Tuesday 18 September 2012

Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Ungelitegemea Kigwangalla aseme nini kuhusiana na ujumbe wa mchumia tumbo, eti Kigwangalla anasema chuki dhidi ya CCM, huku Bakari anasema Serikali ilisahau kutoa agizo mapema, ilisahau? 


From: "hkigwangalla@gmail.com" <hkigwangalla@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, 18 September 2012, 21:44
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Bariki, umechambua vizuri sana, very fairly and squarely! Wengi hapa wamejaa ushabiki na chuki dhidi ya CCM na serikali yake na hivyo hata hoja nzuri za Hizza hawawezi kuziona, hata hoja potofu zenye mapungufu, za Hizza hawawezi kuziona!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 17 Sep 2012 12:02:53 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Ni tamko zuri ila limejaa kasoro nyingi mojawapo ni ile ya kusema kufanya mkutano/maandamano. Kwa mujibu wa hali halisi ilivyokuwa, kilichofanyika ni ufunguzi wa tawi jipya na pia suala halikuwa kusubiri Sensa iishe bali suala lilikuwa ni wao chadema kuendelea na shughuli zao za kisiasa ambazo zilipangwa mapema zaidi kama ambavyo Sensa ilivyokuwa imepangwa. Tofauti kubwa ni kwamba Serikali ilisahau kutoa kauli ya kuzuia shughuli za kisiasa wakati wa Sensa tangu awali na hivyo kutoa tamko wakati wa Sensa umekaribia inazua tafsiri mbaya zaidi kwa baadhi ya watu.

Mimi kama mwananchi ambaye kwa sehemu nimeelimika, lazima wadau wote wakiri makosa....kuanzia wananchi hadi Serikali yenyewe. Hivi nini kilishindikana kwa wahusika kutoa kauli ya kuzuia shughuli zote (mikutano na mikusanyiko yote ikiwemo ya Dini) wakati wa Sensa? Kauli ambayo ilipaswa itolewe hata ingewezekana mwaka jana ili watu wanapopanga shughuli za kila siku wajue kipindi fulani hakipaswi kuingiliwa??? nafikiri tusiangalie tatizo lililotokea bali tuangalie kiini cha tatizo. Kama ni watu wa mipango mbona tupo tumejaa na wala haiumizi kichwa kupanga. Suala la kupanga ni tatizo hata kwenye uongozi wa michezo ndiyo maana mechi kila siku zinabadilishwa wakati wenzetu Ulaya mechi itabadilishwa kutokana na hali ya hewa kubadilika lakini si vinginevyo.

Tubadilike kwanza ili mwingine akikosea tumpe adhabu ya milele

2012/9/17 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
NA RICHARD TAMBWE HIZZA

WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini
waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha
Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa
mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana
kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika
kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la
polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa
yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na
kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa
vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya
majimbo 239).

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana
na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi
waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa
habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa
kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote
hatukuyategemea.

Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na
msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki
baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania
ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo.
Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania
wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa
na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri
sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea
na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la
polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia
wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo
walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je,
uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la
kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa,
najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano
na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo
inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi
kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).

Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima
wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha
kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi?
Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa
mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria
dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo
Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa
ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na
mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua
ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya
nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo
kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu
ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria
viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata
upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria
inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.

Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha
mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je,
ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza
sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha
kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu
Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka
katika taasisi zetu za habari?

Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko
lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini
wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na
kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani
tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao
wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na
vyombo vyake?

Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea
kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko
ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida
sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa
katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama
zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.

Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji
ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika
shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira
hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment