Wednesday 26 September 2012

Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Nakuunga mkono bwana Makundi.Let the zanzibaris go if they wish too.Tanzania bara has no more to offer or discuss.It there choise 2remain or go.Ngupula



------------------------------
On Wed, Sep 26, 2012 1:51 PM EEST Willy Makundi wrote:

>
> Nico, kwa Seif na wenzake wengi, kuhoji uhalali wa Muungano ni hatua ya kwanza kuhoji Uhalali wa Mapinduzi ya Zanzibar na serikali yake.
>
>Kama Articles of the Union hazikuwahi kupata Ratification je Mapinduzi ya Zanzibar yalipata Ratification wapi? If the Union is null and void, the Revolution was criminal. Aliyoyatenda Karume kwa kutumia Upanga ni halali wakati aliyoyatenda kwa kalamu na karatasi ni batili?
>
>For many years I wanted to hold on to this Union. At this point, if Zanzibaris want out of the Union, let them go - with prejudice. Waondoke woote na Watanganyika huko warudi woote. Alimradi hawahatarishi usalama wetu na sisi wao, wakae kwao na sisi kwetu. Kuhusu mali na biashara zao zilizoko walikokuwa tutajadili pole pole baada ya kutengana.
>
>You think this is irrational? How rational do you think their claim for the legitimacy of the Union is?
>
>Waacheni waende! Tena kwa muda mfupi iwezekanavyo na tusiwe na ahadi yoyote ya majadiliano kuhusu ushirikiano wa baadaye.
>
>Do you think I am p***d off? You betcha!
>
>
>
>mchilyi7.0
>ps! Nimeambiwa jukwaa lina demokrasia zaidi nimekujachungulia.
>
>
>
>-----Original Message-----
>From: Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com>
>To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
>Sent: Tue, Sep 25, 2012 9:50 pm
>Subject: Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
>
>
>
>Ngoja nichangie kidogo nami. Kama vile kijana na binti wanaamua kuwa marafiki. Baada ya urafiki kunoga wanaamua kukaa pamoja. Kama Fred leo nao wanapata mtoto. Wanaendelea kuishi pamoja. Wanaongeza wa pili, watatu nk. Mzaliwa kwanza anafika umri wa kwenda nasari. Basi anapelekwa shule hatimaye wote wanakuwa shule. Wazazi wanasikia watoto wao wanaishi pamoja. Hatimaye wanaanza kwenda kuwatembelea na zawadi. Wanashiriki sherehe za ubatizo/ubarikio/kuwekwa wakfu, kipaimara nk. Ingawaje hakuna karatasi za bomani au za kanisani lakini wana barua za mapenzi tele na sasa wana watoto ambao wana vyeti vya kuzaliwa na vingine vikibeba majina ya wazazi wote wawili. Miaka inaenda hadi hawa wanakuwa wazee. Watoto wakuwa nao wanakuwa na wenzi wao. Lakini ndugu wenye wivu siku zote huuliza kam hiyo ni ndoa ijapokuwa sheria ya serikali na vigezo vyote vitambua hiyo ndoa. Utashangaa wajukuu wakiuliza maswali eti babu wewe ulifunga ndoa wapi? Tuoneshe cheti cha ndoa.
Babu anawaonesha barua urafiki na maendeleo waliyofanya kwa miaka 48 na ushee hivi na bibi. Baba na bibi wanakufa kama ilivyo kaida kufa lakini wanaacha wosia nyuma - wosia wa baba. Muishi kama familia moja na wala msibaguane kutakana na kaya zenu.
>
>Nauliza, je hiyo ni ndoa halali? Na hao watoto wa ndoa ni watoto halali? Je na wajukuu ni halali au haramu? Ni mwendawazimu tu na shetani ndio watasema hiyo siyo ndoa halali! Kichaa tutamwombea atapona tu na shetani tunalo jina la kumkemea na ashindwe milele!
>
>
>
>
>
>
>
> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
> To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
> Sent: Tuesday, 25 September 2012, 19:15
> Subject: RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
>
>
>
>
>Jabir,
>
>Niliwahi kuuona Mkataba wa Muungano pale Mtaa wa Lugoda - tulikuwa mimi, Makunga na Jesse. Ile nakala ilipotolea wapi sijui. Lakini pia nimewahi kuambiwa kuwa kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano kuna nakala za Muungano ingawa sijawahi kwenda kuulizia kwa sababu hili suala halinisumbui. Ninachokitaka ni taifa langu la TANZANIA na siyo makaratasi.
>
>Aidha, ukisoma makala za kitaaluma za wanazuoni waliouchimbua muungano utabaini kwamba wanasema kuwa baada ya Nyerere na Karume kuusaini mkataba huo, Nyerere aliupeleka muswada wa sheria ya muungano kwenye Bunge la Tanganyika ili mkataba huo uwe sheria lakini Karume kwa kuwa hakuwa na bunge yeye alitakiwa aupeleke kwenye Baraza la Mapinduzi na hakuna uhakika iwapo alifanya hivyo. Hivyo, makosa ya wapi ulipelekwa au uko wapi leo yasilete suala jipya kwamba eti hakukuwa na muuungano wa mkataba. Hamuwezi kuungana bila mkataba hata kama mkataba huo ni wa maneno. Nadhani unafahamu aina za mikataba na kimsingi hata katiba inaweza isionekane kama ilivyo ya Uingereza. Sisemi kwamba huu wa kwetu hauonekani au iwe hivi na vile, bali ninachosema ni kwamba tusiwadanganye watu kwamba eti huu si muungano wa mkataba kwa kuwa ili wawili ama zaidi muungane ni lazima mkubaliane na makubaliano yenu ndiyo mkataba kisheria.
>
>Kuhusu hicho mnachosema kwamba muungano wa kikatiba - ni usanii wa lugha ambao unaweza kufanikiwa kwa watu wachache tu, labda wenye nia ya kupokea lolote masikioni mwao ili kukidhi haja zao za kisiasa. Katiba ni nini? Katiba si chombo cha kuunganisha mataifa mawili bali ni zao la watu wa mataifa mawili au moja au zaidi kukaa pamoja na kuamua kwamba huu ndio uelekeo na uelekezi wetu kama taifa. Ndiyo maana hatutengeneza Katiba ya Muungano hadi baada ya miaka kadhaa kupita huku ile ya Tanganyika ikitumika kwa muda kuziba pengo kutokana a kuundo ule wa serikali mbili. Huwezi kuutumia mkataba badala ya katiba wala katiba badala ya mkataba; ni vitu viwili tofauti na wala hatuwezi kusema kimoja ni bora kuliko kingine.
>
>Kwenye jukwaa moja niliwaambia kwamba watu waache kudanganyana na akaibuka muungwana mmoja pale niliposema hakuna kitu kama "muungano wa mkataba" duniani (kwa maana ya akina Seif) na yeye akatolea mfano wa Muungano wa Ulaya (EU). Alikuwa amechoka kufikiri tu. Kama Zanzibar inataka muungano wa mkataba na inaulinganisha na ule wa EU, sasa mbona tayari upo wa kwetu Addis Ababa uitwao Muungano wa Afrika (AU)? Sasa huo wanaousema akina Seif utakuwa kati ya nchi zipi wakati yakitekelezwa ya kwao Tanzania itavunjika na kuzaliwa vinchi viwili vya kibabaishaji? Je, haitakuwa muingiliano wa mambo? Hawajalifikiri hili. Unawezaje kuwa na huo muungano wa mkataba wa vinchi hivi ndani ya AU yenye muungano wa mkataba tayari?
>
>Hii ya muungano wa kikatiba na wa kimkataba ni lugha za akina Maalim Seif wanaotaka muungano huu uvunjike. Wanatumia lugha za kujikosha tu lakini shida yao kubwa wauvunje muungano (kwa maslahi binafsi zaidi na ubaguzi) lakini kwa kuwa wanajua kuwa Zanzibar bado itahitaji kuitegemea Bara, basi wanajipendekeza na wazo la muungano wa mkataba. Nani alisema kuna muungano usiokuwa na mkataba? Nchi iliyoungana inawezaje kukaa bila katiba?
>
>Ndiyo maana nasema, tuache kudanganyana; tuwe wakweli kwamba Wazanzibari wengi wamedanganywa na pia wengi watanataka kila kilichomo ndani ya muungano na kilichomo je ya muungano - ndiyo kisa cha kusema vunja muungano huu lakini tunautaka huu.
>
>Semeni mtakavyo kama ikibidi tu na hakuna anayewazuia lakini msidhani kwamba tutakaa kimya, na pia sisi tunaoutaka muungano tukijibu haina maana tunawakataza nyie msioutaka msiseme mpendalo.
>
>Ushan'fahamu Jabir?
>
>Matinyi.
>
>
>
>
>Date: Tue, 25 Sep 2012 09:13:12 -0700
>From: jabirgood@yahoo.com
>Subject: Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
>To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
>Matinyi, M, mkataba wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ww umepata kuuona? Unajua kama huu umewahi kuulizwa hata Bungeni, achilia mbali kwenye Mahakama Kuu Zanzibar ambako Zanzibar Attorney General alisema yeye hajawahi kuuona.
>
>Inabaki ukweli kwamba muungano huu ni wa kikatiba. Umetajwa na Katiba ya URT ya 1977. Na muungano wa kikatiba na wa mkataba ni vitu viwili tofauti.
>
>Kweli, CUF wamekuwa na msimamo wao kuhusu Muungano. Lakini sauti ya sasa inakuja ktk wakati tofauti sana na huko nyuma. Na ujue sasa wanaotaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano Tz si CUF peke yao, hata CCM wengi wameamua kubadilika.
>
>Mzee Hassan Nassor Moyo na baadhi ya mawaziri ktk SMZ ni baadhi yao.
>
>Uzuri ni kwamba sasa kuusema Muungano huu si UHAINI. Kwa hivyo, usikasirike watu wakiusema, si ndio wanavyouona? Nawe ni haki yako kuuona unavyouona. Basi mawazo yote haya yaachiwe yasikike na wanaoyatoa wawe huru.
>
>Hata Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba anasema jambo hili - watu wapewe uhuru kutoa maoni yao na wao wanachukua kila maoni yanayotolewa.
>
>Nimalize kwa kukukumbusha kuwa suala la mjadala khs Muungano wa Tz, limeigharimu sana Zanzibar, zaidi kuliko Bara ambako

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment