Monday 10 September 2012

Re: [wanabidii] Re: Wakazi wa Bonyokwa tunahitaji msaada wa kutengenezewa barabara

Mheshimiwa Mbunge wetu. Hebu tupia macho pia suala la foleni kwa barabara ya ubungo kimara mbezi. Jamani tunapata shida sana, pengine wewe na viongozi wengine muangalie namna ya kupata angalao suluhu ya dharura. Mkandarasi ashauriwe afanye matengenezo sehemu moja kwa awamu badala ya kufunga sehemu nyingi kwa wakati mmoja hali inayoongeza foleni.

--- On Mon, 9/10/12, John Mnyika <mnyika@yahoo.com> wrote:

From: John Mnyika <mnyika@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] Re: Wakazi wa Bonyokwa tunahitaji msaada wa kutengenezewa barabara
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Matthew Mdidi" <matthew.mdidi@yahoo.com>
Received: Monday, September 10, 2012, 3:02 AM

Matthew na wengine,

Asanteni kwa maoni na mapendekezo yenu.

Nawaomba wananchi na wadau wa sekta binafsi mnaotumia Barabara ya Kimara-Mavurunza-Bonyokwa muwasiliane na Diwani wa Kimara Pascal Manota 0784954657 awape utaratibu wa kuchangia kuwezesha kukodi grader kusawazisha na malori kuweka vifusi kwenye maeneo korofi kwa dharura wakati tukisubiri matengenezo ya haraka yanayopaswa kufanywa na Serikali kwa kodi zetu; mimi tayari nimeshampatia mchango wangu wa shilingi laki mbili kati ya milioni moja zinazohitajika, wewe je?

Izingatiwe kwamba tayari Wizara ya Ujenzi ilishakubali kuihudumia barabara hii na wiki chache zilizopita niliandika barua kwa meneja wa TANROADS Mkoa wa Dare es Salaam kutaka hatua zake kwa hali mbovu ya barabara hiyo pamoja na kuwa kero wa wananchi inamwaibisha Rais Kikwete mbele ya wakazi husika kwa kuwa alitembelea mwaka 2010 na kuahidi itajengwa kwa kiwango cha lami.

Aidha, mwaka 2011 ilifanyiwa matengenezo ya kawaida lakini kwa sasa imeharibika tena kufuatia mvua zilizonyesha, hali mbovu ya barabara hiyo inaathiri pia hatua za kupunguza msongamano kwenye barabara ya Morogoro wakati huu ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) unapoendelea kwa kuwa barabara hiyo hutumika kama njia mbadala kutoka Manispaa ya Kinondoni mpaka Manispaa ya Ilala.

Leo na kesho nitakuwa kwenye mfululizo wa mikutano ya baraza la madiwani wa jiji hivyo wakati nikiendelea kufuatilia majibu ya hatua za haraka za serikali kuwezesha matengenezo makubwa, naomba  utaratibu kwa kushirikiana na diwani na watendaji kwa ajili ya kuunganisha wananchi wa maeneo husika na wadau wengine ili kufanya matengenezo madogo kupunguza kero uendelee.

 

 

John Mnyika (Mb)

10/09/2012

 

--- On Fri, 8/24/12, Matthew Mdidi <matthew.mdidi@yahoo.com> wrote:


From: Matthew Mdidi <matthew.mdidi@yahoo.com>
Subject: Wakazi wa Bonyokwa tunahitaji msaada wa kutengenezewa barabara
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "mnyika@yahoo.com" <mnyika@yahoo.com>
Date: Friday, August 24, 2012, 12:49 PM

Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kimara, barabara ya kwenda Bonyokwa kuanzia eneo la Kimara Mwisho ina hali mbaya sana.
 
Kwa kuwa nafahamu serikali yetu haina pesa za kugharimia huduma muhimu za jamii niko tayari kuwahamasisha wenzangu tuchange pesa za kununulia dizeli kwa ajili ya greda la kusawazishia barabara hiyo.
 
Kama Mbunge wangu utakuwa umebanwa na majukumu mengi ya Kitaifa, unaweza kumtuma Diwani wetu apite nyumba hadi nyumba kuchukua michango hiyo.  
 
Kama Mheshimiwa Diwani naye atakuwa amebanwa sana, naamini Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu anaweza kutuchangisha pamoja na kuwa anatoka Chama Cha Mapinduzi.  
 
Kama haya yote yatashindikana itabidii umwombe Mama Salma Kikwete atembelee tena eneo letu ili barabara hii itengenezwe usiku na mchana.
 
Tunaomba ulipe umuhimu hili wasije akina Nchemba wakapata la kuongea. Asante sana Mheshimiwa.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment