Monday 24 September 2012

RE: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Wanabidii,
 
Nakubali kuwa wanasiasa ni binadamu na wana imani zao na pia wangependa kumtumikia Mungu na pale inapobidi kumshukuru kwa yale aliyowawezesha. Ila suala hili linahitaji tafakuri ya kina sana. Hapa Tanzania, hatuna haja ya kwenda mbali. Tumewahi kuwa na kiongozi ambaye aliheshimika sana. Huyu si mwingine bali ni marehemu Baba wa Taifa. Ninaamini kuwa marehemu Baba wa Taifa alikuwa muumini mzuri sana wa imani yake. Lakini hebu tuangalie namna ambavyo alivyoweza kujipambanua kama Rais wa nchi na kama muumini safi wa kanisa Katoliki. Huu ndio mfano mzuri wa kuigwa. Alikwenda kanisani, akasali lakini alikuwa makini sana kuhakikisha kuwa vitendo vyake na maneno yake havina hata dalili ya kuonyesha kuwa anatumia udini kwa upande mmoja ili kujinufaisha kisiasa. Sikuwahi kusikia Mwalimu anatoa mamilioni ya pesa kuchangia kanisa achilia mbali kujenga. Alishughulika na masuala ya jamii. Jamii hiyo ni Watanzania wote. Huo kwangu ndio mfano mzuri sana.
 
Leo hii kuna trend mbaya sana ya kutumia makanisa na misikiti na majumba ya dini ili kukusanya wafuasi watiifu kwako ili waweze kukusaidia, wawe ni mtaji wa kisiasa. Na baadhi ya watu wanashindwa kuwa na akili na mawazo makali ya kuweza kibaini na kugundua kilichoko nyuma ya pazia. Wao wanaangalia hapa juu juu. Lakini wale wanaoangalia masuala haya kwa makini sana, wenye akili wanajua kuwa hapa ni kutafuta wafuasi waaminifu ili kujinufaisha kisiasa. Malengo na shabaha ni wazi ya kisiasa ila kwa kutumia mkakati na ujanja ambao unaweza kughilibu watu ili washindwe kuliona lililopo nyuma ya pazia.
 
Kwa umaskini huu tulionao, unapowaahidhi watu kuwajengea kanisa, kujenga kituo cha watoto na sehemu ya biashara ya kina mama kufanya biashara, je unategemea watu hao watakunyima ufuasi wao mtiifu?! Ukishafanya hivyo, kwa maneno mengine umewa-disempowered watu. Umewafanya wakutegemee wewe. Umeua na kuzika hata ule uwezo wao mdogo wa kujiletea maendeleo yao wao wenyewe. Watakufanya wewe kama Mungu, watakuabudu, lolote utakalosema litakuwa la kweli hata kama si la kweli, watampinga yoyote yule atakasema jambo baya juu yako. Ukiwaomba kura watakuchagua kwani wafuasi wako waaminifu. Wewe unawapa vitu ambavyo wao hawana na wao wanakupa utiifu wao. Hii ndio Tanzania tunayoijenga. Tanzania ya watu ambao wanasubiri Mbunge au Waziri aje kuwajengea kanisa, shule, kisima n.k. Tunajenga Tanzania ya hand outs. Watu wanasubiri kupewa. Kama wewe ni kiongozi mzuri, kwa nini usibuni sera nzuri zitakazowawezesha wananchi wenyewe kujikomboa wenyewe? na kufanya shughuli za maendeleo wao wenyewe.
 
Lakini kubwa zaidi na la kujiliza, hivi pesa za kufanya haya yote zinatoka wapi? wanapata wapi pesa? wakati tunapokea misaada kama hii, kwa nini tunalalamika tunaposikia kuwa kuna ufisadi na mikataba ya hovyo? Ndio maana sasa kila kabila, kila dini, na kila imani ingependa miongoni mwa Mawaziri na viongozi, wawe ni watu wanaotoka miongoni mwao, ili waweze kufaidi hiyo keki ya Taifa. Waziri akiwa ametoka katika kabila lenu basi nyinyi mambo yenu si mabaya. Waziri akiwa anatoka katika imani yenu ya dini Mungu awape nini? tena mnaswali naye kanisa moja au msikiti mmoja? hiyo neema kubwa, kwani atafisadi huko na nyinyi angalau mtaambulia, japo mavumba.
 
Hii ni nchi ya 'patronatage system' . Patroni ni yule mwenye resources nyingi. Anazipata vipi hizo resources? kwa kutumia ofisi yake na wadhifa wake, halafu anatafuta wafuasi au clients ambao anawapa vitu inaweza kuwa fedha, nguo, chumvi, sukari, mahindi, mifuko ya cement n.k. Na watu hawa au wafuasi hawa waaminifu, wao wanampa uaminifu wao, wanampa kura, wanamchagua. Sikubaliani kabisa na hizi sera za kuigeuza Tanzania kama nchi ya hand outs. Ninaamini katika ideas, mikakati na sera nzuri ili kila dini, kila mwananchi aweze kutumia akili, ubunifu ili kuweza kufaidika na fursa zilizopo. Siamini katika kuwatatulia wananchi matatizo yao. Ninaamini katika kuwatia shima na ari ili wananchi wenyewe kwa kutumia vipawa vyao waweze kutatua matatizo yao wao wenyewe. Maendeleo ni ya watu na ni watu wenyewe ndio wanaoweza kujiletea maendeleo yao. Huwezi kupeleka maendeleo kwa watu.
 
Wakati tunaendelea kuitumia dini vibaya, tujue kuwa tunazidi kumong'onyoa misingi ya Taifa letu, tunamng'onyoa Tunu za taifa letu. Tusishangae huko tunakokwenda iwapo tutabaguana kwa misingi ya kidini na kikabila.
 
Uongozi ni kitu kigumu sana. Ndio maana wengine hawataki kuwa viongozi, tena wa kisiasa. Sababu kubwa ni kuwa wakati mwingine uongozi huwa unakunyang'anya hata haki zako za msingi kama binadamu, kutokana tu na kofia hiyo uliyoivaa. Inawezekana kabisa, Mwalimu alishindwa kuchangia makanisa au hata kujenga makanisa, ingawa labda alipenda kufanya hiyvyo, lakini hakuweza kufanya kwa sababu alijua kuwa yeye ni Rais wa Watanzania ambao wana dini mbalimbali na labda alijiuliza iwapo nitachangia kanisa, je nitaeleweka vipi? nitajenga taswira gani? tutafakari kwa makini.
 
Selemani
 
Date: Mon, 24 Sep 2012 00:15:06 -0700
Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela
From: pasamila292000@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Sio ibada peke yake
 
Ni ibada pamoja na kufaidika kisiasa
 
Kwa hali ya siasa na kijamii iliyopo ni vigumu kutenganisha dini na siasa
 
Kutenganisha hivi vitu ni lazima siasa ifanye vizuri peke yake na dini zifanye vizuri peke
 
Sasa hivi kuna muungano usiokuwa na mpaka kwa sababu upande wa siasa na jamii upo hoi hali ambayo inalazimisha kufanya dini kama jukwaa la kujihuisha

2012/9/23 <nevilletz@gmail.com>
Yes Dennis,
Hilo ndo suala la kujadili maana pale kwenye eneo la Ibada, hapakuwa mahali mwafaka pa kauli yake!

Pale alipaswa kuzungumzia afya yake na jinsi Mungu alivyomponya.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
Date: Mon, 24 Sep 2012 09:32:49 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Kumshukuru mungu ni kitu kizuri, vipi kuhusu kutumia siku hiyo kutoa matamko ya kisiasa? Hivi pale alipokuwa anasema polisi wa dar wawataje wanaoiba mafuta bandarini haikuwa ni kwenye hiyo hiyo sherehe? Kama nimeona vibaya au kusikia vibaya nisamehewe bure!!!!!

2012/9/24 <nevilletz@gmail.com>
Katika historia ya madhehebu ya Kiprotestant, (sina uhakika na Roman Catholic), utoaji wa shukrani mbele ya Mungu ni jambo la hiari ambalo muumini yeyote anaweza kufanya baada ya kuponywa au kuepushwa na hatari yoyote ile.

Wengine huomba kusindikizwa (kuungwa mkono) na ndugu zake, marafiki na katika hali hii sadaka ya shukrani inaweza kuwa tukio kubwa linaloambatana na sherehe.

Kwa mtu kama Dk Mwakyembe, akiwa muumini wa kanisa la Moravian, kwake kutoa shukrani baada ya kuugua muda mrefu na baadaye kuteuliwa kuwa Waziri ni jambo lililotarajiwa!

Kwa maana hiyo, tunaweza kuwa na maoni na mitizamo tofauti kuhusu sadaka ya Mwakyembe, lakini kwetu sisi tunaoabudu katika madhehebu kama Lutheran, Anglican, Menonite, AICT, Presibiterian nk ni jambo la kawaida. Sio jambo geni wala la kustaajabisha hata kidogo!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
Date: Sun, 23 Sep 2012 21:32:54 -0700 (PDT)
Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Eh!! Mimi nilidhani ni uhuru wa mawazo? Nimesema ya kwangu, sikusema mtu afuate; nawe umetoa ya kwako, of course sitayafuata!! Ndo demokrasis hiyo!! LKK
 
From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
To: Wanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, September 23, 2012 9:16 PM
Subject: RE: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

LKK unatoa hoja ya ajabu kweli. Kwa sababu wewe umeacha kutoa michango Kanisani kwa hiyo unataka na wengine waache? Wewe umekuwa lini kipimo cha tabia ya wengine tangu lini? Tuwaache wanasiasa wana dini zao na hobbies zao.
Mbona wanachangia Simba na Yanga? Mbona wanachangia harusi? Kama fedha wanazotoa kama michango ni halali, nini kitanatuuma? Au Katiba na Sheria zetu zinakataza viongozi wa Serikali wasishiriki shughuli za dini zao? Tuwabane wasichote fedha za serikali kwa shughuli yoyote ya binafsi kwanza. Lakini, hatuwezi kuwazuia kushiriki katika shughuli za binafsi wanazozipenda; ni haki yao!

Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela
To: wanabidii@googlegroups.com
From: tony_uk45@yahoo.co.uk
Date: Sun, 23 Sep 2012 16:59:25 +0000

Nico,

Watu hawakumbuki historia ya utawala kuwa wafalme wote wa enzi za kiimla, fascist, imperials n.k walikubalika kwanza kwenye himaya za kidini (the holly-sea etc..). Bila hivyo hupati ufalme!

Baada ya frustrations za kila aina waumini kwenye dunia ya umaskini hukimbilia dini, kwa bahati mbaya ni dini za kuletwa na sio asili, kama mkombozi wao. Dunia ya ulaya, marekani, zenye utajiri na maisha bora waumini wanazidi kupungua!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com>
Date: Sun, 23 Sep 2012 17:51:06 +0100 (BST)
Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Kwani kuna ajabu gani kufanya hivyo? Mbona tangu zamani siasa zinafanywa tu kwenye sehemu za ibada? Au baada ya mwamini kushinda na kuitwa na viongozi wa dini hata kupewa nasaha na wengine hata kujenga nyumba za ibada tangu awamu ya pili na kuna nyumba za ibada zinaitwa kwa majina ya utani ya viongozi? Tuache unafiki. Hivyo vitu vinafanyika ingawa siyo sahihi. Wengine hata kutumia nafasi zao kutaka kuingiza nchi kwenye jumuiza za kidini. So what do you want to say? People especially politicians come to positions loaded with their religious missions and prejudices. But this is dangerous though, but who will speak? Fear of being kolimbaed! Mara ngapi hotuba za serikali zimetolewa kwenye sherehe za dini wakati tunaimba kutenganisha siasa na dini? Mara ngapi sherehe za dini zimekuwa na wageni rasmi wanasiasa pamoja na kuzindua mikanda ya dini au kufanya harambe za nyumba za ibada? Mpaka wa siasa na dini ni nini? These are imaginary boundary eti state and religion are independent units! Is a lie! Wanigeria husema hivyo. Kisiasa ndio. Ila Ijumaa wanasiasa huenda kuswali na Jumapili wanasiasa huenda kusali. Na wakiwa ibadani ni washiriki na hutii hiyo mamlaka. Ni kama mume na mke tu. Hata mke akiwa waziri akija nyumbani hata kama bwana na taxi driver lazima atakuwa kichwa cha nyumba.

From: Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, 23 September 2012, 17:39
Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Huko tuendako makanisa yatakuwa ya kuabudu watu kwa vile walijitolea kujenga na kufadhili makanisa. Makanisa na misikiti itakuja kuitwa majina ya wanasiasa! Kanisa la mwakyembe, kanisa la lowaasa, msikiti wa kigwangala nk.

Tuuchukie upumbavu huu unao hamishiwa kwenye nyumba za ibada.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
From: Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
Date: Sun, 23 Sep 2012 09:33:16 -0700 (PDT)
Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Ndo maana mi nilishaacha siku nyingi mambo haya ya michango! Kuna maskini wengi wa kuweza kusidiwa, si lazima kanisani. Maana unachanga asubuhi, jioni jamaa yuko kaunta na toto akifaidi sedaka yako!! LKK
 
From: Laurean Rugambwa <rugambwa@hotmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, September 23, 2012 7:28 PM
Subject: Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Matinyi,
Penda usipende kaka, huo ndo mradi na Mtaji wa kisiasa kwa sasa. Tumeona viongozi wastaafu baada ya kuona waliowaachia madaraka hawa wajali waliingia na kujikita makanisani! Makanisani ndo mahala pa kujificha na kubebwa. Ndio siasa zetu zinakoenda huko.

Ukwasi ulioko kanisani unatisha, hakuna auditor huo,hakuna bodi, hakuna mtu wa kuueleza umma fedha zile tunachanga kanisani zinatumikaje.

Hao viongozi wa dini kazi Yao kuchangisha fedha kwa anayeweza fanya hivo, fedha chafu, waumini wachafu ukichangia tu fedha wewe unapewa kiti cha Mbele, unatukuzwa. Mambo ya ajabu!

Kanisani sasa hivi ni Kama saccos, wako busy wanachangishana fedha,hawafanyi kazi ya injili, muda mwingi ni michango, sasa watakataaje wanasiasa?

From LR

On 23 Sep 2012, at 18:26, "Mobhare Matinyi" <matinyi@hotmail.com> wrote:

.... lakini sipendi tabia ya wanasiasa na viongozi wengine wa kijamii kujibanzabanza kwenye nyumba za ibada kama ninavyoichukia hii tabia iliyoibuka siku hizi ya wanasiasa kutoa salamu hii:
 
...Asalamu Aleikumu, Bwana asifiwe.
 
Tunazidi kuwa taifa la kijinga.
 
Sipendi uunganishaji wa siasa na dini; sipendi viongozi wa dini kuabudiwa. Nasema sipendi.
 
******************************
 
> Subject: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela
> To: wanabidii@googlegroups.com
> From: hkigwangalla@gmail.com
> Date: Sun, 23 Sep 2012 14:31:17 +0000
>
> Tuko hapa nduli kanisani, Ikolo, Kyela kumuunga mkono Dr. Mwakyembe wakati akimshukuru Mungu kwa kumponya. Ameamua kujenga kanisa na kituo cha chekechea na biashara za akinamama kama sadaka yake kwa Mungu. Sisi tumekuja kumsindikiza. Bravo Komredi! Walikuwpo watu wngi akiwemo S Sitta, Tizeba, Mulugo, Maige, Kilufi, Zambi, Mtutura, Mwambalaswa, Mwandosya, Ngoye, Lembeli etc bila kuwasahau Ndg. Mboka - kijana aliyemuokota Dr. Mwakyembe kwenye ajali ya Ihemi Iringa, inayosadikiwa kuwa ilelenga kuondoa uhai wake, pia Ndg Paul Makonda, Rais wa TAHLISO na ambaye anagombea Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM, Ndg. Eng Chambo
> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
>
> --
> Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
> Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
> Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

0 comments:

Post a Comment