Thursday 6 September 2012

Re: [wanabidii] siasa uchwara kwenye haki za walemavu..

Nashukuru kufikisha kilio hiki.
Tuanze na kuvunja kipengele cha "binadam wote ni sawa". Tukifumue na
kionyeshe ni usawa upi? Walemav wa ngoz hatuwez kushiriki 70% ya
shughuli za kila siku.
Hatuwez kushinda kwenye jua kwa muda mrefu, maana hiyo hata kilimo ni
vigumu! Vinginevyo uwe na mtaji mkubwa wa kuajiri watu. Utaupataje?
Sijui.
Hatuwez kuingia katika idara yoyote ya ulinzi, si jeshi la polisi wala
lingine lolote, hatuwez kuhimili mikiki mikiki ya mafuzo.
Hata kukaa sokoni kutwa nayo ni ngumu kutokana na hali ya hewa. Ni
vigumu kwa mlemavu wa ngozi kufanikiwa kama wengine. Inahitaji nguvu
za ziada zaidi hata ya uwezeshwaji wa wanawake n.k.
Sisemi tupewe vyeo vya bure serikalini au tupewe prority kila sehem!
Vyema serikali ikatengeneza sera za kutuinua kwa namna mbalimbali,
kama lilivyopita suala la ada. Pia elimu iwe ni lazima kwa mlemavu
yoyote! Tena iwe sheria, wapo wazazi weng vijijini hawaoni nafasi za
walemavu katika maisha ya kawaida, wanaamini hata tukiwapeleka shule
watafeli kulingana na mapungufu yaliyopo.
Alshaimaar na Baruhani nawapa hongera hapo walipofikia, ila bado
sijaona part yao kama viongoz wa ngazi fulani katika mapigano ya haki
za walemavu, kuwa icon yetu haitoshi kusema wanaweza! Suala si kuweza,
ila ni kwa kiasi gani? Waonyeshe tofauti inayohitajika.
SHUKRAN kwa kalamu yako.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment