Tuesday 18 September 2012

RE: [wanabidii] MADAKTARI WAMWOMBA RADHI RAIS NA WATANZANIA

Yona Maro,
Watanzania si wajinga kiasi hicho. Tatizo la kukosekana huduma bora  za afya halitayeyuka kama barafu wakati wa jua kali eti vile watu kama wewe na hao wanokupa taarifa  wanaibua uvumi kutokana na waroho wachache wasiowatakia Watanzania maendeleo kama hao walioinamisha vichwa chini kwa aibu ya kujijua  kuwa ni madakatari mamuluki wa wanasiasa waumini wa "siasa uchwara"( nukuu ya Mh. Rostam Aziz!) wanaotawala Tanzania kwa sasa. Mungu si Athumni, ipo siku tutafika Watanzania nasi  tutafika tunakotaka kwenda.
Mwl. Lwaitama
 
> Date: Mon, 17 Sep 2012 09:49:56 -0700
> Subject: [wanabidii] MADAKTARI WAMWOMBA RADHI RAIS NA WATANZANIA
> From: oldmoshi@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Ndugu zangu
>
> Nasikia Baadhi ya madaktari waliokuwemo kwenye mgomo wamewaomba radhi
> watanzania na rais wa tanzania mhe jakaya mrisho kikwete kutokana na
> mgomo uliotokea .
>
> Mimi kama mtanzania nimewasamehe na nawatia moyo waendelee na kazi zao
> kama kawaida na wale waliofunguliwa mashtaka mbalimbali yanayohusiana
> na mgomo , wafutiwe kesi hizo warudi makazini na hata wale wanafunzi
> pia wasamehewe warudi makazini kama kawaida .
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

0 comments:

Post a Comment