Monday 17 September 2012

Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Naomba kumwuliza swali Mzee Richard Tambwe Hiza; Hivi ni kwa nini mikutano yote inayoandaliwa na CCM, askari wanatoa ushirikiano wa ziada kuhakikisha mikutano inafanyika kwa amani, mpaka waajiriwa wakuu wa kiserikali wanaacha kufanya kazi za kiofisi wakienda kwenye mikutano hiyo, wakitumia magari ya serikali! Na, kwenye mikutano hiyo Polisi hawabebi hata virungu, zaidi ya radio calls. Lakini kwenye mikutano ya Wapinzani! Lahaula!! Hata silaha ambazo hazijawahi kutolewa armoury zitatolewa siku hiyo. Kuna mizania ya usawa hapa? Kwa sababu hata maelezo yako hapo chini yanaonyesha jinsi ulivyolalia upande mmoja.
 
Amazia.

From: lucas haule <kisacha2003@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, 17 September 2012, 2:01
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA
Kwani ile nafasi ya kuropoka pale ccm lumumba bado ipo, tambwe huyu ajawahi kujiuliza swali sahihi?

--- On Mon, 9/17/12, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, September 17, 2012, 1:49 AM

NA RICHARD TAMBWE HIZZAWIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchiniwaliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo chaChanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwamara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautianakifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katikakukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi lapolisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwayaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi nakujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwavibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati yamajimbo 239).Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokanana msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishiwaliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wahabari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwakuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wotehatukuyategemea.Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana namsiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chukibaina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzaniaambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo.Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzaniawote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwana nini/nani?Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubirisensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokeana yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi lapolisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuiawasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalowalikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je,uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu lakutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa,najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamanona mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyoinasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizikutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzimawamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimishakufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi?Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaamapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheriadhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyoTundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpaushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa namgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavuaubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani yanchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambokwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababuya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheriaviliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipataupinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheriainafuatwa na utekelezaji wake unatimia.Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribishamwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je,ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokezasehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo chakutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetuMwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutokakatika taasisi zetu za habari?Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamkolililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa niniwanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria nakuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhanitunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au naowameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali navyombo vyake?Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendeleakushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomokoili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaidasheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwakatika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakamazitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitajindugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katikashughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasirahasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.comKujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+http://us.mc1133.mail.yahoo.com/mc/compose?to=unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatumaDisclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  

0 comments:

Post a Comment