Thursday 13 September 2012

Re: [wanabidii] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Utaratibu Wa Kupokea Michango Ya Kijumuiya....

Mbona tumeanza kujadili mambo yasiyokuwa na tija? Huko tulikofika ni
mbali sana na hakuendani na lengo zima la kutoa michango yetu na
salaam za rambirambi kwa familia ya marehemu Mwangosi.

Kuna watu hawakufurahia jambo la michango ya vikundi kuwa na majina ya
vyama vya siasa au vikundi bila shaka ni wanachama wa chama pinzani.
Majina mengi yaliyopo kwenye orodha ni ya watu binafsi walioguswa na
msiba wa marehemu Mwangosi. Kwa mtanzania ni jambo la kawaida kutoa
rambirambi anapotutoka mtu. Si jambo la ajabu wala la kushangaza watu
katika makundi mbalimbali kujitokeza na kutoa salaamu za rambirambi
kwa wafiwa. Na wakati mwingine kueleza pengo walilolipata kwa
kuondokewa na marehemu.

Mimi siyo mwanachama wa Chadema lakini naona hapa kundi linamgusa
mlalamikaji ni Chadema. Tukumbuke kwamba marehemu alikuwa anatafuta
habari za Chadema kufungua matawi huko Nyololo na hivyo sioni ubaya
wowote kama wanachama wa Chadema popote walipo kuchangia rambirambi
kwa jina la chama chao maana wameona wamuunge mkono shujaa aliyekufa
kwa kutafuta habari zinazowahusu. Kama na kundi alilomo mlalamikaji
linapenda kutuunga mkono linaweza kuleta mchango kupitia blog hii kwa
jina lao sioni kama kuna tatizo

Binafsi ningewashauri wanachama wa Chadema ata tawi lile walibatize
jina la Mwangosi ili kumuenzi ipasavyo shujaa huyo.
Ninamuomba mlalamikaji atwambie jina gani watumie kama mchango ni wa
kikundi si wa mtu mmoja? Tunataka wajitambulishe vipi? Wapo ambao
awakutaka kujitambulisha (anonymous) na wapo wliotaka kujulikana
wamejitambulisha kwa majina yao, sijui hao nao unawaambie wanataka
kujitangaza na kujipatia umaarufu na hivyo unawashauri waende habari
na maelezo?

Binafsi nafikiri kujitambulisha ni vizuri maana unaelewa kwamba
mchango wako umepokelewa na utapelekwa ulikokusudia upelekwe (familia
ya Mwangosi). Na hii ni muhimu zaidi kama mchango ni wa kikundi maana
wanaopewa kuwasilisha ni wachache.

Mtu au kikundi kujitambulisha ni vyema na wala hakuna tatizo michango
inakaribishwa toka kwa yeyote aliyeguswa. Isionekane kama ni dhambi
kikundi kutoa rambirambi zake kupitia blog hii. Nafikiri pia kwa
Chadema kutoa rambirambi si kutafuta umaarufu kwa damu za watu bali ni
msiba uliotokea kwenye shughuli yao na hivyo unawahusu haswaa.
Tusiwakatishe tamaa watu au vikundi ambavyo vingependa kutoa michango
yao kupitia blog hii eti kwa sababu wanatafuta umaarufu

2012/9/13 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>:
>
> Kailima,
> Huyo ndivyo alivyo si unaona anamtuhumu mkusanya michango kuwa ni mwana CCM. Uwe makini naye.
>
>
>
> ------------------------------
> On Thu, Sep 13, 2012 07:15 BST kailima kombwey wrote:
>
>>Mzee Lwaitama.
>>
>>Mjengwa hajaanzisha harambee ya kutunisha mfuko wa chama ameanzisha
>>harambee ya kukusanya michango kwa ajili ya Mjane wa Maangosi.
>>
>>Kama chama chochote kinataka kujitangaza kupitia michango hiyo kifunge
>>safari hali kwa Mjane kikiwa na kundi la wanahari kisha watoe mchango wao
>>kisha wana habari wawapige picha za video na mnato ili warushwe hewani na
>>wajipatie umaarufu kupitia damu ya mwanadamu.
>>
>>Mratibu wa michango katoa msimamo kwamba hakuna masuala ya itikadi zozote
>>za kidini au za kichama. Kama wewe unadhani siyo haki washauri hao
>>unaodhani hawatendewi haki bila kuonekana ni chama au dini gani watafute
>>njia nyingine ya kujinadi kupitia damu ya mtu ili wajinadi. Nashauri waende
>>Idara ya Habari Maelezo au waende Iringa au Tukuyu ili wajidadi na siyo
>>kupitia hapa.
>>
>>Chukua mud utafakari.
>>
>>Nakutakia asubuhi njema.
>>On Sep 13, 2012 9:01 AM, "Lutgard Kagaruki" <lutgardk@yahoo.com> wrote:
>>
>>> Sawa kabisa Mwalimu. LKK
>>>
>>>
>>>
>>> ------------------------------
>>> *From:* Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>
>>> *To:* wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>> *Sent:* Wednesday, September 12, 2012 8:52 AM
>>> *Subject:* RE: [wanabidii] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Utaratibu
>>> Wa Kupokea Michango Ya Kijumuiya....
>>>
>>> Ndugu Mjengwa,
>>> Nakupongeza kwa kujitolea kubeba jukumu hili la kitukufu la kuongoza
>>> harambee ya Mjane wa Daudi Mwangosi. Mimi nitajangia kabla ya mwisho
>>> wa wiki hii. Ila napata shida kuelewa kwa nini mtu au kikundi kinataka
>>> kuchangia halafu tusipewe taarifa ya jina la mtu huyu au kikundi hiki.*Pale msibani Rungwe tuliwaona Mh Prof Mwandosa wa CCM na Mh. Dr Slaa wa
>>> Chadema wakiwa wamekaa pamoja kwa karibu kabisa na wote wakijitolea kila
>>> mtu kufuatilia elimu ya watoto kadhaa wa marehemu Mwangosi*. Sijaelewa
>>> kwa nini unayasema haya ninayo nukuu "*ili kuepuka kuchanganya siasa
>>> kwenye suala hili la kijamii na la kibinadamu katika kumsaidia mjane wa
>>> marehemu, kama mratibu wa harambee hii, napendekeza kuanzia sasa wale wote
>>> watakaochangishana kijumuiya, hususan za kiitikadi, basi, michango yao
>>> iwakilishwe hapa kama michango ya kutoka Jumuiya za Watanzania, popote pale
>>> walipo hapa duniani.*" Kwa nini wewe ujue ni nani walichangia pamoja na
>>> itikadi zao, na sisi wengine tusijue wala familai hisijue? Mantiki yake
>>> ni nini? Kama wewe utajua na sisi wote na familia yake ijue kama
>>> wanaochanga ni jumuia ya CCM au jumuia ya Chadema au ya CUF au TLP...
>>> Sioni ubaya wowote kila mtu anayetoa mchango kujitambulisha kikamilifu kwa
>>> jina au jumuia ili tumfahamu, Mh Prof Mwandosa wa CCM na Mh. Dr Slaa wa
>>> Chadema , pamoja na Mh Shy Rose Banj wa CCM wameonyesha mfano mzuri
>>> wakutoficha kuguswa kwao na msiba huu na michango yao kwa ndugu wa marehemu
>>> imetangazwa kwa wote. Kwa nini wewe ujue waliochanga na wengine wote
>>> tusijue? Na wewe itikadi yako wengine tunahisi ni CCM lakini ilo si hoja na
>>> michango tutakutumia. Kwa hiyo mimi nilidhani ni vizuri waache watu
>>> wanaochanga kama jumuia za CCM au CUF au Chadema tuwajue. Hata polisi
>>> wakitaka kuchanga mmoja mmoja walioguswa sioni ubaya kuwatangaza tuwajue.
>>> Hata hao wanao jiita Anonymous tafadhali waombe wakuruhusu uwataje kwa
>>> majina maana kwenye harambee hii kila kitu kiwe wazi kwa sababu hii
>>> ni harambee takatifu... Kwa nini kujificha kujulikana kuwa mtu
>>> umechangia, tena wengine kwa hela nyingi?!!! Jambo la kitakatifu kama hili
>>> lifanywe kwa uwazi ndugu yangu Mjengwa. Mchango wangu nitakutumia kabla
>>> ya mwisho wa wiki hii na nawahimiza rafiki zangu wote washiriki harambee
>>> hii kupitia namba za simu ulizotoa. Kwa heshima na taadhima.
>>> Nawasilisha.
>>> Mwl Azaveli Lwaitama
>>>
>>>
>>> ------------------------------
>>> Date: Wed, 12 Sep 2012 05:58:11 +0100
>>> Subject: [wanabidii] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Utaratibu Wa
>>> Kupokea Michango Ya Kijumuiya....
>>> From: mjengwamaggid@gmail.com
>>> To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>>
>>>
>>> Ndugu zangu,
>>> Wengi wameendelea kuitikia wito wa kumchangia mjane wa marehemu mwandishi
>>> Daud Mwangosi .
>>>
>>> Imeanza pia kujitokeza michango ya kijumuiya. Ni jambo jema sana. Hata
>>> hivyo, ili kuepuka kuchanganya siasa kwenye suala hili la kijamii na la
>>> kibinadamu katika kumsaidia mjane wa marehemu, kama mratibu wa harambee
>>> hii, napendekeza kuanzia sasa wale wote watakaochangishana kijumuiya,
>>> hususan za kiitikadi, basi, michango yao iwakilishwe hapa kama michango ya
>>> kutoka Jumuiya za Watanzania, popote pale walipo hapa duniani.
>>>
>>> Natumia fursa hii pia, kwa kutambua kuwa kuna jumuiya mbali mbali za
>>> Watanzania, na za marafiki wa Tanzania kwenye karibu kila kona ya dunia
>>> hii, kuwaomba wenyeviti wa jumuiya hizo kukusanya japo michango midogo kwa
>>> Wanajumuiya wenzao, iwe Watanzania au marafiki wa Tanzania, walio na
>>> utayari wa kuchangia hata kiasi kidogo tu cha pesa kwa mjane wa marehemu.
>>>
>>> Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwangu kwa njia zifuatazo; M-Mpesa,
>>> Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61
>>> 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la
>>> mpokeaji- Maggid Mjengwa, Tafadhali nijulishe kama utatuma kwa njia ya
>>> Western Union )
>>>
>>> Natanguliza shukran,
>>>
>>> Maggid Mjengwa.
>>> http://mjengwablog.com/
>>>
>>> --
>>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>>
>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>>> ukishatuma
>>>
>>> Disclaimer:
>>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>>
>>>
>>> --
>>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>>
>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>>> ukishatuma
>>>
>>> Disclaimer:
>>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>>
>>>
>>>
>>>
>>> --
>>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>>
>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>>> ukishatuma
>>>
>>> Disclaimer:
>>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>>
>>>
>>>
>>
>>--
>>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>>Disclaimer:
>>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment