Saturday 15 September 2012

Re: [wanabidii] Bendera Ile Ya Taifa Kijijini Mtandika, Tafakari...

Nakubaliana nawe kwa asili mia moja. Nchi/utaifa unatakiwa uwekwe mbele
kwanza. Wiki mbili zilizopita niliona mikutano ya vyama vya Democrats na
republicans imesheheni bendera za nchi yao badala ya bendera za vyama
vyao; wala sidhani wana bendera za vyama vyao, ila wana logo za vyama
vyao. Wanatanguliza utaifa wao kwanza. Ziko nchi nyingi duniaini ambapo
vyama vya siasa vinafanya hivyo. Sipingi Vyama kuwa na bendera zao lakini
basi watangulize taifa kwanza.




> Ndugu zangu,
>
>
> Ni kweli, Watanzania tunaendekeza sana siasa za vyama na kuiasahau
> Tanzania
> yetu. Leo asubuhi sana niliianza safari yangu kutoa Msamvu , Morogoro kuja
> Iringa. Ni kawaida kando ya barabara kwenye makazi ya watu au vibanda vya
> biashara kukuta ikipepea, ama, bendera ya CCM, Chadema, CUF, Simba au
> Yanga. Lakini, ni nadra sana kuiona ikiperushwa bendera ya taifa letu.
>
> Leo pale kijijini Mtandika, nje kidogo ya Ruaha Mbuyuni niliona kwenye
> banda moja la biashara ikipepea bendera ya taifa. Nilishtuka kuiona ,
> niliguswa pia. Nlipunguza hata mwendo kumwangalia kijana yule aliyekuwa
> akifanya biashara yake ya vitunguu huku bendera ya nchi yake ikipepea.
>
> Maana, bila shaka kijana yule kwa mapenzi ya nchi yake aliitafuta mwenyewe
> bendera ile ya taifa. Kwa vile, unapoona mahali kuna vijana wanapeperusha
> bendera za vyama yaweza kuwa na tafsiri ya ama, ni wapenzi wa vyama hivyo,
> na kuwa wamezitafuta wenyewe, au kuna kada wa chama husika aliyekuja na
> kugawa bendera hizo kwa vijana hao.
>
> Ndio, tunahitaji kufanya jitihada za kuwafanya watu wetu waipende nchi yao
> waliyozaliwa, kutoka ndani ya mioyo yao. Na moja ya jitihada hizo ni
> kuwapa
> maarifa yatakayowawezesha kujitambua, kujiamini na kuthubutu.
>
> Maggid,
> Iringa.
> 0788 111 765.
> http://mjengwablog.com
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
> be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
> --
> This message has been scanned for viruses and
> dangerous content by MailScanner, and is
> believed to be clean.
>
>



--
This message has been scanned for viruses and
dangerous content by MailScanner, and is
believed to be clean.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment