Saturday 15 September 2012

Re: [wanabidii] CHADEMA WAMBURUZA NAPE MAHAKAMANI

Mheshimiwa Nape Tunategemea mambo mengi mazuri kutoka kwako wewe ukiwa Msemaji Mkuu wa chama kinachoongoza nchi hii ya Tanzania, na ambacho kina sifa ya kuwa chenye kudumisha Amani na Mshikamano Tanzania.Nadhani kusema unataka kwenda mahakamani kuthibitisha Chama kidogo kuliko cha kwako kuwa kinafadhiliwa fedha kutoka ulaya ni kama kujishushia heshima yako wewe binafsi na chama unachokiongoza ambacho ni kikubwa kuliko hiki unachoshindana nacho.Kwanza chama hicho si kikubwa kama cha kwako, pili ili kikue ni lazima kipewe misaada mbalimbali, kwa lengo la kukuza demokrasia. hapa sioni ulichokiona wewe hata ukaona ni jambo baya kupewa fedha hawa wachanga!unakuwa kama mtu mzee anayefukuzana na mtoto ili amnyanganye kitumbua alichopewa na dada yake. Angalia,usije ukawa Rais wa Tanzania siku moja ukaanza kufukuzana na wananchi eti kwa kuwa wanafanikiwa.Furahi pale vyama vya siasa vinapopata nguvu ya kushindana na hicho chako kwa kuwa matokeo ni MAENDELEO ya Tz.Vyama hafifu vya upinzani matokeo yake ni kufisha ushindani na mwisho nchi inakosa maendeleo.

USHAURI: 1.Acha kabisa wazo la kwenda mahakamani kutoa ushahidi huo kwani utakudhalilisha hata kama ni wa kweli!
2.Huyo anayekushauri kwenda mahakamani anakushauri vibaya ili apate kitu kwako.achana naye.
3.Unashauriwa hata wewe uwachangie hao unaosema wanafadhiliwa ili waweze kuwa na nguvu ya kushindana na wewe ili mchezo(siasa) unoge.Siasa za ushindani ndizo zilizoko sokoni sasa na hakuna jinsi nyingine!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!


From: mngonge <mngonge@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, September 14, 2012 4:59 PM
Subject: Re: [wanabidii] CHADEMA WAMBURUZA NAPE MAHAKAMANI

Inaelekea Nape kaanza kutapatapa, binafsi nilimuona kwenye runinga
akisema anao ushahidi wa kutosha na kwamba kama ni mahakamani Chadema
waende. Si mara ya kwanza kusikia maneno kama hayo toka CCM. Wakati wa
uchaguzi mdogo Igunga walisema Chadema imepeleka vijana nchi za nje
kujifunza kupigana. Swali ilikuwaje serikali isichukue hatua kama ina
taarifa hizo? Hayo na mengine mengi yanayofanana na hayo
wamekwishaongea sana

Nafikiri umefika wakati kwa wanasiasa kuacha kuropoka hovyo kama
hakuna ushahidi wa kutosha. Nape acha woga kabiliana na kesi yako
kusanya vielelezo vyako ukavionyeshe mahakamani si unavyo?

Huu ni mtihani mkubwa kwa CCM maana ikidhibitika kiongozi mkubwa kama
Nape ni mropokaji basi sura nzima ya chama itakuwa imechafuka.
Mtajioshaje na sabuni gani ili mtakate mbele ya watanzania?

2012/9/14 Mathias Lyamunda <mathias.lyamunda@gmail.com>:
> Kauli alizotoa Nape zilikuwa ni za kupaka matope chadema, chadema ina
> uhusiano na chama tawala cha ujerumani na hilo liko wazi iama ccm ilivyo na
> uhusiano na vyama vingine na huwa inasaidiwa pia! Nape alichokisema ni
> kwamba tunapokea mabilioni kutoka nchi za nje, na kwamba tunauza nchi! Hiyo
> kauli ni zito sana haiwezi kuachwa hewani!
>
> On Sep 14, 2012 8:05 AM, "Jonas Kiwia" <jonaskiwia39@gmail.com> wrote:
>>
>> Taarifa nilioipata hivi punde tooka Radio One Stereo.Nimesikia Tundu Lissu
>> akisema wamepeleka kesi mahakamani ili Nape akaeleze ukweli juu ya kauli
>> alizotoa juu ya Chadema kupokea hela tooka wafadhili.
>>
>> Nape alipoulizwa na mwandishi wa habari wa Radio One alisema anarudia
>> kusema Dr Slaa anazeeka vibaya kwa sababu alimsikia akisema mwenyewe ni
>> kweli Chadema inapata helakutoka kwa wafadhili sasa iweje wampeleke
>> mahakamani alihoji Nape.
>>
>> Tungoje tusikia yatakayojiri Mahakamani.Maana kauli anazozitoa na
>> kuzisimamia Tundu Lissu hua si za kubahatisha.Sasa sijui kwa mwenzetu Nape?
>> Jonas Kiwia  |  Director
>> Speedy Computers
>> Tel:+255 754882825  |  Cell: +255 715882825 |
>> P.O.Box: 55133  |  Dar esSalaam  |  Tanzania
>> Email:jonaskiwia39@gmail.com  URL:www.speedycomputersonline.com
>>
>>
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment