Wednesday 26 September 2012

Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Ndugu Jesse Kwayu,ki ukweli umenipa raha.Huu ndio ukweli.Wabara hatuna haja ya kujimbeleza hata kidogo yanapokuja masuala ya muungano.Ikibidi uvunjike tu.Hatuna cha kupoteza.Na wanzibari wasipofyata mkia wakakaa kimya,wakumbuke ile methali 'ukimuamsha aliyelala utalala mwenyewe'. Regards,Ngupula Godfrey.


------------------------------
On Wed, Sep 26, 2012 4:24 PM EEST denis Matanda wrote:

>Kwayu,
>
>Hongera sana kwa kumwaga hizo nyanga humu....................Niwaombe na
>wengine wenye moyo wa kutopenda kufunguka kwenye mambo ka' haya wafunguke
>watu tuelimike!!!!!
>
>2012/9/26 Jesse Kwayu <jesse.kwayu@guardian.co.tz>
>
>> Matinyi umenena, ****
>>
>> Kwamba tatizo siyo mkataba Muungano uko wapi, ila kuna kitu nyuma ya pazia!
>> ****
>>
>> Nimekuwa na kawaida ya kujizuia kusema mambo juu ya Muungano hasa
>> ninapoona kauli za kuubeza.****
>>
>> Kwa kawaida, watu hupenda kitu kama kina faida kwao. Hupenda kitu ambacho
>> walau wana cha kunufaika nacho.****
>>
>> Ninapozungumza haya ninamaanisha kwamba kama kina Jabir na wengine hawajui
>> basi leo wajue, iliyokuwa inaitwa Tanganyika haijanufaika na Muungano kama
>> ilivyo kwa Zanzibar, huu ni ukweli mchungu.****
>>
>> **1. **Zanzibar hakuna ardhi yoyote ya maana ya kuwekeza,
>> Wazanzibari wametapakaa kila kona ya iliyokuwa inaitwa Tanganyika wakiwa
>> wamewekeza; ni haki yao!****
>>
>> **2. **Zanzibar haina rasilimali yoyote ya maana, lakini
>> wananufaika na rasilimali zote za iliyokuwa inaitwa Tanganyika; ni haki yao!
>> ****
>>
>> **3. **Zanzibar walianza kelele nyingi baada ya ile iliyokuwa
>> ikiitwa Zanzibar route kufungwa. Hii ilikuwa ikitumiwa na baadhi ya
>> wafanyabiashara wajanja kwamba wanaagiza bidhaa kwa ajili ya Zanzibar
>> ambako ushuru wa forodha ulikuwa chini, lakini soko lao lilikuwa iliyokuwa
>> ikiitwa Tanganyika; ilipodhibitiwa kwamba kama bidhaa hizo zinakwenda
>> Tanganyika ni lazima tu zilipiwe ushuru sawa na wengine wanaoingiza bidhaa
>> kwa ajili ya soko hilo; kwao hilo likachukuliwa kama ni uonevu kwa kuwa tu
>> wameambiwa biashara ni lazima uwe uwanja sawa;****
>>
>> **4. **Fikiria nafasi za uongozi katika nchi; Zanzibar wana nafasi
>> nyingi zaidi kuliko ilivyo kwa iliyokuwa inaitwa Tanganyika; wakazi
>> wasiofikia milioni na nusu wa Zanzibar wana uwakilishi wa kupindukia ndani
>> ya Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, wana mawaziri, wana mabalozi,
>> wakurugenzi na maofisa wengine wakubwa ndani ya serikali na mashirika ya
>> umma ambao hawafanani na uwiano wa idadi ya wakazi wa pande hizi mbili za
>> Tanzania; kwa waliokuwa Tanganyika haijawahi kuwa tatizo kwa hali hiyo na
>> wanaikubali; wana Bunge lao (Baraza la Wawakilishi), wana serikali yao na
>> mawaziri kedekede; ruksa na haki kwao!****
>>
>> **5. **Tanganyika ni basket food ya Zanzibar, kila kitu; nasisitiza
>> kila kitu, kuanzia nyanya (nyonyo), vitunguu, mchele, nyama, kila aina ya
>> mbogamboga, kutaja kwa uchache tu; hivi vyote vinapatikana kama vile
>> vinatoka mkoa mmoja kwenda mwingine; haki yao!****
>>
>> **6. **Tanganyika ni uwanja wa kujidai wa Wazanizbari, wamewekeza
>> kweli kweli, hawabaguliwi na hakuna uwezekano wa kubaguliwa kwa sababu humu
>> Tanganyika wanaonekana kama tone la maji ndani ya bahari kuu; haki yao!***
>> *
>>
>> **7. **Hizi ni baadhi tu ya faida, lakini Wazanzibari wanaoeneza
>> hoja za kuubeza Muungano hawataki kuzitaja kwa kuwa watasutwa; lakini
>> niseme hapa pia kwamba nini msukumo huu wa kuamini kuwa Muungano ni tatizo?
>> Wanaamini kwamba bila Muungano watapata marafiki wengi huko duniani,
>> watapata misaada mingi huko duniani, watapata vya bure na kusaidiwa ili
>> kuleta maendeleo; ni kelele zilezile za kutaka mteremko, siyo kitu kingine.
>> Wenye hoja hizi wanasahau kwamba katika dunia tunayoishi leo hakuna taifa
>> lolote lililoendelea kwa misaada, nasema halipo, ingekuwa hivyo ndivyo basi
>> Tanzania isingekuwa kama ilivyo leo.****
>>
>> **8. **Nilisema awali kwamba nimekuwa na tabia ya kujizuia
>> kuzungumza mambo haya, lakini nimefunguka leo kwa kuwa wapo wanaotaka
>> kuaminisha watu kwamba Tanganyika inafaidi sana Muungano, ukweli ni kinyume
>> chake;****
>>
>> Kama alivyosema Matinyi hapo juu, ni vema wanaopiga ndogo ndogo ya Mungano
>> wa mkataba wakasema wazi kuwa hawautaki Muungano ili tuanza upya na kwa
>> amani, lakini ukweli utabaki kuwa watakaopata hasara hapa siyo waliokuwa
>> Tanganyika, hawana cha kupoteza, wana cha kufaidi zaidi kwa kupata fedha za
>> kigeni kwa kila kinachoelekea kisiwa cha Zanzibar, wana cha kufaidi kwa
>> sababu suala la kufanya *babysitter* halitakuwako tena, ni wazi na
>> dhahiri mambo haya. Nawasilisha.****
>>
>> Jesse ****
>>
>> ** **
>>
>> ** **
>>
>> *From:* wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] *On
>> Behalf Of *Mobhare Matinyi
>> *Sent:* Tuesday, September 25, 2012 9:16 PM
>> *To:* Wanabidii googlegroups
>>
>> *Subject:* RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!****
>>
>> ** **
>>
>> Jabir,
>>
>> Niliwahi kuuona Mkataba wa Muungano pale Mtaa wa Lugoda - tulikuwa mimi,
>> Makunga na Jesse. Ile nakala ilipotolea wapi sijui. Lakini pia nimewahi
>> kuambiwa kuwa kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano kuna nakala za
>> Muungano ingawa sijawahi kwenda kuulizia kwa sababu hili suala
>> halinisumbui. Ninachokitaka ni taifa langu la TANZANIA na siyo makaratasi.
>>
>> Aidha, ukisoma makala za kitaaluma za wanazuoni waliouchimbua muungano
>> utabaini kwamba wanasema kuwa baada ya Nyerere na Karume kuusaini mkataba
>> huo, Nyerere aliupeleka muswada wa sheria ya muungano kwenye Bunge la
>> Tanganyika ili mkataba huo uwe sheria lakini Karume kwa kuwa hakuwa na
>> bunge yeye alitakiwa aupeleke kwenye Baraza la Mapinduzi na hakuna uhakika
>> iwapo alifanya hivyo. Hivyo, makosa ya wapi ulipelekwa au uko wapi leo
>> yasilete suala jipya kwamba eti hakukuwa na muuungano wa mkataba. Hamuwezi
>> kuungana bila mkataba hata kama mkataba huo ni wa maneno. Nadhani
>> unafahamu aina za mikataba na kimsingi hata katiba inaweza isionekane kama
>> ilivyo ya Uingereza. Sisemi kwamba huu wa kwetu hauonekani au iwe hivi na
>> vile, bali ninachosema ni kwamba tusiwadanganye watu kwamba eti huu si
>> muungano wa mkataba kwa kuwa ili wawili ama zaidi muungane ni lazima
>> mkubaliane na makubaliano yenu ndiyo mkataba kisheria.
>>
>> Kuhusu hicho mnachosema kwamba muungano wa kikatiba - ni usanii wa lugha
>> ambao unaweza kufanikiwa kwa watu wachache tu, labda wenye nia ya kupokea
>> lolote masikioni mwao ili kukidhi haja zao za kisiasa. Katiba ni nini?
>> Katiba si chombo cha kuunganisha mataifa mawili bali ni zao la watu wa
>> mataifa mawili au moja au zaidi kukaa pamoja na kuamua kwamba huu ndio
>> uelekeo na uelekezi wetu kama taifa. Ndiyo maana hatutengeneza Katiba ya
>> Muungano hadi baada ya miaka kadhaa kupita huku ile ya Tanganyika ikitumika
>> kwa muda kuziba pengo kutokana a kuundo ule wa serikali mbili. Huwezi
>> kuutumia mkataba badala ya katiba wala katiba badala ya mkataba; ni vitu
>> viwili tofauti na wala hatuwezi kusema kimoja ni bora kuliko kingine.
>>
>> Kwenye jukwaa moja niliwaambia kwamba watu waache kudanganyana na akaibuka
>> muungwana mmoja pale niliposema hakuna kitu kama "muungano wa mkataba"
>> duniani (kwa maana ya akina Seif) na yeye akatolea mfano wa Muungano wa
>> Ulaya (EU). Alikuwa amechoka kufikiri tu. Kama Zanzibar inataka muungano wa
>> mkataba na inaulinganisha na ule wa EU, sasa mbona tayari upo wa kwetu
>> Addis Ababa uitwao Muungano wa Afrika (AU)? Sasa huo wanaousema akina Seif
>> utakuwa kati ya nchi zipi wakati yakitekelezwa ya kwao Tanzania itavunjika
>> na kuzaliwa vinchi viwili vya kibabaishaji? Je, haitakuwa muingiliano wa
>> mambo? Hawajalifikiri hili. Unawezaje kuwa na huo muungano wa mkataba wa
>> vinchi hivi ndani ya AU yenye muungano wa mkataba tayari?
>>
>> Hii ya muungano wa kikatiba na wa kimkataba ni lugha za akina Maalim Seif
>> wanaotaka muungano huu uvunjike. Wanatumia lugha za kujikosha tu lakini
>> shida yao kubwa wauvunje muungano (kwa maslahi binafsi zaidi na ubaguzi)
>> lakini kwa kuwa wanajua kuwa Zanzibar bado itahitaji kuitegemea Bara, basi
>> wanajipendekeza na wazo la muungano wa mkataba. Nani alisema kuna muungano
>> usiokuwa na mkataba? Nchi iliyoungana inawezaje kukaa bila katiba?
>>
>> Ndiyo maana nasema, tuache kudanganyana; tuwe wakweli kwamba Wazanzibari
>> wengi wamedanganywa na pia wengi watanataka kila kilichomo ndani ya
>> muungano na kilichomo je ya muungano - ndiyo kisa

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment