Friday 14 September 2012

Re: [wanabidii] Nini kifuate baada ya Maandamano ya Waandishi Jangwani?

Ndugu Selemani Rehani na wachangiaji wengine mumenena nawaunga mkono
asilimia mia kwa mia. Haitakuwa jambo la busara na ujasiri kwa
wanahabari pamoja na umma kwa ujumla kuishia hapa, lazima kuchukua
hatua zaidi.

Hawa wanaojiita ndugu zetu wakati huo huo wanatutesa( brutality),
kutunyanyasa na kutuchinja kama kuku lazima tuwachukulie hatua
stahiki. Ni muhimu kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote
waliohusika kwa namna moja au nyingine ili tukomeshe unyama
wanaowafanyia raia.

Ninashauri tujitahidi kufahamishana vizuri nini majukumu yao, nini
mipaka yao na je sheria zinasemaje? Ili tuone kama kuna sheria na
taratibu zilitungwa kwa sababu ya kuwalinda wakoloni na vibaraka wao
tuzipigie kelele zibadilishwe haraka iwezekanavyo.

Pia ninashauri muungano wa wanahabari uwe chachu na kiunganishi kwa
watu wote wanaopenda haki na uhuru wa kila mtu, tuwatafute lawyers
kuona ni namna gani wanaweza kuzisaidia familia za marehemu wote
waliouwawa kwa njia kama ya Mwangosi kuifungulia kesi serikali pamoja
na wote wanaohusika na unyama huo.

Nina imani watanzania na watu wote wanaopenda haki na amani watawaunga
mkono kuchangia gharama za kesi hizo. Kwa pamoja tutaweza, ukombozi wa
haki na uhuru wa mwanadamu hauji kiraisi raisi tu lazima tujifunge
kibwebwe

Mungu ibariki Tanzania, Mungu iokoe nchi kutoka kwenye mikono ya shetani

2012/9/14 Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>:
> Wanabidii,
>
>
> 1. Hatua za kisheria: Nakubaliana na wazo la kuendelea kuchukua hatua za
> kisheria kama ilivyopendekezwa hapo chini pia na wachangiaji wengine. Ni
> vyema wanasheria wakashirikishwa ili watoe muongozo na ushauri wa namna bora
> zaidi na utaratibu mzuri unaotakiwa kufuatwa.
>
> 2. Shinikizo: Tumejifunza kuwa shinikizo ni njia nzuri sana ya kuifanya
> serikali iwajibike. Hivyo tuendelee ku-demand wale waote waliohusika na
> ukatili huu wawajibike na wafikishwe katika vyombo vya sheria. Haya
> yafanyike kwa kuendelea kuandamana na kupaza sauti zetu katika kila kona.
> Waziri mwenye dhamana, IGP, RPC ni miongoni mwa watu wachache tu ambao
> wanatakiwa kuwajibika.
>
> 3. Tuwe na mkakati wa kuhakikisha tunaungwa mkono na jamii yote: Ili tuweze
> ku-achieve katika hili, ni lazima tuyaangazie matukio yote ya mauaji
> yaliyofanywa na Polisi. Tusijikite katika tukio la marehemu Mwangosi peke
> yake. Tuyatazame matukio ya mauaji kwa upana wake na kwa ujumla wake. Kwani
> wote hawa ni Watanzania na ni binadamu. Pia tuyatazame hata yale yaliwahi
> kufanyika miaka ya nyuma. Kwa mfano yale mauaji ya Zanzibar mwaka 2000/01,
> mauaji ya Arusha, Arumeru, Igunga, Singida, na Morogoro. Pia tuyaangalie
> mauaji yanayofanywa na Polisi katika maeneo ya migodi. Wapo wananchi wengi
> tu wamepigwa risasi na kufa.
>
> Ili tungwe mkono ni muhimu tukapanue mjadala lakini pia tufikishe taarifa
> kwa kila mwananchi ili kila Mtanzania aweze kuelewa yanayotokea katika
> uhalisia wake. Tunalazimika ku-document matukio haya na kufanya
> dissemination na awareness kubwa kwa kupitia njia mbalimbali. Lazima
> tupeleke ujumbe ambao ni very clear kuwa Polisi wanafanya mauaji. Lakini
> tusiishie hapo tu, tunganishe kero nyingine zinazowakabili wananchi kutokana
> na utendaji mbovu wa Jeshi la Polisi, kama vile kukithiri kwa rushwa,
> matatizo ya traffic barabarani, kutumia nguvu kupita kiasi, kubambikizia
> kesi watu, kuwalinda wahalifu, na utamaduni uliojengeka wa kuwaacha wahalifu
> miongoni mwa polisi na wasiokuwa polisi wakitamba bila kuchukuliwa hatua
> zipasazo (impunity).
>
> 4. Mjadala wa kina: Lakini pia tuwe na mijadala ya kina kutathmini na
> kuangalia utendaji wa Jeshi la polisi kwa ujumla wake. Historia yake?
> uhusiano wake na chama tawala/tabaka tawala? Je jeshi letu liko huru?
> linafanya kazi zake kwa kuzingatia weledi? je ni kweli jeshi letu ni non
> partisan? sheria za Jeshi la polisi zikoje? yaani the legislative framework,
> je sheria ya Police Force and Auxiliary Services Act 2002 inaendana na
> katiba yetu? je Police Force Regulations 1995 zinasemaje?, Police General
> Orders zinasemaje? mafunzo ya polisi? mishahara na mazingira wanayofanyia
> kazi polisi? uhusiano wa vyama vya siasa na polisi ukoje?
>
> sheria ya vyama vya siasa inasemaje? Pia hatuna budi kuangalia madaraka
> makubwa ya Rais, je yanatusaidia kuwa na taasisi kama hizi huru? Iwapo Rais
> anamteua IGP, Rais anateua viongozi wakubwa wa Jeshi la Polisi, anamteua
> Jaji Mkuu na majaji wote, anateua Baraza la Mawaziri mojawapo ni mwenye
> dhamani ya kusimamia Jeshi la Polisi, anamteua mwanasheria mkuu wa serikali,
> anateua wenyeviti walioko katika Tume muhimu kama vile tume ya haki za
> binadamu, ambazo ungetegemea zingeweza kuwalijibissha jeshi la polisi,
> anateua msajili wa vyama vya siasa na mwenyekiti na makamishina wote wa Tume
> ya uchaguzi n.k. Huyo huyo Rais ndio Mwenyekiti wa Chama, je hapo unategemea
> nini? Ni lazima Jeshi la polisi litahakikisha kuwa chama kilichoko
> madarakani kinaendelea kutawala, jeshi la polisi litalinda ruling class kama
> ilivyokuwa wakati wa wakoloni.
>
> Hivyo inabidi tu-link mjadala huu na sheria nyingine kandamizi kama sheria
> ya magazeti ya 1976. Na kwa kweli mjadala huu ni muhimu ukatoa mapendekezo
> ambayo yatasaidia kupeleka miswada Bungeni ya kuweza kuondoa sheria
> kandamizi kama zilivyoainishwa na Tume ya Nyalali na pia haya yatakuwa ni
> mawazo mazuri sana kuingia katika marekebisho ya katiba.
>
> Muhimu sana tuwe na taasisi huru na watumishi wa umma ambao ni neutral,
> hawaegemei upande wowote. Licha ya kuingia katika mfumo wa vyama vingi,
> taasisi zetu bado si huru. Licha ya mabadiliko mengi, Jeshi la polisi liko
> politicized na hayakufanyika marekebisho ya msingi ili liweze ku-save katika
> mazingira mapya ya kisiasa. Taasisi nyingi zinaegemea chama tawala na hili
> ni lazima tulijadili, ndio maana walioko katika chama tawala walikuwa
> wakipinga suala la kuandika katiba mpya. Kwani wanalijua hili. Tumerithi
> sheria mbaya kutoka kwa Wakoloni na hakukuwa na juhudi za msingi kuziondoa
> au kuzifanyia marekebisho. Huu ni wakati muafaka kuwashirikisha wadau wote
> katika kufanya mabadiliko ya msingi. Tunahitaji taasisi huru, vyombo huru na
> watumishi wa umma ambao ni non-partisan. Naomba tuwashirikishe wataalam wa
> fani mbalimbali ili tuweze kuwa na mjadala wenye afya.
>
> Inapofika Kamanda Kova anawaamulia watu kuwa wasifanye maandamano bali eti
> wafanye press conference, then unajua hapa there is something wrong.
> Unaposikia leo Mkuu wa Wilaya, pia ni Mbunge unaona kuwa hatuna mfumo mzuri,
> unaposikia mkuu wa Wilaya pia ni mjumbe wa Baraza la CCM vijana, then unajua
> hatuna mfumo mzuri na hatuwezi kuwa na utawala bora, kwani hakuna structure
> ya accountability, hakuna separation of powers na hakuna checks and
> balances. Mabadiliko ya katiba ni lazima yatupe mambo haya. Na ni wajibu
> wetu kuyadai na kubadilishana mawazo na wananchi wote kwa ujumla ili wayaone
> haya. Ndio maana hata uteuzi wa majaji ni utata mtupu.
>
> Ahsante
>
> Selemani
>
>
>
> ________________________________
> Date: Fri, 14 Sep 2012 01:26:26 -0700
> From: calabashtz88@yahoo.com
> Subject: Re: [Mabadiliko] Nini kifuate baada ya Maandamano ya Waandishi
> Jangwani?
> To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Sifahamu kama bongo kuna structures za 'citizen's arrest' ambapo mwananchi
> anaweza kumfanyia arrest alleged mhalifu.
> Lakini mke na wazazi/ndugu wa marehemu wanaweza kufungua mashtaka ya madai
> ya fidia.
> 1. Kwenye kesi kama hizi, watuhumiwa na asasi wanayo represent kikazi k.m.
> wale watuhumiwa polisi ambao waliofanya hicho kitendo cha mauaji (kisheria
> inabidi tuseme wanaodaiwa kufanaya mauaji- japokuwa picha tumeziona) na
> asasi 2 yaani jeshi la polisi (inaweza kuwa Mkoa au Makao Makuu) na wizara
> inabidi wafunguliwe mashtaka ya jinai- hapa yatakuwa 'Mauaji kwa makusudi'.
> 2. Wizara husika nayo inaweza kufunguliwa
> mashtaka kwenye Mahakama ya Katiba kujibu tuhuma za 'Abuse of Public
> Office'.
> 3. Mke wa marehemu na watoto wake na wazazi wa marehemu wanatakiwa kupeleka
> madai mahakamani ya fidia kutoka jeshi la polisi; wizara na wale waliofanya
> mauaji.
> Tatizo hapa ni kesi ya nyani etc.
> Waendesha mashtaka ni polisi; wanaotakiwa kufanya upelelezi ni polisi.
> Kuhusu abuse of public office hiyo ni masuala ya kikatiba na mahakama ya
> katiba.
> Fidia ni civil suit.
> Wa press club ya Iringa wajaribu kutafuta WLAC ili kupata ufafanuzi zaidi
> juu ya madai ya fidia.
> Aidha UPC tunaweza kufungua mashtaka mahakama ya katiba juu ya police
> brutality na kuzuiliwa kufanya kazi zetu kwa amani na usalama.
>
> From: Katulanda Frederick <fkatulanda@gmail.com>
> To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
> Sent: Friday, September 14, 2012 10:33 AM
> Subject: [Mabadiliko] Nini kifuate baada ya Maandamano ya Waandishi
> Jangwani?
>
> Kuibana serikali kunataka mbinu, weredi wa hali ya juu, je, unashauri
> nini kifanyike baada ya maandamano ikiwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
> Iringa na Askari wengine hawatafikishwa mahakani?
>
> Tujadiliane.
>
> --
> 'Walk The Talk'
> Frederick M. Katulanda
> Cell: +255 784 642620,
> Alternative:+255 754 642620
> E-mail: fkatulanda@yahoo.com
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
>
>
>
>
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
>
>
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment