyima haki ya uraia kwa sababu hatujui wajomba wala shangazi zao? Kumejithihirisha kwa siku za hivi karibuni ugonjwa wa kusingizia watu uraia hasa pale inapoonekana ni tishio kwa masklahi fulani au vigumu kuwadhibiti kwa hoja. Tusipoteze muda mwingi kudili na watu! tudili na hoja zao!

Alex.


From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, September 13, 2012 12:29 PM
Subject: [wanabidii] UTATA KUHUSU URAIA WA SHEIKH PONDA

Ndugu zangu

Nimesikia katika vyombo vya habari kwamba Baraza la waislamu Tanzania
limetamka kwamba Mwanaharakati maarufu wa kiisilamu tanzania Sheikh
Issa Ponda sio raia kwa sababu hana mjomba wala shangazi .

Pamoja na Tuhuma hizi Sheikh Issa ponda mwenyewe hajaja mbele kuuambia
umma kuhusu utata wa uraia wake , mimi nafikiri ni wakati mzuri kwa
sheikh ponda kuthibitisha uraia wake kwa kutoa nyaraka muhimu mapema .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment