Monday 17 September 2012

Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Bwana Richard,maswali yako uliyojiuliza ni mazuri,lakini naomba nikuulize kwa nini pia hukujiuliza maswali haya kama kweli wewe ni mzalendo na unaitakia mema nchi hii..

1.Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri
sensa ipite? 
Swali langu,ni je kulikuwa na uhalali gani wa polisi kukizuia CHADEMA wasifanye kile walichotakiwa kufanya na wakati mikutano mingine kama hiyohiyo iliendelea kufanywa na vyama vingine kama CCM na huku sensa ikiendelea?Je,ni kwa namna gani mkutano wa CHADEMA wa kufungua tu tawi ungeathiri uchukuaji wa sensa ambayo ilikuwa ni maalumu tu kwa wale ambao hawakuhesabiwa?

2. Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea
na yanayotokea mara kwa mara nchini? Katika swali hili ningeomba ujiulize,kwanza je ni kweli CHADEMA ni wakaidi? na ni maafa mangapi yameikuta nchi yetu?.Je,polisi wanafanya kazi bila kuingiliwa na maslahi ya watawala
Bwana Hiza,
Mwanahalisi ameandika ukweli wa tukio lote la kutekwa Dr Ulimboka,cha maana ilichokiona serikali ni kulifungia gazeti hilo.Tukio la kutekwa Dr Ulimboka,cha maana jeshi la polisi ilichokiona ni kumshitaki mtu ambaye kwa dhahiri hakuhusika na ni punguani wa akili.Watanzania wameamua kuvumilia tu ili siku ziende... Mabomu ya Mbagala ni moja ya maafa makubwa sana nchini petu,lakini mpaka sasa watanzania hatujaelezwa chochote. Zanzibar,mali na makanisa yamechomwa moto na vurugu zinaendelezwa na kundi la uamsho linalofanana kwa dhahiri na la kundi hatari la Mungiki....serikali yako haijasema chochote, ilichofanya ni kuwaita hao ni wahuni tu.Ni muhuni gani anayejua kutofautisha kanisa na msikiti? Haya tena,na jengo la CCM na mali zimeharibiwa na kundi hilohilo....najua cha maana kitachofanyika na serikali ni kuwaita wahuni tu.Viongozi wa kiislamu wamehamasisha kwa dhahiri na hata CD zipo za mahamasisho hayo kuwa watu wagomee sensa,cha maana jeshi la polisi ilichokifanya ni kukamata wadanganyika na amri ilipotolewa na wadanganyaji,hata hao wadanganyika waliachiwa huru bila mashtaka.



3. Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia
wasiifanye? Hili naomba ni kujibie,isingekuwa sawa kwani taarifa za kiitelijensia kutoka serikalini zilionyesha kuwa hiyo ingehatarisha mustakabali wa nchi.


4. Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo
walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je,
uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?
 Katika hili swali langu,je ni halali polisi walipowaachia wagomea sensa kwa amri ya waislam?na je,kwa kufanya hivyo uhalali wa jesho la polisi kuwepo umeondolewa?

Bwana Hiza,kwa kukurahisishia kazi ni kuwa,mtazamo wa serikali yako ni huu CHADEMA ni chama cha kikristo,na ni hatari sana katika awamu yetu hii ya kufaidi. Serikali itafanya lolote iwezalo kupambana nacho hata kama hakuna sababu.....

Regards,Godfrey Ngupula



From: "tikooza@yahoo.com" <tikooza@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, 17 September 2012, 12:17
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA


Hivi nchi hii bado ina mbumbu wa kudanganyika kirahisi!!

Tuache masihala na maisha ya watu.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

-----Original Message-----
From: nevilletz@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 17 Sep 2012 09:11:47
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Tambweee,
Juhudi zako nimeziona, hongera sana kwa kujitahidi kuukwepa ukweli. Hapa suala muhimu ni kwamba polisi walimuua Mwangosi, wauaji hawakubaliki kwa sababu zozote zile.

Iwe polisi walitoa kibali au hawakutoa, iwe CCM kinaogopa kunyang'anywa dola na Chadema au vinginevyo, sisi hilo hatujui. Tunajua neno moja kwamba polisi ni wauaji na walidhamiria katika kile walichofanya.

Kwa maana hiyo damu ya Mwangosi na wengine waliowauwa kwa kisingizio cha kutuliza vurugu, itaendelea kuwalilia. Ili kuondokana na lawama hizi, wafanye kazi ya polisi ambayo kimsingi siyo kuua bali kulinda usalama wa watu.

Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

-----Original Message-----
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 17 Sep 2012 01:49:53
To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

NA RICHARD TAMBWE HIZZA

WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini
waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha
Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa
mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana
kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika
kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la
polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa
yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na
kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa
vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya
majimbo 239).

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana
na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi
waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa
habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa
kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote
hatukuyategemea.

Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na
msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki
baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania
ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo.
Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania
wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa
na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri
sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea
na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la
polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia
wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo
walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je,
uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la
kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa,
najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano
na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo
inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi
kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).

Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima
wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha
kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi?
Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa
mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria
dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo
Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa
ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na
mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua
ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya
nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo
kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu
ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria
viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata
upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria
inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.

Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha
mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je,
ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza
sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha
kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu
Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka
katika taasisi zetu za habari?

Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko
lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini
wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na
kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani
tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao
wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na
vyombo vyake?

Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea
kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko
ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida
sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa
katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama
zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.

Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji
ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika
shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira
hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment