Tuesday 11 September 2012

Fw: Re: [wanabidii] TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA DHIDI YA MAUAJI YA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI

WAZO langu kwa CDM. Historia inaonyesha chama tawala kimetumia mbinu nyingi huko nyuma kudhoofisha vyama vya upinzani. Vyama hivyo ni NCCR (Mageuzi) na CUF. Na katika kujaribu kutumia mbinu hizo hizo kwa CDM kimegonga mwamba. baadala yake kikaamua kutumia mbinu ambayo naweza kuita "LAST RESORT STRATEGY" Kuua kwa gharama yeyote. Nia ni kutengeneza mazingira ya uwoga kwa watanzania. Ushauri wangu kwa CDM ni kutotengeneza mazingira ya kuonyesha wamefanikiwa baada ya kusababisha haya mauaji. Ni kwamba CDM msionyeshe hali ya KUTAHARUKI kupita kiasi au niseme mnatakiwa KU-REACT BUT DO NOT ALLOW TO OVER-REACT. Maana hiyo itakuwa indicator mojawapo ya wao kuhesabu mafanikio. CDM mnakiwa ku-react halafu operate under low-profile while you maintain your "STAND" au UJASIRI. Maana katika mapambano kwenye uwanja wa vita wakati mwingine unaruhusiwa kumkabiri adui hata kwa kukanyaga maiti na akiona hivyo atajua huyu adui ni JASIRI. Maintain your profile tell people you are united with them and you are not responsible with any killing. I repeat DO NOT OVER-REACT. COOL DOWN, PLAN, MAKE DECISION without affecting any innocent CDM member who strongly support you. To them this has been the last weapon in their barracks/store. If you can stand this! They won't have any other alternative apart from accepting DEFEAT! Time for downfall is arround the corner. 

--- On Mon, 9/10/12, paul lawala <pasamila292000@gmail.com> wrote:

From: paul lawala <pasamila292000@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA DHIDI YA MAUAJI YA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, September 10, 2012, 4:50 AM

Huu msamiati "nguvu kupita kiasi" siuelewi na inawezekana haueleweki
hata kwa polisi, nauliza nguvu kiasi inapimwaje?

2012/9/6  <fatma_elia@yahoo.com>:
> Nimelipenda tamko hili. Kwa kweli kilichosemwa hapa ndicho kinachotakiwa kifanyike na sio tu nyimbo za Amani na Utulivu huku raia wasio na hatia wakiendelea kukatishwa maisha na waliowekwa kuwa walinzi wa Amani na Utulivu
> Hongera Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba kwa kuliona hilo mapema kabla hawajatumaliza soote manake huko ndiko tunakoelekea
>
> Fatma
>
> Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
>
> -----Original Message-----
> From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Thu, 6 Sep 2012 08:05:42
> To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
> Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: [wanabidii] TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA DHIDI YA MAUAJI YA
>  MWANDISHI DAUDI MWANGOSI
>
> TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA DHIDI YA MAUAJI YA MWANDISHI DAUDI
> MWANGOSI
> ''Mauaji Ya Waandishi Na Wananchi YatavurugaMchakato Wa KupataKatiba
> Mpya Tanzania!''
>
> JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumepokea taarifa za kuuawa kinyama
> kwaMwandishi Daudi Mwangosi wa Channel 10na Mwenyekiti wa Chama cha
> waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) kwa mshtukona masikitiko
> makubwa. Kama ilivyokwishaelezwa na wengi, kifo cha mwandishi huyu ni
> cha kwanza cha aina yake katika tasnia ya habari nchini na kinatishia
> si tu uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa habari kwa ujumla wake, bali
> pia kifo hiki na vingine vya siku za karibuni vinauweka mchakato wa
> Katiba Mpya njia panda. Vitendo vya mauaji ya raia vinazidi kushamiri
> siku hadi siku. Wapo wananchiwanaouawa na watu wanaoitwa wenye hasira
> kali kwa tuhumaza uhalifu. Wapo raiawanaouliwa na majambazi na
> wahalifu wenginekwa sababu ya ulinzi duni katika maeneowanayoishi.
> Aidha, wapo pia wananchi wanaopoteza maisha yao kila siku kwa tuhuma
> za kwamba ni wachawi.Ukiacha hao, idadi kubwa ya watanzania wanaishi
> na ulemavu wa ngozi wamepotezamaisha kwa kukatwa viungo au kuuliwa
> kabisa kwa imani za kishirikina. Hali sasa imefikia kuwa mbaya hadi
> kuna watanzania wanajisikia salama zaidi wakiwa mwituni kuliko
> majumbani. Yote haya yanasikitisha sanakwa ujumla wake! Haki ya kuishi
> inayowekwa na kulindwa na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
> wa Tanzania imeanzakuingia dosari katika Tanzania.Ukiacha mauaji
> yanayofanywa na watu wasiojulikana au miongoni mwa raia, yamekuwepo
> pia mauaji yanayozidi kuongezeka ya raia yanayofanywa na wawekezaji au
> matajiri nchini. Zipo kesi kadhaa za mauaji ya namna hii.
>
> Hayo nayo yamekuwa yakitokea kwa sababu ya ulinzi mdogo ambao wananchi
> wanao kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Jeshi la Polisi,
> ambalo ndio lenye dhamana ya kulinda watu na mali zaohaliwezi kukwepa
> lawama katika aina zote hizo za mauaji. Itakumbukwa pia kuwa ajali za
> magari, mabasi na meli zinagharimu sanamaisha ya watanzania katika
> siku za karibuni. Kwa kiasi fulani, hata kukithiri kwa ajali hizi nako
> kunahusishwa na mwenendo mbovu wa usimamizi wa vyombo vya usafiri
> unaofanywa na idara mbalimbali za serikali ikiwemo kikosi cha usalama
> barabarani. Roho zawatanzania zinazidi kupotea kutokana na udhaifu
> mkubwa unaosababishwa na rushwa na mambo mengine ya ukosefu wa maadili
> katika vyombo vya usimamizi wa haki. Mauaji ya raia yanayofanywa moja
> kwa moja naaskari wa Jeshi la Polisi nayo yanazidi kuongezeka
> sanakiasi cha kutishia amani na utulivu wa nchi yetu. Aidha, mauaji
> yanayohusishwa na siasa nayo yanazidi kuongezeka na kuzidisha chuki ya
> kisiasa ambayo ni mbaya sana kwa ustawi wa nchi yetu. Kwa mfano katika
> miezi ya Karibuni, kumekuwepo matumizi ya nguvu kuzidi kiasi kwa raia
> wanaokuwa wakipanga na kufanyamaandamano au mikusanyiko yenye lengo la
> kujadili au kupinga jambo fulani. Matokeo yake, kumetokea majeruhi na
> mauaji ambayo yamesababishwa na vurugu ambazo zinatokana na Jeshi la
> Polisi kudhibiti vitendo halali vya wananchi. Kwasababu hiyo, JUKWAA
> LA KATIBA TANZANIA tunatoa witoufuatao kwa Jeshi la Polisi na idara
> nyingine za serikali zenye dhamana ya kulinda usalama wa raia, malina
> mipaka ya Nchi yetu:
>
> 1.1. Jeshila Polisi liache kutumia nguvu kuzidi kiasi katika matukio
> yote ya kulinda mikutano na matukio ya hadhara. Tujuavyo sisi, Jeshi
> la Polisi linalotumia risasi za moto, mabomu ya kivita, maji ya
> kuwasha na gesi ya kutoa machozi dhidi ya raia ambao hawajabeba hata
> fimbo za kuchungia mifugo. Ni Jeshi lisilojiamini na linaloonesha woga
> wa ajabu. Kwa hadhira kama za Nyololo, Morogoro, Mbeya, Dar es Salaam
> na nyinginezo miezi yaKaribuni, Jeshi la Polisi lingeweza kuwatuliza
> wananchi kwa kutumia filimbi tu. Matumizi ya nguvu na kumwagia maji ya
> kuwasha hata wazee wastaafu wanaodai haki zao inaweza kuwa ndio laana
> inayopelekea Polisi kusikia furaha kuua kila mara. Ipo kanuni ya
> kimataifa inayowataka Polisi kutumia nguvu kidogo sana inayolingana tu
> na nguvu ya umma wanaokabiliana nao katika kutuliza ghasia.
>
> 2.Wakati huu wa mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania na
> hata baada ya hapo, Jeshi la Polisi lijiepushe kuingilia shughuli za
> Kisiasa kwa kuziunga mkono au kuzivuruga. Mikusanyiko mingi ambayo
> imepelekea mauaji wakati polisi ikijaribu kuivunja ni matukio
> yaliyolenga kupata majibu ya kisiasa na siyo ya kipolisi. Wajibu wa
> Jeshi la Polisi
>
> katika wakati kama huo ni kulinda na kuwezesha wananchi husika kueleza
> madaiyao kwa uhuru na bila kuvurugwa na kundi jingine lolote la watu
> wasiopendezwa na madai ya kundi husika. Tabia inayozidi kushamiri ya
> Jeshi la Polisi kutaka kujibu au kuzima hoja za Kisiasa au kiuchumi
> kwa mtutu wa bunduki, mabomu, maji ya kuwasha na virungu ni tabia ya
> Jeshi kutaka kuingilia kazi isiyo yake na ndio maana inawashinda.
> Aidha, kama Polisi wangekuwa niwataalam wa Siasa, wangegundua kuwa
> wanachokifanya ni kuahirisha matatizo na si kuyatatua!
>
> 3. Jeshi la Polisi na vyombo venye dhamana ya ulinzi vijitambue upya
> kuwa vina wajibu wa kulinda raia, mipaka na mali zao si vinginevyo.
> Mauaji yanayoendelea nchini ni uporaji wa haki ya kuishi na haki
> nyingine nyingi chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana
> ile ya Zanzibar.Aidha, Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla wana
> wajibu wa kuhakikisha na kudumisha ustawi wa wananchi kwa mujibu wa
> ibara ya 8 (1) (b) nahawana mamlaka ya kuua raia. Ikumbukwe kuwa
> mamlaka yote kikatiba katika Tanzaniayako kwa wananchi na serikali
> pamoja na Jeshi lake la Polisi watapata madaraka na mamlaka hayo
> kutoka kwa Wananchi. Nani amewapa Polisi mamlaka ya kuua watanzania?
> Nani amewapa Jeshi la magereza mamlaka ya kuwapiga na kumwaga damu za
> Waandishi? Nani amewapa askari wanyamapori mamlaka ya kupiga risasi
> hovyo nakuua ng'ombe mbele ya wenye maliyao?
>
> 4.Athari za matukio ya mauaji na fujo zinazosababishwa na Jeshi la
> Polisi kutawanya waandamanaji au mikusanyiko mingine ni kubwa sana
> katika kuathiri vibaya hamasa ya wananchi kwenye Mchakato wa Katiba.
> Mpaka sasa, tayari watu wengi wameingia wasiwasi na wameamua
> kutoshiriki mikutano ya kutoa maoni ya Katiba inayoendeshwa na Tume ya
> Mabadiliko ya Katiba nchini. Endapo Jeshi la Polisi halitaacha kuua na
> kutishiaraia kwa kila wanachokifanya, mchakato wa Katiba utavurugika
> kabla Katiba mpya haijapatikana. Kwa mwenendo wa sasa, Jeshi la Polisi
> litakuja kupiga mabomu na kuua hata wananchi watakapokuwa katika
> Mabaraza ya Katiba wakijadili na kupinga baadhi ya vipengele
> vitakavyoingizwa katika rasimu ya Katiba. Pia, itafika wakati wananchi
> watataka kuandamana kwa amani kuunga mkono au kupinga mambo Fulani
> katikaKatiba. Kwa hali ilivyo, Jeshi la Polisi litaona hiyo ni fursa
> ya kutumia mabomu na risasi kuzuia wasiseme wanayotaka kusema. Hii ni
> hatari kubwa sana!
>
> 5. Mikusanyiko, maandamano na shughuli za mikutano ya Siasa ni matendo
> halali na haki ya kila mtanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
> Muungano, 1977 ibara ya 8, 20 na 21. Suala la kutoa taarifa kwaJeshi
> la Polisi kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Polisi ni suala la
> kuwajulisha tu kwa lengo la kuwaweka tayari endapo kutahitajika msaada
> wa Jeshi la Polisi wakati wa shughuli kamahiyo. Tabia iliyoota mizizi
> ya Polisi kujiona kama wamepewa taarifaili watoe au kukataa kibali ni
> uelewa finyu wa Katiba na sheria za Nchi. Ipo haja ya kuongeza uelewa
> wa wasimamizi wetu wa sheria ili wawe na uelewa mpana wa sheria na
> ibaraza Katiba wanazozisimamia badala ya kujiona kama wana wajibu wa
> Msajili wa vyama vya Siasa wa kuratibu shughuli za vyama. Mikutano,
> mikusanyiko, mihadhara, maandamano na mijadala ni haki ya Kikatiba ya
> Kila mtanzania binafsi na kwa makundi. Kwa kuwa haki ya kuishi
> iliyoporwa kwa MwandishiDaudi Mwangosi ndio haki kubwa kuliko zote,
> JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunataka jambo hili lisiishiekuunda Tume za
> uchunguzi pasipo kufanyia kazi mapendekezo yake. Aidha, kwa kuwa
> uchunguzi unaofanywa hauhusiani na kilichomuua ndugu Mwangosi wala
> kundi gani limemuua, tunapendekeza busara itumike kwa viongozi wa
> Jeshi la Polisi, kuanzia Kamanda wa Polisi Mkoawa Iringa kuachia ngazi
> ili kupisha uchunguzi huru wa Tume itakayoundwa na Mheshimiwa Rais
> ikihusisha na kuongozwa na mhimili wa Mahakama. Taarifa ya uchunguzi
> ipelekwe Bungeni na Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kujadiliwa na ushauri
> wa kibunge. Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
> tunaitamka rasmi kuwa batili kwa kutumia kanuni ya sheria za kiasili
> inayosema kuwa mtu au kundi hawezi kuwahakimu wa kesi inayomhusu
> mwenyewe. Bila kufanya hivyo, tunapata wasiwasi kama Tume ya namna
> hiyoinaweza kufanya kazi yake kwa uhuru. Kuachia ngazi kwa Kamanda wa
> Polisi mkoani Iringa kutakuwa ishara kuwa Jeshi la Polisi linahitaji
> kuwa makini zaidi katika kufanya kazi yake ya kulinda amani, mali na
> maisha ya watanzania. Kwa sasa, zipo hisia kuwa Jeshi la Polisi lipo
> juu ya sheria na Katiba, jamboambalo tunapenda kulikanusha vikali!
>
> Mwisho, tunapenda kutoa rai kwa serikalikutangaza rasmi kuwa itachukua
> jukumu la kutunza, kusomesha, kulisha na kuhudumia familia aliyoiacha
> Daudi Mwangosi kuanzia sasa kwa muda wa miaka 20 watakapoweza
> kujitegemea wenyewe. Itakuwa ni fedheha kuiona familia aliyoianzisha
> Marehemu Mwangosi ikisambaratika kwa sababu kichwa cha nyumba hiyo
> kimesambaratishwa na bomu la Polisi ambalo kodi yake
> Mwangosiilichangia kulinunua. Kufikia hapa, tunapenda kutangaza rasmi
> kuwa msiba huu nimsiba wa KIKATIBA na tunaomba ufahamike hivyo kwa
> umma wote wa watanzania na kote duniani.
>
> Mungu ailazeroho ya Marehemu Mwanahabari Daudi Mwangosi mahali pema
> peponi Amina!
>
> Imetolewana kusainiwa kwa niaba ya JUKWAA LA KATIBA TANZANIA,
> Deus MKibamba
> Mwenyekiti
> Alhamis, 06 Septemba 2012
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment