Monday 17 September 2012

RE: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Labda nimuulize Mgosi Tambwe,hivi ni mikutano ya Chedema tu ndiyo ilikuwa kizuizi cha shughuli za sensa kufanyika,Tamasha la Fiesta na Ufunguzi wa Kampeni za Bububu hivikua vizuizi?.Ebu tuwe wakweli maana Tanzania ni yetu sote bila kujali itikadi ya vyama vyetu,unapoamua kuwa mnafiki,tutaiharibu tanzania yetu.Wahenga wanasema,ukiwa mnafiki ujanani,uzeeni utakuwa mchawi

-----Original Message-----
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Sent: Monday, September 17, 2012 11:49 AM
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

NA RICHARD TAMBWE HIZZA

WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini
waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha
Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa
mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana
kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika
kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la
polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa
yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na
kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa
vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya
majimbo 239).

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana
na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi
waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa
habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa
kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote
hatukuyategemea.

Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na
msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki
baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania
ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo.
Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania
wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa
na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri
sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea
na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la
polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia
wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo
walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je,
uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Wananchi wote tunapaswa kuhes


[The entire original message is not included]

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment