Monday 24 September 2012

Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Tony, mimi mtakumbuka hapa niliwahi kusema kisiasa kwamba kuna utata...kuna utata lakini sikuujua utata huo uko wapi, maana am a lay man kwenye sheria, sasa huyu kauonesha wazi utata huo, na nilivyoona wala si wa kupuuza, maana kuna forgery, impersonation, wrong declaration of identity etc...na haya ni makosa ya jinai!

Raia mwema katoa taarifa, sasa dola ichukue tu hatua za kisheria!

Mi nashauri afuate taratibu za kisheria badala ya kufanya hili ni jambo la kisiasa...pia apunguze uadui na watu, maana anawafanyia uadui mpaka ambao hawamo, km vile mimi anavyonilazimisha nionekane hasimu wake kwenye siasa wakati siko hivyo na wala siko tayari kuwa hivyo!

HK!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 25 Sep 2012 06:15:32 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Deo,

Mtafasiri halali wa sheria ni mahakama na sio mtu wa Uhamiaji na hivyo unaweza kuwa sahihi au yeye akawa sahihi mbele ya watafasiri halali wa kikatiba! Pia wote mnaweza kuwa sahihi na hivyo mahakama ikachukua msingi asili wa maamuzi!

Ushauri wa HK. Kwa HB unabakia palepale, apunguze maadui na ahalalishe uraia kama kuna dosari yeyote.
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: "Deodatus Balile" <deobalile@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 25 Sep 2012 06:05:05 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Tony/Kigwa,

Wala hapa mimi sizungumzi siasa zenu, nazungumza uhalisia. Msipinge hoja yangu kwa hisia bali kwa hoja. Ninavyoandika hapa ninazomkononi sheria zote mbili na kwa waliokuwa Morogoro wiki iliyopita katika semina ya Uhamiaji wanajua nikisemacho.

Tusipotoshe sheria kwa masilahi ya matumbo yetu, basi. Sisemi zaidi ya hapo. Huyu aliyeandika si yupo? Ajibu hoja yangu kisheria na si kisiasa, basi.

Huyu mtu kasema anapatikana kwa DSO Nzega, hakuna makuli pale tunaifahamu kazi ya watumishi wa ofisi hiyo, basi.

Balile
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: hkigwangalla@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 25 Sep 2012 05:45:02 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Dis, usichokijua ni kwamba Hussein ana maadui wengi sana nje ya Nzega na ni wenye nguvu na ushawishi mkubwa kuliko watu wote wa Nzega ambao ungeweza kusema ni maadui zake...mimi kila siku husema in life, let alone politics, call no man a foe!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Dismas Anthony <anthonydismas1@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 25 Sep 2012 07:59:13 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Mimi siamini kama huyu aliyeandika ni usalama wala mtu wa uhamiaji bali ni mwanasiasa mwenzake tena yaweza kuwa Mpinzani wake huko Nzega. Hii ni vita ya kisiasa tu.Tuendelee tutasikia mengi sana.
Mimi ninaamini huwezi kuwa msafi eti kwa kumchafua mwingine. Timiza wajibu wako kama kiongozi na wananchi wanajua. Hivi kweli haya mambo kama ni kweli watajua kupitia barua hii? Mbona sasa hawamshtaki? lengo ni moja kisiasa tu, chaguzi zikipita kwishney. 

2012/9/25 Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Balile,

Kwa maelezo ya huyo jamaa ni lazima kafanya utafiti na ulizotoa kama sifa za uraia naona unampa moyo tu! Sheria iliyotumika kwenye hoja hii ni sahihi, ukubali wala usikubali kwa mahusiano yako na Bashe, bado hoja inabaki! Apunguze maadui itasaidia sana kama ushauri uliotolewa hapa!

Kuna siku maadui zake watamnasa na kumrudisha hadi mpaka wa Somalia na ndipo ataona wimbo na chorus yake. Siri ni kupunguza ambitions za kisiasa na kubaki kama mfanya biashara mzuri tu! Kwenye siasa inamjengea uadui.

Huyu aliandika hapa sio afisa wa usalama bali naona ni mtu wa uhamiaji na ana taarifa za Ndg Bashe zote ila kuna shinikizo linalozuia asichukuliwe hatua za kisheria. Tafsiri ya sheria sio rahisi ulivyoieleza kwenye hoja yako ya awali!

Pole zake sana!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: J L <chingaone@gmail.com>
Date: Tue, 25 Sep 2012 01:31:49 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Balile!
Kwa hali hii inatisha, kama serikali itaendelea kutoa ajira nyeti kwa watu wenye tabia  hizi sijui tutakuwa na taifa gani siku zijazo? watu wanaona sifa kusimama mbele za watu na kusema nafanya kazi usalama wa Taifa  ili hali hata hajui kutunza unyeti kama   kazi yake inavyotaka, inasikitisha na kuondoka kabisa maana na uhalisia wa kazi yenyewe, inatisha

2012/9/24 Deodatus Balile <deobalile@yahoo.com>
Ndugu zangu Watanzania salaam.

Nimeisoma taarifa hii na nimepata masikitiko makubwa kwa sababu zifuatazo;-

1. Mwandishi wa barua hii inaonekana ana uelewa wa masuala ya kisheria kwa maana kuwa amesomea sheria

2. Mwandishi wa barua hii inaonyesha ni mtumishi wa idara nyeti yaani Usalama wa Taifa na ndiyo maana ameweza kupata vielelezo vyote alivyoambatanisha

3. Mwandishi wa barua hii kwa makusudi au kwa dharau kuwa Watanzania walio wengi akidhani sote ni mbumbumbu wa sheria ameamua kuipotosha jamii na uongozi kwa kuchezea mantiki ya sheria husika na kujaza uongo wenye kufanikisha malengo yake juu ya Bashe.

4. Bila kujua amejikuta akisema ukweli juu ya taratibu alizopaswa kufuata Bashe katika kupata uraia alipotumia neno KUTHIBITISHA uraia wake.

5. Kumbe kama taarifa zinazoendesha nchi yetu ni majungu ya aina hii ndiyo maana milele hatutatoka kwenye umasikini. Ni hatari kuendesha nchi kwa umbea.

6. Ikiwa Hussein alifanya kosa la kubadili siku ya kuzaliwa, nakubaliana na mwandishi wa barua hii kuwa hilo ni kosa kisheria, lakini ni jinai ambayo adhabu yake haihusiani na uraia.

Baada ya maelezo hayo niseme kuwa mimi nimeamua kusomea sheria baada ya kushuhudia upotoshaji wa kutisha kwa nyakati mbalimbali kwa muda wa miaka karibu 20 niliyofanya uandishi wa Habari.

URAIA wa mtu unatolewa kwa vigezo viwili tu. HAKI YA UBINI yaani DAMU ya mmoja wa wazazi wako na ya pili ni HAKI YA UDONGO kwa maana ya ARIDHI (nchi) ulikozaliwa.

Ndiyo maana Tanzania kwa sheria hiyo hiyo aliyoitaja huyu mpotoshaji kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 inaruhusu URAIA wa nchi mbili hadi umri wa miaka 18.

Kwa hiyo Bahe kwa kuzaliwa Nzega ana haki ya UDONGO. Mkondo wa kumpatia uraia mtu wa aina hii kisheria ni Kuthibitisha uraia kwa kukana uraia wa wazazi wake ikiwa wote si Watanzania na mhusika amezaliwa nchini.

Ikiwa mmoja wa wazazi wako ni Mtanzania, moja kwa moja unakuwa Mtanzania isipoluwa ukifikisha miaka 18 unapaswa KUTHIBITISHA uraia wako na si KUOMBA. Hili ndilo amefanya Bashe.

Wale wa miaka 10 na 7 mfululizo nchini ni wale wasio na kimoja kati ya nilivyovitaja HAKI YA UDONGO au HAKI YA DAMU. Ni wale waliozaliwa nje ya Tanzania na wazazi wao si Watanzania hivyo haki hizi zipo huko walikozaliwa ila wanataka kuwa Watanzania ndipo inawapaswa kutimiza masharti ya miaka 10 wakija nchini mwetu.

Najiuliza mtu aliyesomea sheria na kupewa dhamana katika Idara nyeti ya Usalama wa Taifa kwa nini apotoshe viongozi na jamii kiasi hiki?

Je, mtu huyu aliyesema anapatikana kwa DSO ni mara yake ya kwanza kupotosha kama alivyofanya hili la Bashe?

Kama ana ujasiri ajitokeze kwa jina lake mimi na yeye tuanze kuweka vifungu vya sheria husika kisha tuone nani ataibuka mshindi katika mjadala huu.

Hii ni aibu kwa taifa letu kuwa na watumishi wanaofikiria kwa kutumia MATUMBO.

Upotoshaji huu, hapana. Mungu ibariki Tanzania tuondokane na wapotoshaji hawa.

Balile
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

Date: Mon, 24 Sep 2012 10:58:38 +0000
Subject: Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Duh!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
Date: Mon, 24 Sep 2012 13:07:32 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Mambo ya aibu kabisa! Vita ya kisiasa inakuwa kama personal. Watu wako obsessed na character assasination na hawaoni jingine la maana la kufanya kwa ajili ya nchi yao.
 
Sio juu yangu kuamua kuwa Bashe au Bashir ni raia au sio raia lakini huu utumiaji wa uraia kama silaha ya maangamizi kwa wapinzani wenu wa kisiasa ni mtego wa panya. Yeyote aushangiliae mpeni pole!!!!
2012/9/24 paul lawala <pasamila292000@gmail.com>
Vita vya makundi ndani ya CCM au?

Mbona kila uchaguzi ukija ndiyo Tunasikia habari za uraia?

Au ndiyo zile siasa zinazoitwa "maji taka"

2012/9/24 Gwaigwa Maduhu <gmaduhu@gmail.com>:
> Maganga Masanja,
> NZEGA.
> TABORA
> +255786731566 (DSO)
> 18th Sept. 2012
>
> Katibu Mkuu,
> Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu DODOMA.
>
> Mheshimiwa,
>
>
>
>
> Yah: Taarifa Kuhusu Ndugu Husein Mohamed Bashe
>
> Tafadhali husika na kichwa cha barua hii hapo juu.
>
> Mimi ni mkazi wa Nzega na ni mwanachama hai wa CCM hapa Nzega. Nimeshuhudia
> na kusikia mengi yakisemwa kuhusu wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi
> katika chama hapa Nzega nikaona ni vyema kama mwanachama na kama raia mwema
> nikatoa taarifa nilizonazo ili mzifanyie kazi wakati mkiwajadili wagombea wa
> nafasi mbalimbali na pia mkajiridhisha kuhusu taarifa hizi ili mfanye
> maamuzi yanayofaa kwenye vikao vyenu. Mimi nimefuatilia swala hili kwa
> kusoma maelezo aliyoyachapisha Huseni Bashe kwenye mitandao na pia kuongea
> na baadhi ya wazee wa hapa mjini Nzega(walioipokea familia ya shehe Mohamed
> Ibrahim na mkewe) na kubaini ukweli ufuatao, pia nimesoma sheria ya
> uraia(The Tanzania citizenship act, principal legislation, Chapter 357
> revised edition, 2002)
>
> Ndugu Husein Mohamed Bashe ama Husein Mohamed Ibrahim Bashir (tunashangaa
> kwa nini jina lake limekuwa likibadilika badilika – wengine wakidhani ni
> katika kutafuta uhalali wa kujiita Mnyamwezi kama nyaraka zake za kughushi
> Uraia zinavyoonyesha), ambaye anajulikana hapa Nzega kama mtoto wa Shehe
> Mohamed Ibrahim, alizaliwa Nzega Mnamo Tarehe 26/08/1975 (kumbukumbu rasmi
> za kuzaliwa kwake zinapatikana Ofisi ya Vizazi na Vifo, Nzega - kwenye cheti
> chake cha halali cha kuzaliwa; Shule ya Msingi Kitongo, Nzega, aliposajiliwa
> darasa la kwanza Mwaka 1984; na Chuo Kikuu Mzumbe alipodahiliwa kuanza
> masomo ya shahada ) na wazazi wake wote wawili wakiwa wasomali pure kutokea
> Somalia, na wote hawa hawakuwa Raia wakati Huseni akizaliwa. Baba yake
> Husein amepata Uraia 1987 kwa taratibu za kuomba kisheria. Mama yake Huseni
> anayejulikana kwa jina la Zainab Abdi hajawahi kuwa raia wa Tanzania na
> hajawahi kuomba na kupewa Uraia (hivyo anaishi nchini kinyume cha sheria).
>
> Kwa kuwa wazazi wote wawili wa Huseni hawakuwa raia wakati wanamzaa yeye na
> wadogo zake wote watano kwa mujibu wa sheria wote hawa si raia na wako ndani
> ya Tanzania kinyume cha sheria.
>
> Kama raia mwema nimepata taarifa kwamba kuna mtandao wa wasomali ambao
> wameingia nchini siku hizi na wametengeneza genge la kutafuta uhalali wa
> kuishi nchini hapa na kutawala nyanja mbalimbali za uchumi na jamii na hivyo
> nikahofia kwamba isije kuwa ndugu Huseni naye ni mmoja wapo uki zingatia
>
>
> amekuwa akifanya jitihada za kina na kwa kutumia nguvu kubwa sana ya pesa
> (ambazo hatujui anazipataje ukilinganisha na hali ya maisha ya familia yake
> na wazazi wake hapa Nzega) kutafuta ubunge na uongozi ndani ya chama tawala.
> Wengine hapa Nzega wamekuwa wakisema kwamba anatafuta ubunge kwa nguvu namna
> hii ili ahalalishe uraia wake wa uongo alionao na atafute namna ya kuingiza
> ndugu zake nchini Tanzania kwa kutumia nguvu ya kisiasa. Watu wengi wamepata
> mashaka hapa Nzega na kuna minong'ono kwamba anafadhiliwa na huo mtandao wa
> kiharamia wa kisomali wenye nia ya kutafuta namna ya kupenyeza watu wao
> kwenye system. Hili hasa ndiyo limenitisha na kunifanya niamue kutoa taarifa
> hii ili vyombo vya dola vilifanyie kazi na ukweli uthibitike.
>
> Mwaka 2005 aligombea Ubunge na alipewa alama ya D kwa sababu ya 'utata' wa
> Uraia wake.
>
> Mwaka 2008 aligombea uenyekiti wa UVCCM Taifa na vikao vilimjadili na
> kuonyesha utata kwenye uraia wake, na hapo alikimbia kutengeneza kiapo cha
> kugushi cha haraka haraka cha kuthibitisha uraia wake.
>
> Watu wengi, na mimi nikiwemo tulibaki na mashaka yetu kwamba ni katika
> mazingira gani mtanzania wa kuzaliwa atalazimika kula kiapo kuthibitisha
> uraia wake? Hivi ni wangapi kati yetu wamewahi kufanya hivyo? Kwangu hili
> limekuwa likinipa mashaka makubwa na kunifanya niamue kufanya ufuatiliaji wa
> kina.
>
> Mwaka 2010 aligombea ubunge na alikatwa jina na vikao vya juu vya CCM kwa
> sababu ile ile ya 'utata' kwenye uraia wake. Mwaka 2010 Waziri wa Mambo ya
> ndani Laurence Masha alithibitisha kwenye vyombo vya habari kuwa ndugu
> Huseni Bashe ni raia japokuwa hapa Nzega ambapo wanamfahamu ndugu huyu na
> chimbuko la familia yake toka wanaingia walibaki na mashaka yao. Hali hii na
> wasiwasi nilionao juu ya mtandao huu vimenifanya kuandika waraka huu ili
> kukiomba chama kitupe ukweli wa swala hili ni nini na pengine kumtaka Huseni
> Bashe, mama yake na wadogo zake wafuate taratibu za halali za kutafuta uraia
> wao.
>
> Hata hivyo pamoja na waziri wa mambo ya ndani kutoa uthibitisho huo kwenye
> vyombo vya habari hakumpa ndugu Huseni Bashe hati yoyote ile ya kumpa Uraia.
> Hivyo maneno yale yanabaki kuwa kauli ya kisiasa isiyo na mashiko yoyote
> yale kisheria kwa mujibu wa sheria hiyo niliyoitaja hapo juu.
>
> Kwa kuwa baba yake alipewa uraia tarehe 27/05/1987 baada ya kuishi kwa hati
> ya ukazi kwa muda mrefu na kuamua kuomba uraia na kufuata taratibu zote
> hakuna utata kwamba alikuwa raia wa Somalia kwa muda wote kabla ya hapo.
> Hata Huseni mwenyewe amejaza kwa kuthibitisha hili kwenye fomu yake ya
> kugombea Ubunge kuwa baba yake alizaliwa mwaka 1947 sehemu inayoitwa Buroa,
> Mkoa wa Buroa kule Somalia. Japokuwa maelezo yaliyopo kwenye mtandao
> aliyoyatoa kumshambulia mbunge wa nzega mheshimiwa dr. Kingwangallah
> anaandika hadithi tofauti kwamba baba yake alizaliwa Tabora mjini.
>
> Uraia wa mama yake unabaki kuwa ni swala lenye kuhitaji uchunguzi na
> uthibitisho. Huseni hutoa maelezo ya kwamba mama yake ni mnyamwezi wa Tabora
> jambo ambalo halikubaliki maana hata Kiswahili, achilia mbali kinyamwezi,
> hakifahamu vizuri na pia hata muonekano wake ni wa kisomali bila shaka
> yoyote. Kwa maelezo ya Husein Bashe kwenye andiko la kashfa kwa mbunge wa
> nzega dr. kingwangallah anadai kuwa wazazi wa mama yake ni wazaliwa wa
> Tanzania, Sumbawanga (Baba yake na Mama Husein) na Boma Ng'ombe (bibi yake
> na mama Husein) kwamba walichagua uraia wa Tanzania
>
>
> kutoka ule wa Somaliland wakati wa Uhuru lakini hakuna kumbukumbu hata moja
> kuwa waliandikwa kwenye rejista ya raia wa Tanzania waliosajiliwa kama
> 'aliens' kwa mujibu wa sheria iliyokuwa inatambua uraia wa kuandikishwa,
> yaani 'citizenship by registration' ya watanzania minorities wakati tukipata
> uhuru. Habari hizi zinaonekana ni za uongo kwa kuwa tayari tuna ushahidi wa
> cheti cha kugushi cha mama yake na mama Husein Bashe (aliyejulikana kwa jina
> la Amina bint Ahmed) na tuna taarifa kwamba babu yake kizaa mama na Husein
> alitokea kijiji cha Belibeli kule Somaliland akiingia Tanzania na mkewe bi
> Amina na watoto (akiwemo mama Husein – Zainab bint Abdi).
>
> Alichokifanya Huseni Bashe ili apate Uraia
>
> Kwa mujibu wa sheria ili upate uraia wa Tanzania ni lazima uwe umeishi
> nchini kwa kibali cha ukazi na umeishi kwa kipindi kisichopungua miaka 10,
> saba kati ya hiyo uwe umeishi mfululizo huku ukiwa mwema na mwenye faida kwa
> nchi kijamii ama kiuchumi (second schedule, conditions for citizenship by
> naturalization, section 9(1) ya sheria niliyoitaja hapo juu) . Na maombi
> hayo yanaanzia kwenye kata unayoishi (kanuni namba 8 iliyomo kwenye Tanzania
> citizenship regulations (section 28)) pia alitakiwa mwombaji (Huseni Bashe)
> kutangaza kwenye magazeti ya kila siku kwa siku 2 zinazofuatana (kanuni ya
> 3 ya kanuni nilizozitaja hapo juu). Mpaka naandika hapa hakuna gazeti wala
> mtu hata mmoja katika
> niowahoji aliyekumbuka kuona tangazo la namna huyo kumhusu Husein Bashe.
>
> Kwa kufuata utaratibu huu unaoelekezwa na sheria na kanuni zake alijua
> angepoteza matumaini ya kuingia kwenye siasa mapema na ingewezekana kuwa
> ndiyo ukomo wake kabisa. Aliamua kutafuta njia fupi ya kupata uhalali wa
> uraia wake kwa kugushi hati za kuzaliwa za mama yake mzazi na za bibi yake
> kizaa mama (ambazo naziambatanisha hapa). Kwa kufanya hivi alijua atapata
> uhalali wa kutumia kipengele cha sheria kinachosema kama mzazi wako mmoja ni
> mtanzania na wewe umezaliwa Tanzania basi unaukana tu uraia wa mzazi mmoja
> ambaye hakuwa mtanzania wakati unazaliwa. Hivyo alipata mwanya wa kuukana
> uraia wa baba yake na kudai amebaki na uraia wa mama yake (ambaye alidai
> kuwa ni mnyamwezi na hata kwenye hati ya Husein Bashe inaonekana hivyo).
>
> Hati ya kuzaliwa ya mama yake mzazi na Husein Bashe ninayo kivuli chake na
> nitakiambatanisha na barua hii pia cha bibi yake. Vyeti vyote hivi ni vya
> kugushi na hili tumelithibitisha RITA. Cheti cha mama yake Huseni Bashe kina
> taarifa zifuatazo:- No. of Entry 3032, Namba ya cheti A. 17404 na
> kimesainiwa na L. M. Manson tarehe 14/02/1984, kimetolewa wilayani Tabora,
> na kinadai mama yake Husein Bashe, mwenye jina la Zainab bint Abdi alizaliwa
> Government European Hospital na ni wa kabila la Isihakia kutokea Somalia. Na
> kile cha Bibi yake Husein Bashe kina No. of entry 3508, na namba ya cheti A
> 17399, na kimesainiwa na A. B. Hodgson, kimetolewa wilaya ya Moshi tarehe
> 14/02/1984, amezaliwa Boma la Ng'ombe, na jina lake ni Amina Binti Abeid, na
> ni wa kabila la Isihakia. Jambo la kuvutia ni kwamba kwenye vyeti vyote hivi
> aliyesaini ni mtu mmoja (japokuwa ni mikoa miwili tofauti na siku moja).
>
> Mbali na RITA kukana kutokuvitambua vyeti hivi kuna kila alama ya kugushi
> kwenye nyaraka hizi kwanza vyote vimesainiwa na kutolewa siku moja, na mtu
> mmoja kwenye mikoa tofauti na serial number za kufuatana (17404 na 17399!)
> pia walioandikwa kusaini wana majina tofauti yanayoonesha kuwa ni foreigners
> (Manson na Hodgson). Watu wenye majina hayo hawajawahi kuwepo Tabora wala
> Moshi. Pia hakujawahi kuwa na hospiali yenye jina hilo lililotajwa hapa
> Tabora na ni kitu kisichowezekana kwa ofisa
>
>
> wa serikali kukosea jina la Boma Ng'ombe na kuandika Boma la Ng'ombe pia
> kuandika kwamba ipo
> wilaya ya Moshi badala ya wilaya ya Hai.
>
> Uchunguzi wangu umebaini kuwa mama yake hakuzaliwa Tanzania na kwamba
> aliingia Tanzania kupitia Rundugai akiambatana na wazazi wake na wajomba wa
> Huseni Bashe (mmoja yupo Dodoma – maarufu kama Charles mnene, na ambaye
> alinipa historia hii bila kujua ninachokifanya) wakati huo mama yake mzazi
> Husein akiwa na umri wa miaka 8/9.
>
> Alitafuta njia fupi ya kujipatia uraia ili kukwepa mlolongo wa taratibu kwa
> sababu za kisiasa. Kiuhalali – alitakiwa alipofikisha umri wa miaka 18 aanze
> kuishi kwa kibali cha ukazi kwa kipindi cha miaka 10 ndipo afanye maombi
> yake rasmi ya kupatiwa Uraia jambo ambalo lingemnyima sifa ya kugombea
> uenyekiti wa UVCCM Taifa mwaka 2008, hivyo alikwepa akapita njia fupi. Sasa
> kwa kufanya hivyo amevunja sheria kwa kugushi nyaraka za uraia za mama na
> bibi yake na ana kosa la kujibu kisheria, yeye na pamoja na bibi na mama
> yake.
>
> Anachotakiwa kufanya kwa sasa kuhusiana na Uraia wake
>
> Anatakiwa kuomba kibali cha ukazi na aishi kwa kipindi cha miaka 10, 7 kati
> ya hiyo ikiwa ni ya mfululizo na akiwa ni mtu mwema na mwenye faida kwa nchi
> kijamii na kiuchumi ndipo afanye upya maombi ya uraia.
>
> Tabia ya kugushi nyaraka na taarifa mbalimbali
>
> Amekuwa akidanganya umri wake kwa kuwa na siku mbalimbali za kuzaliwa –
> ushahidi ni taarifa alizojaza kwenye fomu mbalimbali za kugombea nafasi za
> Uongozi kwenye chama, mfano mwaka 2005 alipogombea ubunge alijaza amezaliwa
> mwaka 1976, mwaka 2010 alipogombea ubunge alijaza kuwa amezaliwa mwaka 1978.
> Pia mwaka 2007 alikuwa anagombea Ujumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa alijaza
> kuwa amezaliwa mwaka 1977. Siku yake ya kuzaliwa imekuwa ikibadilika
> badilika kutokana na mahitaji ya wakati huo. Siku yake ya kuzaliwa
> ilibadilika ili apate fursa ya kugombea UVCCM mwaka
> 2008 (kwa kushusha umri wake akidhi vigezo) na tarehe hiyo inapatikana pia
> kwenye kiapo chake cha
> Uraia anachotumia (hivyo nacho ni batili) na pia kwenye kitambulisho chake
> cha mpiga kura (kama inavyoonyesha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura).
> Ukitaka kuamini kuwa amedanganya umri linganisha taarifa hizi na za mdogo
> wake aliyemuachia ziwa anayejulikana kwa jina la Ismail Mohamed, ambaye naye
> amezaliwa mwaka huo huo wa 1978. Kiapo chake cha uraia kilipatikana tarehe
> 24/09/2008 akiwa na umri wa miaka 30, umri ukiwa ni wa uongo kwa kuwa
> alikuwa amefoji vyeti vya kuzaliwa.
>
> Pia mwaka 2005 akigombea Ubumbe aliandika kuwa ana digrii mbili, ya kwanza
> ya Mzumbe nay a pili
> (MBA) ya UNISA, ambayo hakuwa nayo na mpaka leo hii hana.
>
> Pia amewahi kufukuzwa kazi sehemu mbalimbali kwa udanganyifu:- alidanganya
> NMB benki kuwa anaumwa kumbe amelala nyumbani kwa uvivu wa kwenda kazini.
> Bosi wake alipozidi kumtafuta na aliposikia kuwa kuna hatari ya kufukuzwa
> kazi aliamua kutafuta daktari wa uongo ili amfunge POP ndipo akaenda
> kuripoti huku akiwa anatembea akichechemea kwa msaada wa magongo mpaka kwa
> bosi, watu wakampa pole nyingi pale ofisini. Alipoingia na kumueleza bosi
> wake kuwa hakuja kazini kwa sababu
>
>
> alivunjika mguu bosi alimhoji kwa nini hakuchukua seek sheet na kwa nini
> hakutoa taarifa, akashindwa kujibu. Pamoja na hali aliyokuwa nayo bosi
> aliamua kumkabidhi barua ya kumfukuza kazi; Husein alilia sana na kisha
> akatupa magongo akaondoka bila kuchechemea tena kama alivyoingia. Watu
> wakashangaa na kuangua vicheko. Pia amewahi kufukuzwa kazi pale Celtel kwa
> kosa la uzembe na kutokuweka sawa hesabu zake. Amewahi kufukuzwa kazi kwa
> tuhuma za matumizi mabaya ya pesa na kampuni nyingine ya wazungu wa Afrika
> Kusini iliyokuwa inatengeneza kadi za mabenki.
>
> Haya ni baadhi ya mambo niliyoweza kukusanya dhidi ya mtu huyu ambayo
> nadhani mnahitaji kuyajua ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi. Je ni kweli
> Tanzania inahitaji kuongozwa na vijana wa namna hii?
>
> Natanguliza shukrani zangu za dhati nikitarajia mtu huyu atapata
> anachostahili. Wako mtiifu,
>
>
> Maganga Masanja (kwa sababu za kiusalama nimeficha jina halisi ila ukitaka
> kunipata kwa maswali ama kwa ushahidi fika kwa DSO Nzega na mimi
> nitajitambulisha pale)
> Mwanaccm Mwaminifu, Nzega.
>
>
>
>
> Nakala:
>
> 1. Mwenyekiti wa CCM – Kwa taarifa
> 2. Naibu Katibu Mkuu, Mh John Chiligati (Mb.) – kwa ufuatiliaji (maana
> amekuwa akikutaja kwenye hotuba zake kwamba ulimsingizia kwa chuki zako)
> 3. Mwenyekiti wa CCM (M) Tabora – kwa taarifa
> 4. Katibu wa CCM (M) Tabora – kwa ufuatiliaji na uthibitisho
> 5. Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa – kwa uchunguzi wa kina na uthibitisho
> 6. Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU – kwa uchunguzi wa kina na uthibitisho
> 7. Msajili wa vyama vya siasa – ndugu John Tendwa – kwa ufuatiliaji wa hatua
> zitakazochukuliwa na chama cha mapinduzi
> 8. DPP – kwa upelelezi na hatua za kisheria
> 9. DCI – kwa upelelezi na hatua za kisheria
> 10. Kamishna Mkuu Uhamiaji – kwa upelelezi na hatua za kisheria
> 11. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi – kwa taarifa
> 12. Uhamiaji, Nzega – kwa taarifa
> 13. Usalama wa Taifa, Nzega – kwa taarifa
> 14. Mbunge Nzega – kwa taarifa
> 15. DC Nzega – kwa taarifa
> 16. CCM Nzega – kwa taarifa
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Jennifer Livigha
 Founder &  Team Leader
0712221744, 0787221744, 0754798920

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment