Thursday 13 September 2012

Re: [wanabidii] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Utaratibu Wa Kupokea Michango Ya Kijumuiya....

Mwalimu Lwaitama na wengine,

Asanteni kwa michango yenu.

Kwa mtazamo wangu, kumsaidia mjane wa marehemu ni suala la kibinadamu na kijamii.  Nimeona ni jambo la hekima nikachukua taadhari ya kutochanganya suala la itikadi za vyama kwenye hili la kumchangia mjane wa marehemu. Ndio msingi wa hoja yangu, wa msimamo wangu pia, kama mmiliki wa Mjengwablog, mtandao wa kijamii bila kujali dini, rangi, kabila na itikadi za watu.
Maggid Mjengwa,
Dar

2012/9/12 mngonge <mngonge@gmail.com>
Namuunga mkono Mlm Lwaitama, tunajua fika kwamba Mjengwa siyo mtu wa
itikadi yoyote na waliotoa hawajali itikadi lakini kama wapo wasamaria
ambao wanapenda wajulikane kwa itikadi zao tatizo ni nini? We don't
care about your political stand, all what we mind is your contribution
irrespective of other things

2012/9/12 Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>:
> Ndugu Mjengwa,
> Nakupongeza kwa kujitolea kubeba jukumu hili la kitukufu la kuongoza
> harambee ya Mjane wa Daudi Mwangosi.  Mimi nitajangia kabla ya mwisho wa
> wiki hii.  Ila napata shida kuelewa kwa nini mtu au kikundi kinataka
> kuchangia halafu tusipewe taarifa ya jina la mtu huyu au kikundi hiki. Pale
> msibani Rungwe tuliwaona Mh Prof Mwandosa wa CCM  na Mh. Dr Slaa wa Chadema
> wakiwa wamekaa pamoja kwa karibu kabisa na wote wakijitolea kila mtu
> kufuatilia elimu ya watoto  kadhaa wa marehemu Mwangosi.  Sijaelewa kwa nini
> unayasema haya ninayo nukuu "ili  kuepuka kuchanganya siasa kwenye suala
> hili la kijamii  na la kibinadamu katika kumsaidia mjane wa marehemu, kama
> mratibu wa harambee hii, napendekeza kuanzia sasa wale wote
> watakaochangishana kijumuiya, hususan za  kiitikadi, basi, michango yao
> iwakilishwe hapa kama michango ya kutoka Jumuiya za Watanzania, popote pale
> walipo hapa duniani." Kwa nini wewe ujue ni nani walichangia pamoja na
> itikadi zao, na sisi wengine tusijue wala familai hisijue? Mantiki yake ni
> nini? Kama wewe utajua na sisi wote na familia yake ijue kama wanaochanga ni
> jumuia ya CCM au jumuia ya Chadema au ya CUF au TLP... Sioni ubaya wowote
> kila mtu anayetoa mchango kujitambulisha  kikamilifu kwa jina au jumuia  ili
> tumfahamu, Mh Prof Mwandosa wa CCM  na Mh. Dr Slaa wa Chadema , pamoja na Mh
> Shy Rose Banj wa CCM wameonyesha mfano mzuri wakutoficha kuguswa kwao na
> msiba huu na michango yao kwa ndugu wa marehemu imetangazwa kwa wote.  Kwa
> nini wewe ujue waliochanga na wengine wote tusijue? Na wewe itikadi yako
> wengine tunahisi ni CCM lakini ilo si hoja na michango tutakutumia. Kwa
> hiyo mimi nilidhani  ni vizuri  waache watu wanaochanga kama jumuia za CCM
> au CUF au Chadema tuwajue. Hata polisi wakitaka kuchanga mmoja mmoja
> walioguswa sioni ubaya kuwatangaza tuwajue. Hata hao wanao jiita Anonymous
> tafadhali waombe wakuruhusu uwataje kwa majina maana kwenye harambee hii
> kila kitu kiwe wazi kwa sababu hii  ni harambee takatifu... Kwa nini
> kujificha kujulikana kuwa mtu umechangia, tena wengine kwa hela nyingi?!!!
> Jambo la kitakatifu kama hili lifanywe kwa uwazi ndugu yangu Mjengwa.
> Mchango wangu nitakutumia kabla ya mwisho wa wiki hii na nawahimiza rafiki
> zangu wote washiriki harambee  hii kupitia namba za simu ulizotoa. Kwa
> heshima na taadhima.
> Nawasilisha.
> Mwl Azaveli Lwaitama
>
>
> ________________________________
> Date: Wed, 12 Sep 2012 05:58:11 +0100
> Subject: [wanabidii] Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Utaratibu Wa
> Kupokea Michango Ya Kijumuiya....
> From: mjengwamaggid@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
>
>
> Ndugu zangu,
> Wengi wameendelea kuitikia wito wa kumchangia mjane wa marehemu  mwandishi
> Daud Mwangosi .
>
> Imeanza pia kujitokeza michango ya kijumuiya. Ni jambo jema sana. Hata
> hivyo, ili  kuepuka kuchanganya siasa kwenye suala hili la kijamii  na la
> kibinadamu katika kumsaidia mjane wa marehemu, kama mratibu wa harambee hii,
> napendekeza kuanzia sasa wale wote watakaochangishana kijumuiya, hususan za
> kiitikadi, basi, michango yao iwakilishwe hapa kama michango ya kutoka
> Jumuiya za Watanzania, popote pale walipo hapa duniani.
>
> Natumia fursa hii pia, kwa kutambua kuwa kuna jumuiya mbali mbali za
> Watanzania, na za marafiki wa Tanzania  kwenye karibu kila kona ya dunia
> hii, kuwaomba wenyeviti wa jumuiya hizo kukusanya japo michango midogo kwa
> Wanajumuiya wenzao, iwe  Watanzania au marafiki wa Tanzania,  walio na
> utayari wa kuchangia hata kiasi kidogo tu cha pesa kwa mjane wa  marehemu.
>
> Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwangu kwa njia zifuatazo; M-Mpesa, Tigo
> Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31,
> 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la
> mpokeaji- Maggid Mjengwa, Tafadhali nijulishe kama utatuma kwa njia ya
> Western Union )
>
> Natanguliza shukran,
>
> Maggid Mjengwa.
> http://mjengwablog.com
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment