Saturday 8 September 2012

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Waliochangia Na Kiasi Kilichopatikana Hada Sasa.... ( Uptodate)

Nitatoa pia tsh 10,000/= Naomba unipe utaratibu mzuri wa kuituma mkuu
Shedrack Maximilian
B.Sc. Env.Health Science
Bagamoyo District Council, Tanzania
shedrack_maximilian@yahoo.co.uk
+255(0754)944-504
+255(0715)844-504

--- On Sat, 8/9/12, Shy-Rose Bhanji <shyrose2@hotmail.com> wrote:

From: Shy-Rose Bhanji <shyrose2@hotmail.com>
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Waliochangia Na Kiasi Kilichopatikana Hada Sasa.... ( Uptodate)
To: "maggid mjengwa " <mjengwamaggid@gmail.com>, "wanabidii@googlegroups.com " <wanabidii@googlegroups.com>, "mabadilikotanzania@googlegroups.com " <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Saturday, 8 September, 2012, 11:21

Maggid,
Pole nyingi kwa mjane wa Daud Mwangosi na Mungu amlaze peponi mwenzetu.

Nami nitachangia laki 2 kwenye harambee. Naomba nijulishe jinsi ya kutuma pesa.

Mungu akubariki kwa moyo wa kujitolea.

Shy-Rose!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

-----Original Message-----
From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Date: Sat, 8 Sep 2012 06:17:15
To: <wanabidii@googlegroups.com>; <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Subject: [Mabadiliko] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Waliochangia Na
Kiasi Kilichopatikana Hada Sasa.... ( Uptodate)



1. Chris Cremence 100,000
2. Anonymous 500,000
3. Maggid Mj
engwa 100,000
4. Raymond Kasoyaga 20,000
5.Edward Mgogo 10,000
6.Joachim Kiula 5,000
7.Libory Muhanga 5,000
8.Geofrey Kagaruki 10,000
9.Sadiki Mangesho 10,000
10. Edwin Namnauka 40,000
11.Daud Mbuba 10,000
12. Anonymous 200,000
13.Mikidadi Waziri 6,000
14. Bungaya Mayo 5,500
15. Abraham Siyovelwa 50,000
16. Godfrey Chongolo 22,222
17. Jacob Mwamwene 51,000
18. Dennis Bwimbo 153,683
Jumla: 1,298,000 ( Milioni Moja Na Laki Mbili Na Tisini Na Nane Elfu Na Mia Tatu Na Themanini Na Tatu)

Kiasi kilichobaki kutimiza lengo? 900,000 ( Kiasi cha shilingi lakini tisa)
Background:
Ndugu zangu,
Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye tena.
Nimemfahamu Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni kwa kupiga picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.
Mara nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.
Leo Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne; Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.
Jana na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana kusikia habari hizo.
Kwa vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used) na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.
Kutokana na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi.
Napendekeza ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni msaada mkubwa.
Mjengwablog bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.
Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.
Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.
Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.
Namna ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.com/
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment