Wednesday 26 September 2012

RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Na mimi nakubaliana kabisa na Jesse ila nina nyongeza,

Kwanza ni kweli kwamba muungano tulionao unawafaidisha zaidi Wazanzibari japo wenyewe hawaoni. Niliwahi kutembelea pale katika wizara ya masuala ya muungano iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, na kufanya kautafiti tu kadogo. Nikagundua kuwa tangu waziri, baadhi ya wakurugenzi na baadhi ya watumishi wengi ni Wazanzibari.

Siyo hapo tu, ukitazama idara nyingi za serikali Wazanzibari wamejazana, lakini ukienda Zanzibar ni mara chache sana kusikia m-bara anafanya kazi kule. Tena juzi tu hapa wametangaza kuwa wabara watapewa vitambulisho vya ugeni kama wageni wa nchi nyingine. Huu ni ubaguzi wa hali ya juu.

Wazanzibari siyo tu kwamba hawautaki muungano, bali hupenda kujinasibu kuwa wao asili yao ni uarabuni hasa Oman. Ndiyo maana wengi wanadhani muungano ukivunjika watapata misaada mingi kutoka huko na nchi nyingine za uarabuni.

Mbali na Serikalini, ukija uraiani nako wana rasilimali nyingi tu, tangu biashara, kilimo na mengineyo. Hayo yote hawaoni, wanatamani muungano uvunjike tu.

Msimamo wangu mimi ni kwamba, mtoto akililia wembe mpe. Ni kweli wapo wanaoona kuwa kuvunja muungano ni sawa na kupindua nchi. lakini nadhani ifike mahali tuwaache wachukue nchi yeo na Tanganyika tubaki na nchi yetu. Na hili ndilo wanalolitaka japo wengine hawasemi wazi. Ndiyo utawasikia wanasema wanataka muungano wa mkataba, mara serikali tatu na mengineyo.

Vinginevyo chokochoko za muungano hazitakwisha. kila siku serikali inajadili kero za muungano na kila upande unahoji muungano. Muungano ukivunjwa na kila upande ukapima faida na hasara ya kukaa peke yake, huenda siku za usoni pande hizo zikarudiana kwa makubaliano maalum ya wananchi wenyewe.

--- On Wed, 9/26/12, Jesse Kwayu <jesse.kwayu@guardian.co.tz> wrote:

From: Jesse Kwayu <jesse.kwayu@guardian.co.tz>
Subject: RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, September 26, 2012, 2:45 AM

Matinyi umenena,

Kwamba tatizo siyo mkataba Muungano uko wapi, ila kuna kitu nyuma ya pazia!

Nimekuwa na kawaida ya kujizuia kusema mambo juu ya Muungano hasa ninapoona kauli za kuubeza.

Kwa kawaida, watu hupenda kitu kama kina faida kwao. Hupenda kitu ambacho walau wana cha kunufaika nacho.

Ninapozungumza haya ninamaanisha kwamba kama kina Jabir na wengine hawajui basi leo wajue, iliyokuwa inaitwa Tanganyika haijanufaika na Muungano kama ilivyo kwa Zanzibar, huu ni ukweli mchungu.

1.       Zanzibar hakuna ardhi yoyote ya maana ya kuwekeza, Wazanzibari wametapakaa kila kona ya iliyokuwa inaitwa Tanganyika wakiwa wamewekeza; ni haki yao!

2.       Zanzibar haina rasilimali yoyote ya maana, lakini wananufaika na rasilimali zote za iliyokuwa inaitwa Tanganyika; ni haki yao!

3.       Zanzibar walianza kelele nyingi baada ya ile iliyokuwa ikiitwa Zanzibar route kufungwa. Hii ilikuwa ikitumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wajanja kwamba wanaagiza bidhaa kwa ajili ya Zanzibar ambako ushuru wa forodha ulikuwa chini, lakini soko lao lilikuwa iliyokuwa ikiitwa Tanganyika; ilipodhibitiwa kwamba kama bidhaa hizo zinakwenda Tanganyika ni lazima tu zilipiwe ushuru sawa na wengine wanaoingiza bidhaa kwa ajili ya soko hilo; kwao hilo likachukuliwa kama ni uonevu kwa kuwa tu wameambiwa biashara ni lazima uwe uwanja sawa;

4.       Fikiria nafasi za uongozi katika nchi; Zanzibar wana nafasi nyingi zaidi kuliko ilivyo kwa iliyokuwa inaitwa Tanganyika; wakazi wasiofikia milioni na nusu wa Zanzibar wana uwakilishi wa kupindukia ndani ya Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, wana mawaziri, wana mabalozi, wakurugenzi na maofisa wengine wakubwa ndani ya serikali na mashirika ya umma ambao hawafanani na uwiano wa idadi ya wakazi wa pande hizi mbili za Tanzania; kwa waliokuwa Tanganyika haijawahi kuwa tatizo kwa hali hiyo na wanaikubali; wana  Bunge lao (Baraza la Wawakilishi), wana serikali yao na mawaziri kedekede; ruksa na haki kwao!

5.       Tanganyika ni basket food ya Zanzibar, kila kitu; nasisitiza kila kitu, kuanzia nyanya (nyonyo), vitunguu, mchele, nyama, kila aina ya mbogamboga, kutaja kwa uchache tu; hivi vyote vinapatikana kama vile vinatoka mkoa mmoja kwenda mwingine; haki yao!

6.       Tanganyika ni uwanja wa kujidai wa Wazanizbari, wamewekeza kweli kweli, hawabaguliwi na hakuna uwezekano wa kubaguliwa kwa sababu humu Tanganyika wanaonekana kama tone la maji ndani ya bahari kuu; haki yao!

7.       Hizi ni baadhi tu ya faida, lakini Wazanzibari wanaoeneza hoja za kuubeza Muungano hawataki kuzitaja kwa kuwa watasutwa; lakini niseme hapa pia kwamba nini msukumo huu wa kuamini kuwa Muungano ni tatizo? Wanaamini kwamba bila Muungano watapata marafiki wengi huko duniani, watapata misaada mingi huko duniani, watapata vya bure na kusaidiwa ili kuleta maendeleo; ni kelele zilezile za kutaka mteremko, siyo kitu kingine. Wenye hoja hizi wanasahau kwamba katika dunia tunayoishi leo hakuna taifa lolote lililoendelea kwa misaada, nasema halipo, ingekuwa hivyo ndivyo basi Tanzania isingekuwa kama ilivyo leo.

8.       Nilisema awali kwamba nimekuwa na tabia ya kujizuia kuzungumza mambo haya, lakini nimefunguka leo kwa kuwa wapo wanaotaka kuaminisha watu kwamba Tanganyika inafaidi sana Muungano, ukweli ni kinyume chake;

Kama alivyosema Matinyi hapo juu, ni vema wanaopiga ndogo ndogo ya Mungano wa mkataba wakasema wazi kuwa hawautaki Muungano ili tuanza upya na kwa amani, lakini ukweli utabaki kuwa watakaopata hasara hapa siyo waliokuwa Tanganyika, hawana cha kupoteza, wana cha kufaidi zaidi kwa kupata fedha za kigeni kwa kila kinachoelekea kisiwa cha Zanzibar, wana cha kufaidi kwa sababu suala la kufanya babysitter halitakuwako tena, ni wazi na dhahiri mambo haya. Nawasilisha.

Jesse

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Mobhare Matinyi
Sent: Tuesday, September 25, 2012 9:16 PM
To: Wanabidii googlegroups
Subject: RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Jabir,
 
Niliwahi kuuona Mkataba wa Muungano pale Mtaa wa Lugoda - tulikuwa mimi, Makunga na Jesse. Ile nakala ilipotolea wapi sijui. Lakini pia nimewahi kuambiwa kuwa kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano kuna nakala za Muungano ingawa sijawahi kwenda kuulizia kwa sababu hili suala halinisumbui. Ninachokitaka ni taifa langu la TANZANIA na siyo makaratasi.
 
Aidha, ukisoma makala za kitaaluma za wanazuoni waliouchimbua muungano utabaini kwamba wanasema kuwa baada ya Nyerere na Karume kuusaini mkataba huo, Nyerere aliupeleka muswada wa sheria ya muungano kwenye Bunge la Tanganyika ili mkataba huo uwe sheria lakini Karume kwa kuwa hakuwa na bunge yeye alitakiwa aupeleke kwenye Baraza la Mapinduzi na hakuna uhakika iwapo alifanya hivyo. Hivyo, makosa ya wapi ulipelekwa au uko wapi leo yasilete suala jipya kwamba eti hakukuwa na muuungano wa mkataba. Hamuwezi kuungana bila mkataba hata kama mkataba huo ni wa maneno. Nadhani unafahamu aina za mikataba na kimsingi hata katiba inaweza isionekane kama ilivyo ya Uingereza. Sisemi kwamba huu wa kwetu hauonekani au iwe hivi na vile, bali ninachosema ni kwamba tusiwadanganye watu kwamba eti huu si muungano wa mkataba kwa kuwa ili wawili ama zaidi muungane ni lazima mkubaliane na makubaliano yenu ndiyo mkataba kisheria.
 
Kuhusu hicho mnachosema kwamba muungano wa kikatiba - ni usanii wa lugha ambao unaweza kufanikiwa kwa watu wachache tu, labda wenye nia ya kupokea lolote masikioni mwao ili kukidhi haja zao za kisiasa. Katiba ni nini? Katiba si chombo cha kuunganisha mataifa mawili bali ni zao la watu wa mataifa mawili au moja au zaidi kukaa pamoja na kuamua kwamba huu ndio uelekeo na uelekezi wetu kama taifa. Ndiyo maana hatutengeneza Katiba ya Muungano hadi baada ya miaka kadhaa kupita huku ile ya Tanganyika ikitumika kwa muda kuziba pengo kutokana a kuundo ule wa serikali mbili. Huwezi kuutumia mkataba badala ya katiba wala katiba badala ya mkataba; ni vitu viwili tofauti na wala hatuwezi kusema kimoja ni bora kuliko kingine.
 
Kwenye jukwaa moja niliwaambia kwamba watu waache kudanganyana na akaibuka muungwana mmoja pale niliposema hakuna kitu kama "muungano wa mkataba" duniani (kwa maana ya akina Seif) na yeye akatolea mfano wa Muungano wa Ulaya (EU). Alikuwa amechoka kufikiri tu. Kama Zanzibar inataka muungano wa mkataba na inaulinganisha na ule wa EU, sasa mbona tayari upo wa kwetu Addis Ababa uitwao Muungano wa Afrika (AU)? Sasa huo wanaousema akina Seif utakuwa kati ya nchi zipi wakati yakitekelezwa ya kwao Tanzania itavunjika na kuzaliwa vinchi viwili vya kibabaishaji? Je, haitakuwa muingiliano wa mambo? Hawajalifikiri hili. Unawezaje kuwa na huo muungano wa mkataba wa vinchi hivi ndani ya AU yenye muungano wa mkataba tayari?
 
Hii ya muungano wa kikatiba na wa kimkataba ni lugha za akina Maalim Seif wanaotaka muungano huu uvunjike. Wanatumia lugha za kujikosha tu lakini shida yao kubwa wauvunje muungano (kwa maslahi binafsi zaidi na ubaguzi) lakini kwa kuwa wanajua kuwa Zanzibar bado itahitaji kuitegemea Bara, basi wanajipendekeza na wazo la muungano wa mkataba. Nani alisema kuna muungano usiokuwa na mkataba? Nchi iliyoungana inawezaje kukaa bila katiba?
 
Ndiyo maana nasema, tuache kudanganyana; tuwe wakweli kwamba Wazanzibari wengi wamedanganywa na pia wengi watanataka kila kilichomo ndani ya muungano na kilichomo je ya muungano - ndiyo kisa cha kusema vunja muungano huu lakini tunautaka huu.
 
Semeni mtakavyo kama ikibidi tu na hakuna anayewazuia lakini msidhani kwamba tutakaa kimya, na pia sisi tunaoutaka muungano tukijibu haina maana tunawakataza nyie msioutaka msiseme mpendalo.
 
Ushan'fahamu Jabir?
 
Matinyi.
 
Date: Tue, 25 Sep 2012 09:13:12 -0700
From: jabirgood@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi, M, mkataba wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ww umepata kuuona? Unajua kama huu umewahi kuulizwa hata Bungeni, achilia mbali kwenye Mahakama Kuu Zanzibar ambako Zanzibar Attorney General alisema yeye hajawahi kuuona.

Inabaki ukweli kwamba muungano huu ni wa kikatiba. Umetajwa na Katiba ya URT ya 1977. Na muungano wa kikatiba na wa mkataba ni vitu viwili tofauti.

Kweli, CUF wamekuwa na msimamo wao kuhusu Muungano. Lakini sauti ya sasa inakuja ktk wakati tofauti sana na huko nyuma. Na ujue sasa wanaotaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano Tz si CUF peke yao, hata CCM wengi wameamua kubadilika.

Mzee Hassan Nassor Moyo na baadhi ya mawaziri ktk SMZ ni baadhi yao.

Uzuri ni kwamba sasa kuusema Muungano huu si UHAINI. Kwa hivyo, usikasirike watu wakiusema, si ndio wanavyouona? Nawe ni haki yako kuuona unavyouona. Basi mawazo yote haya yaachiwe yasikike na wanaoyatoa wawe huru.

Hata Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba anasema jambo hili - watu wapewe uhuru kutoa maoni yao na wao wanachukua kila maoni yanayotolewa.

Nimalize kwa kukukumbusha kuwa suala la mjadala khs Muungano wa Tz, limeigharimu sana Zanzibar, zaidi kuliko Bara ambako baadhi yenu wengi, mnaona hauna tatizo.

Kwenye mjadala fulani nilipata kusema, Kama Wazanzibari wanasemwa kwa kuupinga Muungano kwa kuona haujawanufaisha, kwanini ung'ang'aniwe kwa nguvu kubwa Tanzania Bara?

Tunasubiri mbele ya safari itakuwaje.

Jabir+

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, September 24, 2012 1:15 AM
Subject: RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Hajasema kipya. Tangu zamani ndio msimamo wa CUF; labda tu tuseme kwamba sasa wamekuja na lugha mpya ya muungano wa mkataba ambao ni upuuzi tu. Hakuna kitu kama hiki duniani. Kwani huu wa sasa hauna mkataba? Je, huo wanaoutaka una tofauti gani na huu wa AU?
 
Date: Mon, 24 Sep 2012 09:29:46 +0300
Subject: Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
From: denis.matanda@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Si ndio msimamo wake ( na wa chama chake) all along au?

2012/9/24 John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>

Dear All,

Makamo wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Katibu Mkuu wa CUF apasuwa bomu kwa CCM na kwa Watanganyika pale alipoweka

msimamo wake na wa CUF wazi kabisa kwa kutamka jana mkutanoni Bububu kuwa..."wakati umefika kwa Wazanzibari kuendesha nchi yao wenyewe 

ikiwa na mamlaka ya ndani na nje na mimi ni miongoni mwa Wazanzibari wanaounga mkono hatua hiyo".

"Wazanzibari wanataka kuendesha nchi yao yenye mamlaka kamili…mimi binafsi ni muumini wa Muungano wa mkataba,"

"Muungano wa mkataba utaturudishia haki zetu Wazanzibari na sasa hivi tuna Serikali, lakini leo Serikali yetu kila kitu 

lazima tukapige magoti Tanganyika," alisema na kufafanua zaidi kuwa:

"Tunataka Benki Kuu yetu ya Zanzibar na Tanganyika watakuwa na yao…halafu tukishapata Muungano wa mkataba Zanzibar itakuwa huru,....." 

"Inshallah kwa uwezo wa Mwenyenzi Mungu, Zanzibar itarudi katika mamlaka kamili…, Wazanzibari wanachokitaka ni kuungwa mkono na mataifa makubwa,"

http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/09/maalim-seif-ataka-zanzibar-huru.html#more

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--

Wasalaam

Denis Matanda,

Mine Supt,

Nzega - Tanzania.

" Low aim, not failure, is a crime"

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
0 comments:

Post a Comment