Thursday 27 September 2012

Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Mobhare,
Nadhani wewe ni muamini wa dini ya Kikiristo (samahani kwa kuanza hivi); na nadhani wewe ni muumini wa "ukweli" kwa kuwa kuamini KWELI ni UHURU (vilevile, nakuomba radhi kwa hili); na pia, nadhani wewe ni muumini wa sayansi ya UTAFITI inayotokana na MAARIFA, UJUZI na MAADILI ya kisomi (weled)i; kama NDIYO, naomba upime hoja hizi juu ya MUUNGANO WA TANGANYIKA na ZANZIBAR.
 
MOJA, "muungano" huu ulizaliwa kwa SHINIKIZO lisilokuwa na shaka tangu awali (yaani, 1964) na ndio maana uliingiwa na watu WAWILI (Nyerere na Karume) na wawili hao walihakikisha kwamba HAWAPINGWI na wale waliowapinga aidha walipotezwa kisiasa na au WALIUAWA (rejea KIFO CHA ABDULLAH KASSIM HANGA na wengino wasiyetajika sana).
 
PILI, Nyerere alimfunika Karume (kwenye siasa) kwa kutumia ujanja wa kuitumia Katiba ya Tanganyika kama "katiba ya mpito" ilikuwa mbinu mahsusi katika kuiweka rehani Zanzaibar kwenye "Mwavuli wa Tanganyika" na hivi ndivyo ilivyokuwa na baadaye kuchukua sura ya Zanzibar (kama nchi) ndani ya Tanganyika (inayoitwa Tanzania).
 
TATU, katika kufanikisha mpango wa kuimeza kabisa Zanzibar ndani ya tumbo la Tanganyika (wengi wanaita Tanzania Bara) nchi iliingizwa kwenye mfumo wa "nchi ya chama kimoja" Julai, 1965 na miaka 12 baadaye TANU iliimeza ASP na kuanzisha Chama Cha Mapinduzi [CCM] ambayo kwa ujumla iliyameza "Mamlaka ya Zanzibar" kutoka "Kisiwandui" hadi Dodoma (Tanganyika) ambapo maamuzi yote ya Zanzibar yanafanywa Dodoma kwa utashi wa CCM-Tanganyika (Tanzania Bara).
 
NNE, Mwalimu Nyerere (1965 hadi 1985) alijipa "nguvu" zote za "dola" na mamlaka ya kuwaamulia Wazanzibari nini kifanyike pasipokuwa na "domo la kusema" sio demokrasia; tazama, mifano ya kumuwajibisha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi na hatimaye kuwafukuza wananchama 17 wa CCM kulikofanywa na Mwalimu Nyerere akiwafukuza akina Maalim Seif Sharif Hamad, Shaaban Mloo, Juma Duni Haji, Hamad Rashid Mohamed na wengineo.
 
TANO, kama ni kweli (kwa jinsi Mwalimu Nyerere alivyotaka nchi iendeshwe); basi, uhakika ni kwamba Mwalimu Nyerere alitumia "udikteta" kuulazimisha "muungano" huku akiwatumia baadhi ya Wazanzibara (sio Wazanzibari) waliotengenezwa katika kufanikisha mpango mahsusi (specific) juu ya kuufanya muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika kuzuia "vuguvugu" la UKOMUNISTI (sio USOSHALISTI wa Nyerere) na ukiitazama historia ya kuanzishwa kwake utaona kwamba wakati mfumo wa muungano unafanywa ulifanywa katika mazingira ya USIRI mkubwa na hata inadaiwa kwamba "wasomi" wa ki-Zanzibari kama Profesa (marehemu) Muhammad Abdul'Rahman Babu hakuwapo Zanzibar. Inasemekana (na ushahidi unaonyesha kwamba hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ziliandaliwa Tanganyika na mwanasheria (Muingereza) wa Tanganyika na mwanasheria wa Zanzibar (Mhindi) Wolfgang Dourado hakuwahi kuiona hati hiyo [!!!!] hadi ilipofanywa sheria na Bunge la Tanganyika).
 
SITA, kama wote tunakubali kwamba MUUNGANO ni watu (na si nchi, kwa vile nchi zinaundwa na watu); wananchi wa pande zote mbili hawakushirikishwa kwenye UAMUZI wa hatma ya nchi zao kwenye "muungano" kwa nini iwe nongwa leo wananchi wa pande mbili (nchi mbili) kuamua hatma yao kwa kuulizwa wanataka nini [?]. Kwa nini muungano ulaimishwe kwa "Nguvu za Dola" kama ni kweli hoja ya muungano ni kuwaunganisha watu (wa pande mbili) wanaotokana na nchi mbili zinazosemekana zilikuwa HURU [???]. Kwa nini Mwalimu Nyerere alikuwa "championi" wa kushinikiza kile alichotaka kiwe na akakifanya "kiwe" vile yeye (Mwalimu Nyerere) alivyotaka?
 
SABA, na mwisho; nadhani umefika wakati sasa waanchi wapewe haki yao kwa UHURU, USAWA na UADILIFU wa hali ya juu kama tunataka AMANI na USTAWI wa wat na wenye manufaa ya UMOJA na UHURU wa "kila mtu kuwa na maoni ya ujenzi ya jamii ya watu waliyo sawa na huru." Kama Mwalimu Nyerere na Shikh Karume waliweza kuwalazimisha wananchi takriban milioni 12 (pungufu au ziada kidogo [+ or -]) haiwezekani leo baada ya miaka takriban 49 kuwalazimisha wananchi wanaokadiriwa milioni 43 [!] kuamini kwamba sababu za muungano miongo mitano iliyopita ni sawa na sababu za muungano leo (2012!); sidhani!
 
Nionavyo mimi; ni wajibu wa kisheria na ni haki kwa wananchi wa nchi mbili kuulizwa juu ya aina ya muungano wanaoutaka! Kwa kuwa Zanzibar ni "nchi iliyojitambulisha kwenye Katiba ya Zanzibar ya 1984 [Toleo la 2010], na kwa kuwa Wazanzibari wameshaanza "kujitambua" na "kujitambulisha" na UTAIFA wao (yaani, WAZANZIBARI) kuna kila sabau ya kuwauliza Wazanzibari wanatakaje juu ya muungano wetu; na vilevile, ni HAKI kuwauliza WATANGANYIKA juu ya hatma ya nchi yao (Tanganyika). Napenda ieleweke hapa kwamba; Tanganyika ni nchi (iliyopoteza utaifa wake kwa kutengeneza muungano) hata hivyo, ndio nchi iliyopata UHURU tarehe 9 Desemba, 1961 na kuendelea hivyo hadi ilipoungana na Zanzibar na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (baada ya kubuniwa jina la TANZANIA).
 
Sidhani kama ni muafaka kudhani kwamba nchi zilizoungana haziwezi kutengana! Na si muhali kushadidia utengano kama watu wa upande mmoja wanaona "muungano" ni dnoana kwao. Kuna mifano michache ndani ya Afrika nchi zimetengana kutoka nchi moja - rejea, SUDAN MOJA (2011) = SUDAN KUSINI + SUDAN (YA WAARABU) na ETHIOPIA MOJA (1990s) = ETHIOPIA (YA ZENAWI) + ELITREA. Na hivi ndivyo historia ilivyo; tumekuwa tukishuhudia vurumai za nchi kutaka kujitenga Afrika, Ulaya, Asia na Latino Amerika...nadhani mambo haya yanahitaji AKILI, BUSARA, HEKIMA na UJUZI wa kuamua kwa UHURU na HAKI kwa watu na si matumizi ya nguvu za kijeshi au kipolisi. Kama tutalazimisha sababu za muungao kama zilivyokuwa 1964 tunaweza (narudia, tunaweza) kusababisha songombingo zitakazowavutia "wapenda vita" kuchukua nafasi ya ombwe la demokrasia ya watu na kuingiza demokrasia ya kijeshi (militarised democracy) kama iliyotumiwa na Sheikh Karume (ASP) na Mwalimu Nyerere (TANU) na baadaye CCM (chama kushika hatamu na kulifanya jeshi [JWTZ] kuwa taasisi ya chama).
 
Nawasilisha,
 
Bakari M Mohamed, BBA [PLM], CPSP [T], MSc (PSCM), Reg. PSP (AU 0005)
  1. Lecturer in Procurement and Supply Chain Management
  2. Procurement and Supply Chain Auditor
  3. Procurement and Supply Chain Specialist, Consultant, Researcher and Trainer in Procurement Contracts Management
  4. Doctor of Alternative Medicines [DAM] & Natural Healing Therapist
Department of Procurement and Logistics Management
Mzumbe University
Box 6
Tel (Office): + 255 23 2604381/3/4
Mobile      : + 255 713 593347

MZUMBE, Tanzania.

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, September 25, 2012 9:15 PM
Subject: RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Jabir,
 
Niliwahi kuuona Mkataba wa Muungano pale Mtaa wa Lugoda - tulikuwa mimi, Makunga na Jesse. Ile nakala ilipotolea wapi sijui. Lakini pia nimewahi kuambiwa kuwa kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano kuna nakala za Muungano ingawa sijawahi kwenda kuulizia kwa sababu hili suala halinisumbui. Ninachokitaka ni taifa langu la TANZANIA na siyo makaratasi.
 
Aidha, ukisoma makala za kitaaluma za wanazuoni waliouchimbua muungano utabaini kwamba wanasema kuwa baada ya Nyerere na Karume kuusaini mkataba huo, Nyerere aliupeleka muswada wa sheria ya muungano kwenye Bunge la Tanganyika ili mkataba huo uwe sheria lakini Karume kwa kuwa hakuwa na bunge yeye alitakiwa aupeleke kwenye Baraza la Mapinduzi na hakuna uhakika iwapo alifanya hivyo. Hivyo, makosa ya wapi ulipelekwa au uko wapi leo yasilete suala jipya kwamba eti hakukuwa na muuungano wa mkataba. Hamuwezi kuungana bila mkataba hata kama mkataba huo ni wa maneno. Nadhani unafahamu aina za mikataba na kimsingi hata katiba inaweza isionekane kama ilivyo ya Uingereza. Sisemi kwamba huu wa kwetu hauonekani au iwe hivi na vile, bali ninachosema ni kwamba tusiwadanganye watu kwamba eti huu si muungano wa mkataba kwa kuwa ili wawili ama zaidi muungane ni lazima mkubaliane na makubaliano yenu ndiyo mkataba kisheria.
 
Kuhusu hicho mnachosema kwamba muungano wa kikatiba - ni usanii wa lugha ambao unaweza kufanikiwa kwa watu wachache tu, labda wenye nia ya kupokea lolote masikioni mwao ili kukidhi haja zao za kisiasa. Katiba ni nini? Katiba si chombo cha kuunganisha mataifa mawili bali ni zao la watu wa mataifa mawili au moja au zaidi kukaa pamoja na kuamua kwamba huu ndio uelekeo na uelekezi wetu kama taifa. Ndiyo maana hatutengeneza Katiba ya Muungano hadi baada ya miaka kadhaa kupita huku ile ya Tanganyika ikitumika kwa muda kuziba pengo kutokana a kuundo ule wa serikali mbili. Huwezi kuutumia mkataba badala ya katiba wala katiba badala ya mkataba; ni vitu viwili tofauti na wala hatuwezi kusema kimoja ni bora kuliko kingine.
 
Kwenye jukwaa moja niliwaambia kwamba watu waache kudanganyana na akaibuka muungwana mmoja pale niliposema hakuna kitu kama "muungano wa mkataba" duniani (kwa maana ya akina Seif) na yeye akatolea mfano wa Muungano wa Ulaya (EU). Alikuwa amechoka kufikiri tu. Kama Zanzibar inataka muungano wa mkataba na inaulinganisha na ule wa EU, sasa mbona tayari upo wa kwetu Addis Ababa uitwao Muungano wa Afrika (AU)? Sasa huo wanaousema akina Seif utakuwa kati ya nchi zipi wakati yakitekelezwa ya kwao Tanzania itavunjika na kuzaliwa vinchi viwili vya kibabaishaji? Je, haitakuwa muingiliano wa mambo? Hawajalifikiri hili. Unawezaje kuwa na huo muungano wa mkataba wa vinchi hivi ndani ya AU yenye muungano wa mkataba tayari?
 
Hii ya muungano wa kikatiba na wa kimkataba ni lugha za akina Maalim Seif wanaotaka muungano huu uvunjike. Wanatumia lugha za kujikosha tu lakini shida yao kubwa wauvunje muungano (kwa maslahi binafsi zaidi na ubaguzi) lakini kwa kuwa wanajua kuwa Zanzibar bado itahitaji kuitegemea Bara, basi wanajipendekeza na wazo la muungano wa mkataba. Nani alisema kuna muungano usiokuwa na mkataba? Nchi iliyoungana inawezaje kukaa bila katiba?
 
Ndiyo maana nasema, tuache kudanganyana; tuwe wakweli kwamba Wazanzibari wengi wamedanganywa na pia wengi watanataka kila kilichomo ndani ya muungano na kilichomo je ya muungano - ndiyo kisa cha kusema vunja muungano huu lakini tunautaka huu.
 
Semeni mtakavyo kama ikibidi tu na hakuna anayewazuia lakini msidhani kwamba tutakaa kimya, na pia sisi tunaoutaka muungano tukijibu haina maana tunawakataza nyie msioutaka msiseme mpendalo.
 
Ushan'fahamu Jabir?
 
Matinyi.
 
Date: Tue, 25 Sep 2012 09:13:12 -0700
From: jabirgood@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi, M, mkataba wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ww umepata kuuona? Unajua kama huu umewahi kuulizwa hata Bungeni, achilia mbali kwenye Mahakama Kuu Zanzibar ambako Zanzibar Attorney General alisema yeye hajawahi kuuona.
 
Inabaki ukweli kwamba muungano huu ni wa kikatiba. Umetajwa na Katiba ya URT ya 1977. Na muungano wa kikatiba na wa mkataba ni vitu viwili tofauti.
 
Kweli, CUF wamekuwa na msimamo wao kuhusu Muungano. Lakini sauti ya sasa inakuja ktk wakati tofauti sana na huko nyuma. Na ujue sasa wanaotaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano Tz si CUF peke yao, hata CCM wengi wameamua kubadilika.
 
Mzee Hassan Nassor Moyo na baadhi ya mawaziri ktk SMZ ni baadhi yao.
 
Uzuri ni kwamba sasa kuusema Muungano huu si UHAINI. Kwa hivyo, usikasirike watu wakiusema, si ndio wanavyouona? Nawe ni haki yako kuuona unavyouona. Basi mawazo yote haya yaachiwe yasikike na wanaoyatoa wawe huru.
 
Hata Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba anasema jambo hili - watu wapewe uhuru kutoa maoni yao na wao wanachukua kila maoni yanayotolewa.
 
Nimalize kwa kukukumbusha kuwa suala la mjadala khs Muungano wa Tz, limeigharimu sana Zanzibar, zaidi kuliko Bara ambako baadhi yenu wengi, mnaona hauna tatizo.
 
Kwenye mjadala fulani nilipata kusema, Kama Wazanzibari wanasemwa kwa kuupinga Muungano kwa kuona haujawanufaisha, kwanini ung'ang'aniwe kwa nguvu kubwa Tanzania Bara?
 
Tunasubiri mbele ya safari itakuwaje.
 
Jabir+
 
 

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, September 24, 2012 1:15 AM
Subject: RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Hajasema kipya. Tangu zamani ndio msimamo wa CUF; labda tu tuseme kwamba sasa wamekuja na lugha mpya ya muungano wa mkataba ambao ni upuuzi tu. Hakuna kitu kama hiki duniani. Kwani huu wa sasa hauna mkataba? Je, huo wanaoutaka una tofauti gani na huu wa AU?
 
Date: Mon, 24 Sep 2012 09:29:46 +0300
Subject: Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
From: denis.matanda@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Si ndio msimamo wake ( na wa chama chake) all along au?

 
2012/9/24 John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>
Dear All,
Makamo wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Katibu Mkuu wa CUF apasuwa bomu kwa CCM na kwa Watanganyika pale alipoweka
msimamo wake na wa CUF wazi kabisa kwa kutamka jana mkutanoni Bububu kuwa..."wakati umefika kwa Wazanzibari kuendesha nchi yao wenyewe 
ikiwa na mamlaka ya ndani na nje na mimi ni miongoni mwa Wazanzibari wanaounga mkono hatua hiyo".
"Wazanzibari wanataka kuendesha nchi yao yenye mamlaka kamili…mimi binafsi ni muumini wa Muungano wa mkataba,"
"Muungano wa mkataba utaturudishia haki zetu Wazanzibari na sasa hivi tuna Serikali, lakini leo Serikali yetu kila kitu 
lazima tukapige magoti Tanganyika," alisema na kufafanua zaidi kuwa:
"Tunataka Benki Kuu yetu ya Zanzibar na Tanganyika watakuwa na yao…halafu tukishapata Muungano wa mkataba Zanzibar itakuwa huru,....." 
"Inshallah kwa uwezo wa Mwenyenzi Mungu, Zanzibar itarudi katika mamlaka kamili…, Wazanzibari wanachokitaka ni kuungwa mkono na mataifa makubwa,"

http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/09/maalim-seif-ataka-zanzibar-huru.html#more

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment