Sunday 9 September 2012

Re: [wanabidii] Fw: MTOTO AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI - SONGEA


Mtoto kuoa mama yake mzazi.
Kwa mtazamo wangu,  ni kwa sababu tu kesi hii  imetoka katika vyombo vya habari kutokana na maendeleo ya habari. Lakini, kesi hizi zipo na huenda ni nyingi Tanzania. Hii ni toto yake tuu.
 
Mfano-kuna makabila ambapo baba akifariki na akiwa na wake wengi, mtoto wa kiume wa kwanza anamrithi mke mdogo (wa mwisho wa baba) ambaye si mama yake (Hehe, Bena etc). Wapo wale ambao mke hurithiwa na ndugu wa mume apende asipende bila ya kuangalia tahadhari ya maambukizi ya ukimwi na other hereditary diseases zenye kuleta uendelezo wa vilema. Zipo mila za makabila ya kumsafisha mume au mke mfiwa ili aweze kuoa au kuendelea na ngono katika jamii. Pamoja na elimu ya afya inayotolewa pamoja na Ukimwi kuwepo watu wanausugu na tamaa. Kuoana binamu kwa baadhi ya makabila kunaendelea. Mtoto wa baba mkubwa na mdogo au shangazi na mjomba na udugu mwingine wa karibu  kwa baadhi ya African tribes, wahindi na Waarabu waliomo nchini. Unaweza ukakuta mfarakano wa ndoa lakini ukakuta wazee hao bado wapo pamoja kwa sababu ni binamu wapo pamoja wanatunzwa na watoto na wajukuu na ndugu wengine kwa sababu hana pa kwenda bado hapo ni kwao anyway. Tunakuta kesi hizi katika tafiti mbali mbali nchini.
 
 
Cha kushangaza nilichokiona kijiji kikubwa kimojawapo cha South  Pare, kijana Graduate  wa Engineering UDSM aliyelelewa na kaka yake baba mmoja na mama mmoja kaka huyo alikuwa ameoa. Kaka alifariki ghafla ktk ajali ya gari lakini alikuwa na maduka, mashine za kusaga, mashamba, nyumba nzuri nyingine kapangiza na mali nyingine-magari.
 
 
Kijana aliitwa kusimamia mali za kaka yake na kutakiwa kumrithi huyo shemeji yake ambaye  hasa ni mama yake kwa kumlea toka awe  mdogo mpaka anamaliza chuo kikuu uinjinia.
 
 
Shinikizo la ndugu wa mke kuwa mama huyo akubali kurithiwa na mtoto aliyemlea lilitokana na kuwa mali hiyo ataikosa akikataa kurithiwa. Ndugu wa mume walikataa mali kugawiwa wakitaka mke arithiwe mali ibaki kwao. Mfiwa alirithiwa bila ridhaa yake kwa lazima alilia kilio ambacho hakikusikilizwa akarithiwa.
 
Mara baada ya kurithiwa  akazaa nae mtoto wa uzeeni (middle age) kijana wake ambaye alikuwa ahami nyumba ya mke huyo (Shemeji yake) akiwa na wivu wa kupindukia. Story zao za kijana kufagia uwanja na kumlinda huyo mama kwa wivu wa hali ya juu zilitufanya watafiti  tuitembelee nyumba hiyo wakati wa utafiti wa 'Maisha ya wanawake wa Tanzania wa umri wakati (40-55 yrs The Female Life Cycle- WRDP Study funded by SAREC). Utafiti ulianzia kuhoji watoto wa kike na kiume ili kulinganisha wa umri wa  miaka 9-13; 14-19; 20-24; 25-39; 40-55; 56-64; 65+. Tumekuta pia vijijini akina mama lea  (watu wazima, vibibi) ambao wanaishi na vijana wadogo waliochetuka kwa bangi maisha yakawashinda. Prostitutes wakishindwa maisha mijini na yupaisha mijini na wanaumwa hoi wakirudi kijijini hudakwa na vibabu ambao wana nyumba, miji na mashambamba ambapo yeye hupana nafuu ya maisha lakini vibabu vinamalizika kwa maambukizo. Yeye anaona kapata ndogodogo wa kujionyesha naye.
 
 
Utafiti wetu ulihoji watu mambo mengi ya maisha pamoja na walianzaje ngono na mtu wa aina gani, maisha yao ya ndoa na malezi ya watoto na changamoto wazipatazo. Utafiti huu kwa old age women 65+ years, ulionyesha vituko ambavyo sitaki nimalize kurasa hapa ila ni kusema, kuwa-kuna mengi katika jamii yetu hatuyachunguzi au hatuyaelewi na kukubali kuwa yapo yanatokea hata kama tunayaona.
 
Hizi mila za mibaba wa umri wa miaka 40-90years+ kuoa katoto ka miaka 12-15 ni kitu gani hiki ambacho bado kinaendelea huyu si mwanae. Bado akina mama walioolewa nae wanayatazama. Hii ni kuongeza matatizo ya Cancer za vagina (Vulva)  na cervix kwa akina mama kwa hizo fungus na virus za kupeana
 
 
Yapo mengi yasiyofaa pamoja na masuala yasukumwayo na ushirikina ya zinaa batili. Bado hayo ya ushoga ambayo yapo karne nyingi. Watu na akili zao, elimu na fedha zao wam, wameoa, wanafamilia, wanasali sana katika mahekalu lakini wamewapangia chumba/nyumba shoga (mwanaume mwenzie kama mkewe) . Ipo inaendelea humu bongoland.
 
Hii ya Songea ya mama na mtoto kuoana kutokana na Wosia wa Baba ni mtoto tu wa tukio.
 
--- On Wed, 8/29/12, Avitt Riwa <avittr@yahoo.com> wrote:

From: Avitt Riwa <avittr@yahoo.com>

----- Forwarded Message -----
From: Joseph Temu <joetemu@hotmail.com>
 JAMANI, WANGONI NI KIBOKO!
 
MTOTO AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI - SONGEA
Umati wa watu uliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma watu wapatao 400 wameomba Serikali ichukue Mkondo wa Sheria pia Mtoto wa Pili wa Mama Kondrada Ngonyani ameomba Serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya condorada ngonyani na joseph Mapunda.

Joseph Mapunda mwenye umuri wa miaka 40 amesema ameweza kuishi kindoa na Mama yake Mzazi Condorada Ngonyani 70 baada ya yeye kukubaliana wenyewe yeye na mama yake mzazi kuishi kindoa kama mume na mke alipo ulizwa Mama alikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mume wake ambaye ni Mtoto wake Joseph Mapunda.
Mama Condorada Ngonyani mwenye umuri wa miaka 70 ambaye ana ishi kinyumba na mtoto wake watatu wa kumzaa mwenyewe kama Mke na Mume hapo anaonekana akisononeka kwa nini jamii iingilie ndoa yake
Kwa mkoa wa Ruvuma hii ni mara ya kwanza mtoto wa kiume Joseph Mapunda pichani hapo juu kutembea na mama yake mzazi. Wana Ruvuma wanauliza tume jikwaa wapi watanzani hadi kupoteza mila desturi na maadili ya mtanzania pia kukiuka sheria za dini
Joseph Mapunda ana sema upendo ni upendo amempenda mama na anaishi kindoa wamependana nyie watu mnataka nini kwetu ?
Mama Condorada Ngonyani anasema mara baada ya kufariki mume wake Mzee Mapunda alimchagua mtoto wake amrithi baba yake
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na wtoto kuangalia kati sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa
 
 
*************************************************************************************** *************************************************************************************** This e-mail and any attachments are proprietary to NMB PLC. Any unauthorized use or interception is illegal. The views and opinions expressed are those of the sender, unless clearly stated as being those of NMB PLC. This e-mail is only addressed to the addressee and NMB PLC shall not be responsible for any further publication of the contents of this e-mail. If this e-mail is not addressed to you, you may not copy, distribute or disclose the contents to anyone nor act on its contents. If you received this in error, please inform the sender and delete this e-mail from your computer.
Get connected with TIGO INTERNET - the fastest and most reliable internet in Tanzania! Read more at www.tigo.co.tz/internet Full details of Millicom and our disclaimer should be inspected at http://www.millicom.com/email_disclaimer.cfm This email should be read solely in conjunction with our disclaimer.
*************************************************************************************** *************************************************************************************** This e-mail and any attachments are proprietary to NMB PLC. Any unauthorized use or interception is illegal. The views and opinions expressed are those of the sender, unless clearly stated as being those of NMB PLC. This e-mail is only addressed to the addressee and NMB PLC shall not be responsible for any further publication of the contents of this e-mail. If this e-mail is not addressed to you, you may not copy, distribute or disclose the contents to anyone nor act on its contents. If you received this in error, please inform the sender and delete this e-mail from your computer.
______________________________________________________________________
This email has been scanned by the Symantec Email Security.cloud service.
For more information please visit http://www.symanteccloud.com/
______________________________________________________________________
CONFIDENTIAL NOTE: The information in this E-mail and any attachments transmitted are originated by SABMiller or any of its subsidiaries companies, is intended to be privileged and/or confidential and only for use of the individual, entity or company to whom it is addressed. If you have received this e-mail in error please destroy it and contact the sender. If you are not the addressee you may not disclose, copy, distribute or take any action based on the contents hereof. Any total o partial unauthorized retention, dissemination, distribution or copying of this message is strictly prohibited and sanctioned by law
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  

0 comments:

Post a Comment