Saturday 15 September 2012

Re: [wanabidii] Bendera Ile Ya Taifa Kijijini Mtandika, Tafakari...

Naweza kusema kwamba moyo wa kutoidhamini bendera yetu umeletwa na
mfumo wetu wa siasa tangu enzi ya mlm Nyerere. Mzee Nyerere aliyafanya
mazuri mengi lakini pia kuna mabaya aliyafanya. Tatizo viongozi wetu
hawakukaa chini na kuyachambua mabaya na mazuri ili tuyaendeleze
mazuri na mabaya kuyarekebisha. Yeye mwenyewe katika hotuba zake
alisema bahati mbaya wameyachukua mabaya na kuyaacha mazuri

Utamskia kiongozi toka serikalini kila anasema lazima ataje serikali
ya chama tawala (CCM) hii inatukuza uanasiasa badala ya uzalendo wa
nchi. Ni nadra sana kumsikia rais wa nchi kama Ufaransa, Marekani,
Uingereza au China akitaja habari ya serikali ya chama tawala labda
uwe ni mkutano wa kisiasa. Siku zote utasikia wanasema serikali ya
Uingereza, Marekani, Ufaransa, China nk. Kwa sababu wanautukuza
uzalendo wa nchi zao.

Tusitegemee kuvuna mchicha wakati tunapanda bhangi' Bendera ya taifa
tangu enzi ya mwalimu Nyerere ilionekana kama mzimu fulani, ukionekana
umevaa nguo yenye rangi kama za bendera ya taifa ungepelekwa jela.
Ukionekana na nguo yenye rangi za vazi la maafande hapo utapigwa hadi
basi. Bendera za TANU na baadaye CCM zilizagaa kila kona hasa hasa
kwenye nyumba za wajumbe wa nyumba kumi. Siku hizi ndo hivyo tuna
vyama vingi na matawi yanafunguliwa kila kona ata kwenye vijiwe vya
wavuta bhangi. Kiongozi wa chama kwa wakati ule hakutofautishwa na
kiongozi wa serikali, chama kilishika hatamu na hadi leo ndiyo mapokeo
yaliyopo.

Wakati umefika wa kubadilika na kuanza kuiona bendera yetu ya taifa ni
muhimu kuliko za vyama vya siasa na vilabu vya mipira. Hiyo haitakuwa
kazi nyepesi mpaka pale viongozi wetu watakapoliona hilo na kulifanyia
kazi ata kuliingiza kwenye mitaala ya ngazi mbalimbali za elimu.

Kwa vile sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kurekebisha katiba yetu ni
vyema tuliangali swala zima la uzalendo kwa nchi yetu. Mfano kwa sasa
cheo cha mjumbe wa nyumba kumi hakieleweki kwa watanzania. CCM
imeendelea kukiona kama cheo cha kichama na hivyo ata pale ambapo kuna
wanachama wawili wa CCM na walibaki ni vyama vingine au hawana vyama
bado tuna mtu anaitwa mjumbe lakini toka CCM.

Nionavyo mimi cheo hicho ni muhimu kuwepo kwa vile kina sababu ya
kuwepo lakini kitambulike kama cheo cha kiserikali na mjumbe
achaguliwe bila kuangalia ana chama au la. Huo utakuwa mwanzo mzuri wa
kuutukuza uzalendo na kuipeperusha bendera ya taifa tangu ngazi ya
chini kabisa. Sijui ni kwa kiasi gani walimu wetu wanaofundisha shule
za msingi na sekondari tunawaandaaje kuwafundisha uzalendo kwa watoto
wetu. Siku hizi ni nadra sana kumsikia mtoto akiimba wimbo wa taifa au
ule wa Tanzania nakupenda. Kwa vyovyote vile kuna mahali tumebugi
stepu


Je sisi wazazi na umma kwa ujumla tunaonyesha mifano gani kwa vijana
wetu? Viongozi wetu hasa hasa toka chama tawala wana mikakati gani ya
kuepuka mapokeo ya kukitukuza chama zaidi badala utaifa kwanza? Hayo
ni baadhi ya maswali ambayo majibu yake yanaweza kutufungulia njia ya
kuupenda na kuutukuza utanzania





2012/9/15 maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>:
> Ndugu zangu,
>
>
> Ni kweli, Watanzania tunaendekeza sana siasa za vyama na kuiasahau Tanzania
> yetu. Leo asubuhi sana niliianza safari yangu kutoa Msamvu , Morogoro kuja
> Iringa. Ni kawaida kando ya barabara kwenye makazi ya watu au vibanda vya
> biashara kukuta ikipepea, ama, bendera ya CCM, Chadema, CUF, Simba au Yanga.
> Lakini, ni nadra sana kuiona ikiperushwa bendera ya taifa letu.
>
> Leo pale kijijini Mtandika, nje kidogo ya Ruaha Mbuyuni niliona kwenye banda
> moja la biashara ikipepea bendera ya taifa. Nilishtuka kuiona , niliguswa
> pia. Nlipunguza hata mwendo kumwangalia kijana yule aliyekuwa akifanya
> biashara yake ya vitunguu huku bendera ya nchi yake ikipepea.
>
> Maana, bila shaka kijana yule kwa mapenzi ya nchi yake aliitafuta mwenyewe
> bendera ile ya taifa. Kwa vile, unapoona mahali kuna vijana wanapeperusha
> bendera za vyama yaweza kuwa na tafsiri ya ama, ni wapenzi wa vyama hivyo,
> na kuwa wamezitafuta wenyewe, au kuna kada wa chama husika aliyekuja na
> kugawa bendera hizo kwa vijana hao.
>
> Ndio, tunahitaji kufanya jitihada za kuwafanya watu wetu waipende nchi yao
> waliyozaliwa, kutoka ndani ya mioyo yao. Na moja ya jitihada hizo ni kuwapa
> maarifa yatakayowawezesha kujitambua, kujiamini na kuthubutu.
>
> Maggid,
> Iringa.
> 0788 111 765.
> http://mjengwablog.com
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment