Friday 14 September 2012

Re: [wanabidii] CHADEMA MWANZA WAPELEKANA MAHAKAMANI

Na ikiletwa na Juma Mzuri!
 


From: paul lawala <pasamila292000@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, September 14, 2012 12:04 PM
Subject: Re: [wanabidii] CHADEMA MWANZA WAPELEKANA MAHAKAMANI

Kumbe ni kutoka habari leo!

2012/9/14 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>:
> DIWANI wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata ambaye amevuliwa uanachama
> na Kamati Kuu ya Chadema, amewasilisha mahakamani zuio la kutekelezwa
> kwa uamuzi huo.
>
> Matata aliwasilisha hati ya kuomba Mahakama izuie uamuzi huo wa
> Chadema jana, kwa madai kuwa umekiuka Katiba ya chama hicho.
>
> Akizungumza jana baada kuwasilisha hati hiyo mahakamani, Matata alidai
> kuwa kabla ya uamuzi huo wa Kamati Kuu, alipaswa kujadiliwa na Kamati
> ya Utendaji ya Wilaya na Mkoa.
>
> "Hakuna mwenye ubavu wa kuzuia Mahakama kufanya uamuzi, wanapaswa
> kuheshimu uamuzi wa Mahakama … mimi nimechaguliwa na watu zaidi ya
> 3,000, Kamati Kuu yenye watu 20 haiwezi kunyima haki watu wangu
> walionichagua kutokana na majungu ya wachache," alidai.
>
> Alidai kushangazwa kuona kuwa Kamati Kuu inatoa uamuzi wa kumvua
> uanachama kabla ya kujadiliwa katika ngazi ya wilaya na mkoa.
>
> Matata alidai kuendelea kupigania haki yake ya msingi kwa mujibu wa
> Katiba ya chama hicho na kueleza kuwa uamuzi wa kumfukuza ulikuwa
> kinyume cha Katiba ya Chadema na ulilenga kumdhoofisha kisiasa,
> kutokana na viongozi wa ngazi za juu na wabunge wa chama hicho
> kumhofia kisiasa.
>
> Mbali na kwenda mahakamani, Matata pia alitangaza nia yake ya kuwania
> umeya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela.
>
> Matata alidai kuwa chokochoko dhidi yake zilianza mapema, baada ya
> kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka juzi ambapo alichukua fomu ya
> kuwania umeya wa Jiji la Mwanza, lakini Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
> Willibrod Slaa aliamua kupindisha Katiba ili kumwengua.
>
> Alidai kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Meya anapaswa kuchaguliwa
> na kamati tendaji za wilaya na mkoa, baada ya kupigiwa kura, lakini Dk
> Willibrod Slaa na baadhi ya wabunge wa chama hicho, waliingilia kati
> na kumpendekeza meya aliyetimuliwa, Josephat Manyerere.
>
> Mbali na Matata, Diwani wa Kata ya Igoma, Adam Chagulani (Chadema)
> amelazimika kusitisha mkutano wake wa hadhara wa kuelezea wananchi
> wake sakata la kuvuliwa uanachama, baada ya kudai kuwa Mbunge wa
> Nyamagana, Ezekiah Wenje (Chadema), amekuwa akitumia watu kumfanyia
> vurugu.
>
> Alidai baada ya kutangazwa kuvuliwa uanachama, alifanya mkutano na
> wananchi wake kuwaelezea kilichotokea na uamuzi ambao atachukua.
>
> Chagulani alidai kuwa ingawa polisi walisitisha mkutano, kabla ya hapo
> Wenje alikuwa amepeleka wapambe wake kutoka mjini kwenda Igoma kwa
> kukodi magari na kuwanunulia 'viroba' ili wafanye fujo.
>
> Hata hivyo, Wenje akizungumza kwa simu na gazeti hili alielezea
> kushangazwa na tuhuma hizo kwani yeye aliondoka Mwanza tangu Septemba
> 7, kushiriki kikao cha Sekretarieti na Kamati Kuu na bado hajarudi.
>
> Naye Arnold Swai anaripoti kutoka Moshi, kwamba Mkuu wa Mkoa wa
> Kilimanjaro, Leonidas Gama amepinga safari ya madiwani wa Manispaa ya
> Moshi inayoongozwa na Chadema kwenda Kigali, Rwanda kwa madai kuwa
> bajeti iliyotengwa ya Sh milioni 123 ni kubwa.
>
> Gama alitoa uamuzi huo jana, wakati akizungumza kwenye kikao cha
> Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, kilichohudhuriwa na madiwani hao
> na baadhi ya wakuu wa idara wa Manispaa ya Moshi.
>
> Kwa mujibu wa Gama, safari hiyo haina tija, endapo watatumia kiasi
> kikubwa cha fedha hizo. Alisema madiwani kwenda kujifunza ni jambo la
> msingi lakini si kutumia fedha nyingi kiasi hicho, ambazo ni kodi za
> wananchi wanaohitaji maendeleo.
>
> "Si kwamba nawakatalia lakini nasema safari kama hii ya wakati mmoja
> na mara moja tu kwa mwaka, siwezi kuikubali kutokana na matumizi
> makubwa ya fedha, wakati shida za wananchi hapa ni nyingi, kama
> mnataka, basi waende wachache watumie Sh milioni 20, hapo sina
> pingamizi," alisema Gama.
>
> Alisema kabla hajamshauri Waziri husika kutoa kibali cha kuwaruhusu
> kusafiri nje ya nchi ilibidi ajiridhishe kwanza na ndipo alipobaini
> kuwapo kwa kasoro ambazo ni kikwazo cha safari hiyo.
>
> Gama alisema moja ya matatizo ni msafara wa watu 57 wanaotarajiwa
> kwenda Kigali kwa siku saba huku malipo ya posho zao yakionesha
> watalipwa siku tatu, jambo ambalo si sahihi.
>
> Alieleza, kwamba kutokana na msafara huo zaidi ya Sh milioni 200
> zingetumika na kuagiza waende wachache, ili fedha zingine zitumike kwa
> maendeleo.
>
> Meya wa Manispaa hiyo, Japhary Michael (Chadema) alisema anashangazwa
> na uamuzi wa Gama kupinga safari hiyo wakati ipo kikanuni na kulaumu
> kitendo cha kuzungumzia suala hilo kwa vyombo vya habari.
>
> Michael alisema wamekubaliana vizuri na uamuzi uliotolewa na Gama na
> hawana pingamizi juu ya hilo, lakini alieleza kuwa ushauri huo
> wangepewa kwenye vikao vya ndani na si mbele wanahabari.
>
> Chanzo: HabariLeo
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment