Friday 21 September 2012

Re: [wanabidii] Kauli ya UAMSHO dhidi ya film

 
Wapo hao wanaohubiri ubungo mataa daily wanahubiri na kujijibu wenyewe wakikashifu ukristo. wakati wa ramadhan maeneo mengine ukikutwa unakunywa maji au unakula unapigwa au huuziwe soda unaambiwa haiuzwi mfungo. yanachomwa makanisa ZNZ, Misri na kwingineko-wakristu wanakula jiwe kimya. Zama hizo wakati wa pasaka au Kristmas misa ya usiku au mchana ya sikukuu wakiingia kanisazi kufanya fujo-hakuna aliyerudisha fujo hiyo. Huu ni uhuru uliokomaa kwa wakristo kuzingatia kutotumia upanga kwa upanga. Tusifike huko kwa wenzetu maana tumeoana watu wa ndini mchanganyiko sio kama huko kwa wenzetu. Tumechanganyika kidini na kikabila. Mungu atuzidishie amani.
 
Fika mitaa ya DSM na miji mingine wakati wa sherehe za ekaristi, kipaimara, christmas ubungo, mwenge etc. Kama upo DSM fika Kanisa la RC Mwenge la Maximillian Kobe. Utashangaa kukuta akina mama wamevaa hijabu lakini wanauza biashara zao pamoja na mapambo, kadi za sherehe husika ili wapate pesa. Utakuta hapo nje wa wigo wa kanisa langoni vijana wanauza vitu mbali mbali wanajua wakritu wakiingia na hasa wakitoka watanunua. Wanauza picha za Yesu na mitume wake na hata kuzitembeza mitaani nao baadhi si dini ya kikristu. Hapo mwenge kanisaniwanauza kanda za nyimbo za kwaya za dini za kikristu, wanauza Rosari za aina aina na nyingine wamevaa shingoni. Nyimbo hizo wanapiga ktk chombo chao za music nao wanacheza lakini anacheza ndombolo au kidukwi. Anachoangalia yeye ni hela au kipato sio utengano wa dini. Ikifika Aid ya waislamu hata vijana wa kikistu na wamama wanauza vya dini hiyo ili wajipatie mkono kwenda tumboni. Hao watakao vurugu nchini waangalie kwanza kinachoendelea. wananchi hawaoni hizo tofauti na vijana wana marafiki mchanganyiko wa dini na tunashirikiana tulipo. kama hili ni la kutakia kula na sifa kisiasa au kidini-imekula kwao. Hali hali sio sio hivyo upendo zaidi kuliko utengano.

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, 21 September 2012, 9:07
Subject: Re: [wanabidii] Kauli ya UAMSHO dhidi ya film
Aliyeiona filamu hii naomba anitumie link ya ni namna gani naweza kuipata!!!!

 
2012/9/21 Charles Misango <misangocharles@yahoo.com>

Binafsi sipendi kabisa mtu ama kundi la watu wa dini moja kukashifu, kudhalilisha, kudhihaki wala kutukana wale wa dini nyingine. Bila kutafuna maneno, naungana na wale wote wanaopinga filamu hiyo kwani ni ujinga mkubwa.
Mungu mwenyewe anajua nani anayemwabudu na nani mwigizaji. Lakini pamoja na kujua hivyo, bado rehema na neema zake anazimwaga kwa wote, ndio maana anapowaangazia jua ama kunyesha mvua, habagui kama sisi tunavyojaribu kubagua.

Lakini wakati ndugu zetu waislamu wakilaumu na kulaani vikali filani hiyo( narudia kukubaliana nao), lazima nao watambue kuwa HAWANA HAKI, kutukana, kudhalilisha, kukashifu dini za wengine hususan wakristo!

Leo hii hapa nchini, makundi mengi ya waislamu wanafanya mihadhara mchana hadi usiku wakiutukana ukristo, tena kwa kutumia biblia wakitafsiri wanavyotaka wao kwa matusi na udhalilishaji mkubwa. Hivyo, nachukua nafasi hii, kuwataka wakati wanapolaani filani hiyo, basi sote tuungane kuwalaani hata wale waislamu wanaoudhalilisha ukristo.

Waislamu wanaotukana dini za wenzao wajue kuwa wanawaumiza wengine kama wao wanavyoumia wakitukaniwa ya kwao! Isiwe Mkuki kwa Nguruwe, kwa binadamu mchungu. Sote kila mtu aheshimu dini ya mwingine hata kama unaamini kuwa yako ndio bora zaidi na ya mwingine ni pumba! Hubiri, tangaza ya kwako kwa umaridadi na watu watavutwa kuja kwako bila kugusa ya wengine. Mambo ya Ngoswe aachiwe Ngoswe mwenyewe
--- On Thu, 9/20/12, John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> wrote:

From: John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] Kauli ya UAMSHO dhidi ya film
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, September 20, 2012, 5:40 PM
Kauli ya UAMSHO dhidi ya film

Ndugu wa Kiislaam,
Inasikitisha sana kuona kuwa kuna baadhi ya Waislaam ambao ni watu wepesi kiasi cha kuweza kuchokozwa na wajinga wasio na 
thamani wakajiingiza katika mitego na vitendo vyao vikawashirikisha pia Waislam wasiokubaliana na vitendo vyao viovu. 
Daima Mwislamu anatakiwa awe katika haki; asimuasi Mwenyezi Mungu ili kuepukana na ghadhabu zake Allah (S.W.).

Uislaam ni dini ilokamilika kwa kumdhaminia mwanaadamu ufumbuzi na miongozo ya mambo yote katika maisha yake ya Dunia na 
ndio maana Allah (S.W.) kakitukuza Kitabu chake kwa kusema:
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  

0 comments:

Post a Comment