Monday 17 September 2012

Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Tukiamua kuwa huo ndio uwezo wa hiza wa kufikir basi watu kama hawa wanastahili'kuhasiwa' ili kuua mbegu-uzao wao. kwa kweli ni hatari kuliko.
Kama mtu aliyeonja darasa kama yeye anaweza kuandika hiki alichofanya akadiriki kukitoa hadharani lazima mtu huyu ni hatari. Na huu ni udhaifu wa siasa zetu. maana ipo siku unaweza kumkuta mtu kama huyu anagombea Urais anapata.

--- On Mon, 9/17/12, Gaston Mbilinyi <mbilinyi.gaston49@gmail.com> wrote:

From: Gaston Mbilinyi <mbilinyi.gaston49@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, September 17, 2012, 8:52 PM

Nimesoma hoja na sijaelewa kama ambavyo viongozi wetu hawajui kwanini
Watanzania tu masikini!

Ila hoja hii imenikumbusha kuwa adui wetu Mkuu anayeitwa UJINGA bado
ni tatizo kubwa nchini!

Chuki ya mtoa hoja dhidi ya CHADEMA imemfanya atoe povu jingi na
kusahau kuangalia upande wa pili wa kilichotokea kama ni kweli gharama
ya CHADEMA kufanya maandamano/Mikutano ni Polisi kuua raia wasiokuwa
na hatia! Ni vema basi mtoa hoja angesema Polisi wangeua walioitisha
ama maandamano au Mikutano!

Sijaona kosa la CHADEMA, na wala sitaunga mkono hoja ya mtu huyu
anayeonekana ni kichaa wa DAY maana wenzake wako BOARDING  pale
Milembe Dodoma. Tulikuwa shule na tulifanikiwa kwasababu shuleni mambo
yote yalitendeka kwa kufuata RATIBA ambayo CHADEMA wanaonekana
kuifuata katika kutekeleza mambo yao. Sikuona mantiki ya kuongeza siku
za sensa hata baada ya muda uliongezwa kumalizika!

Watanzania tukoje? Kila jambo likipangwa kutekelezeka ndani ya muda
fulani lazima muda baadae uongezwe! Ni nini hiyo? Kumbuka muda wa
kusajili simu zetu, uliongezwa! Ku-update taarifa zetu za bank, muda
uliongezwa! Vitambulisho, muda uliongezwa! n.k. Tatizo letu ni nini?
Sasa CHADEMA wanataka kumaliza mambo yao ndani ya muda uliopangwa
wanazodolewa kiasi hicho na mtoa hoja! Si ujinga huo?

Haya, mtoa hoja hatuambii nini faida kwa polisi na kwa taifa hili kwa
kuua raia wasio na hatia? Waliua Igunga, wakaua Arusha, Morogoro,
Nyololo, n.k. Kwa mauajia hayo, Tanzania tunanufaikaje?

Wameajiri watu ili wawe Polisi, lakini wanawatumia kama vyombo! Halafu
tuilaumu CHADEMA! Kwa mtu mwenye akili timammu na mwenye mapenzi mema
na nchi hii kamwe hawezi kushabikia upuuzi unaofanyika Tanzania na
viongozi wetu wanaotumia chombo cha Polisi dhidi ya wenye nchi!

Mungu atusaidie!

On 9/17/12, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
> NA RICHARD TAMBWE HIZZA
>
> WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini
> waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha
> Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa
> mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana
> kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.
>
> Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika
> kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la
> polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa
> yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na
> kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa
> vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya
> majimbo 239).
>
> Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana
> na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi
> waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa
> habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa
> kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote
> hatukuyategemea.
>
> Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na
> msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki
> baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania
> ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo.
> Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania
> wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa
> na nini/nani?
>
> Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri
> sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea
> na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la
> polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia
> wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo
> walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je,
> uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?
>
> Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la
> kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa,
> najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano
> na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo
> inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi
> kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).
>
> Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima
> wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha
> kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi?
> Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa
> mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria
> dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo
> Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa
> ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na
> mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua
> ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.
>
> Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya
> nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo
> kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu
> ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria
> viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata
> upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria
> inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.
>
> Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha
> mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je,
> ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza
> sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha
> kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu
> Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka
> katika taasisi zetu za habari?
>
> Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko
> lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini
> wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na
> kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani
> tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao
> wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na
> vyombo vyake?
>
> Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea
> kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko
> ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida
> sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa
> katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama
> zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.
>
> Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji
> ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika
> shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira
> hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment