Tuesday 18 September 2012

Re: [wanabidii] Lake Manyara National Park eti iko Kenya ? ! ! !

Matinyi- Wakala anaangalia wapi anapata 10% anaweza akauza kizuri au kibovu mradi apate  pato lake (commission)kama wale wanaoangalia pato na ubinafsi wao tu Afrika hata kama wananchi wanaathirika vibaya wao watapokea silaha, kukubali vitakuendelea au kufanyike vurugu nchi isitawalike (Malema S.A na wengine kama yeye Congo, Burundi, TZ).Na wale viongozi wa mila wanaofaidika wao wenzao wakiteseka na viongozi wa vijiji mitaa wakiuza ardhi au kukusanya hela za kuzoa taka na taka zisizolewa na wakandarasi waliongia nao mikataba na masuala mingine ya ubinafsi na hujuma. Hata katika familia na koo wapo ndugu na jamaa utajitahidi kulea na kusomesha ili waje kujikomboa wajitegemee (kuwakomboa)ni wachache sana watakuja kulipa fadhila. waliowengi ndio watakuwa wapanga majungu kwako licha ya wewe kuvumilia mengi wakati ukiishia nao, wakiwa wavivu, waharibu mali, wavunja vyombo, washiba wao kwanza kabla ya wewe mtafutaji uliyetafuta; wakiwa wao sasa wanacho ukiwaomba kitu watakuona ombaomba bugha bora tu ujikalie kwako. Watafaidika wengine toka kwao kuliko wewe. Tendawema wendezako-usingoje shukrani. Hao uliowaelewa ukifa ghafla na hata ukiacha Wosia, watakuwa ni hao watakaofanya njama kudhulumu mafao au miradhi ya familia yako wakiwa wanafahamu ukweli. Hizo ndio tabia za bin-adam. Mnyama anaona yote na kufahamu ila kanyimwa kauli. Bin-adam anaona, kusikia, kunusa zuri na baya na kutafakari, ana uwezo wakulinganisha akatenda. Lakini, anaweza akatenda kinyume kinyume cha silika 5 zote alizopewa na mwenyezi mungu. Na hata mwanasheria anayejua sheria na mwenye dini lakini akiwa wakili wako anaweza atatetea kuwa huna kosa hata kama umetenda kosa analolijua lakini atatafuta vigezo vya kukuokoa na ukamlipa mamilioni (malipo-commission). Kisha akaenda jumba la sala kusali kama kawaida yake kwani si ana dini!!
 
S.Afrka ni wawekezaji wakubwa pia nchini kwetu, tunafaidika na nini kutoka kwao? Makambi yao au makazi ya hoteli na machimbo-biasha zao bila ya shaka wameweka kuta na majibwa makubwa ya kuuma watu. Watanzania na wengine waliohamia huko wanapigwa, kuchomewa mali zao moto kwa visingizio kadhaa. Nao wabongoland wanan'gang'ania huko pamoja na shida zote lakini hapa kwao kina kila kitu cha kujisulubu na kuwekeza bali mradi uonekane upo south. Labda Msumbiji na Angola ambako watanzania wengi wamekimbilia. Lakini, tunasikia huko msumbiji majambazi wakuu watumia silaha msumbiji ni wabongoland.Hatujui kiasi cha ukweli wake.Unapoingia kumkomboa mtu angalia msalaba au kibra ukijua kuwa unafanya kitendo cha upendo cha neema kwa mungu malipo yako ya baadae.
 
Tu mabwege hasa-maana hata pale unapoona kuna vijana na wazee wanachoma matofari wanauza, kuna mawe ya gypsum ambayo ukichoma unapata udongo kama siment unaweza ukajengea, mafundi wajengao nyumba vijijini wapo-wamama na wengineo utakuta wamepanga ndoo foleni kilomita 1 wanachota maji machafu yanayochafuliwa na binadamu, mifugo na wanyama pori. Haiingii akilini kuwa wanaweza kuchanga shilingi 500 kila kaya moja ktk kaya 2000 au watu wazima 2000 kijiji hicho wakapata milioni moja ambapyo ni mifuko 60+ wakachukua tofari, mawe na kuboresha visima vya jadi zaidi ya kimoja kijijini wakapunguza tabu ya kutembea saa nane za usiku kuwahi maji na kuliwa na fisi. Wanaweza wakachanga kila wiki 500/= hizo wakapata fedha baada ya nusu mwaka za kirefu wakachimbiwa na mkandarasi wa kumtafuta wao maana wachimba boreholes wamejaa kibao. Haipandi kichwani hata-ila tuambie kuandamana na kuvunja maduka tunaonewa ni nambari one!! Tupo slow ktk matendo ya kuweka kujudi kuzalisha au kutengeneza vizuri kuliko ya maneno mengi, ushabiki na uharibifu. Ndio maana tunafikia hata kung'oa viti na mabomba ya national stadium baada ya timu zetu kufungwa badala ya kutunza tukaonekana nasi tumesonga mbele.Magereji barabarani hutaki ugharimie uweke mbali, kukata mambomba ya mradi wa mamilioni wa kuleta maji nk. Culture hii ya kipuuzi tuibadili kwa kuingiza unyago wa elimu ya aina fulani mashuleni. 
 
Wanatucheka, mabwege na tutachekwa sana tuendako ktk karne hii ya kujituma binafsi na kujikomboa usitegemee kuajiriwa. Na tukianza vita watakuwa wakwanza kutuleteasilaha huku wao wanavuna madini, wanyama pori nchikavu na wale wa baharini. Mbona wanaingia nchini na ng'ombe pembe ndefu wanakata miti, wanachoma mkaa, wanatubebesha mbao kuvusha tunakubali na kisha tunapiga kelele kuwa tunaonewa? Kwa ubwege tunawabeba kwa bodaboda, makonteina, tunawafisha ndani ya magunia na viroba na ndani ya majumba yetu wanaingia kufungua mahoteli; tunawaoza na tunawapa ardhi kisiri.
 
Kwao wenzetu na majirani zetu-huwezi ukapeleka hata pua ukahamia. Ninakubali hii ya kuwa mabwege. Mwekezaji akifika gate la ukaguzi la GVT hataki kukaguliwa, gate keeper akigoma kufungua mlango anachapwa makofi halafu kesi inachukua miaka kadhaa gatekeeper wa GVT hapati haki mbele ya mahakama ya nchi yake!-Tu mabwege.
 
Tusikilize radio za nchi yetu vijana wanasimulia vitendo vya uchafu wanavyofanyiwa kufikia kupewa hata mbwa ktk mapenzi na hao wageni. Hutokea hata kuwe na kesi ya dhuluma au uonevu ikionyeshwa ktk TV mara utasikia TV station inaomba radhi baadae kwa kuonyesha kesi ya uonevu ambayo ipo mahakamani. Je, tutajuaje ili wanaharakati waifuatilie? Sio kila mtu atajua kinachotokea dunia nzima bila ya vyombo vya habari. Hata ikiwa mahakamani isitangazwe ili wahusika waifuatilie na kutoa misaada ili anayeonea aache kuonea? Sasa inapotokea Nchi jirani na ya mbali inaonea Nchi nyinginekwa kutangaza uongo-Mbuga. Je, Wizara ya Utalii na ya mambo ya nje havihusiki kutatua tatizo once anf for all lisijirudie counter with aggressive adverts internationally kuwa mbuga zipo TZ? Hakieleweki.
 

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, 18 September 2012, 23:35
Subject: RE: [wanabidii] Lake Manyara National Park eti iko Kenya ? ! ! !
Dokta, tatizo ni kubwa zaidi - hao waliotangaza hapo ni Waafrika Kusini. Yaani mambo yamefikia kwamba yeyote tu anaweza kusema kitu fulani ni cha Kenya - ingawa nahisi hawa watu waliokota hizi habari Kenya. Na kwa ubwege tunaendelea kufungua milango ya utalii.  Mawakala wote wa Afrika Kusini wanatumia uwanja wa Nairobi kufikia na kuondokea. Kuna faida gani ya sisi kuwapigania hawa watu kupata uhuru? Cha ajabu ni kwamba KIA ipo pale.   
Subject: Re: [wanabidii] Lake Manyara National Park eti iko Kenya ? ! ! !To: wanabidii@googlegroups.comFrom: hkigwangalla@gmail.comDate: Tue, 18 Sep 2012 20:21:13 +0000Duh! They are just smarter business people these 'aggressive' Kenyans unlike 'slow' Tanzanians (as they always call us)...nobody in the Kenyans gov would actually tell the business people in the tourist sector to advertise as they do but they improvise to attract more clientele towards Kenya... Tanzanians have to change our mindsets...and promote and nurture talents than kill and discourage them...eti sisi tunadhani vipaji vipo kwenye sanaa tu kumbe hata kwenye uongozi na ujasiriamali - na hivi ni vya muhimu zaidi given their impact esp kwenye multiplier effect!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
From: "wkihigwa@yahoo.com" <wkihigwa@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 18 Sep 2012 17:11:33 +0000 (UTC)
To: <wanabidii@googlegroups.com>; <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Lake Manyara National Park eti iko Kenya ? ! ! !

Mi nashaa tunakazana eti tupo tayari kupigana na Malawi kugombania Ziwa Nyasa wakati kuna vitu tunavyo tayari ni vya kwetu wala si vya utata wa mpaka tunawaacha walio nje ya nchi waangie na kufaidi. Nilitarajia kwa njisi wakenya wanavyotumia vibaya ujirani mwema Waziri Membe angekwisha kutoa kauli kukemea tabia hii ya nchi ya jirani kudai baadhi ya rasilimali zetu eti ziko nchini kwao.

Tukitoa kauli ya kulaani hiyo tabia najua itawasumbua na watafikiria mara mbili kabla ya ku-claim na kuwatapeli watalii kwa kuwavusha mipaka bila wao kujuaWilliam Kihigwa
Mobhare Matinyi wrote:

Jamani Watanzania tunazidi kuwa nchi ya mabwege huku wenzetu wakivuna tu...............

.......Soma hapo chini eti Lake Manyara National Park iko Kenya? Hii safari inaanzia Nairobi na kuishia Nairobi na hawa watu wanaletwa Tanzania na kuambiwa kuwa Lake Manyara iko Kenya.............................................

8 day Majestic Wildlife Migration Safari Package

Amboseli Serena Safari Lodge, Kenya.

Places you will visit: This East Africa package includes: Amboseli Serena Lodge, Amboseli National Park, Lake Manyara Lodge, Lake Manyara National Park - Kenya, Serengeti Sopa Lodge, Serengeti National Park, Ngorongoro Sopa Lodge, Ngorongoro Crater - Tanzania.
Suitability: This package is excellent for guests wanting to enjoy a full, rewarding safari through the highlights of Kenya and Tanzania.
Note: Based on arrival and departure from Nairobi.

http://www.eastafrica.co.za/Vacation_Packages-travel/8-day-wildlife-migration-safari-package.html
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.   -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  

0 comments:

Post a Comment